Moja tu - Amechukua u CEO pakiwa na hasara ya 162bn kwa mujibu wa audited accounts za 2006. 2007 hasara ilishuka mpaka 67bn. 2008 imeshuka mpaka 30bn na mpaka june 2009 tayari TANESCO ilikuwa imebreak even. Kama sio mgawo wa Septemba, Oktoba na Novemba wangepata faida mwaka huu.
Mbili - kwa mara ya kwanza Taasisi za fedha zimekopesha TANESCO 400bn na wana service mkopo huo bila tatizo lolote na hivyo kuweka mazingira ya kukopa zaidi.
Huna sababu ya kusingizia watu ushallow nenda kwenye hoja straight. Inamaana bei ya umeme imeongezeka kipindi cha Rashid tu? Mbona hatukuona TANESCO inaimarika kipindi cha NET solution au kipindi kingine wakati bei zikipanda?Na hilo ongezeko ukilinganisha na ongezeko la gharama za uendeshaji huoni? Umecheki vizuri aspect za costs na revenue?Au unakimbilia kwenye revenue unasahau expenses nazo huongezeka. Revenue zimeongezeka kutokana na msisitizo wa makusanyo, kuzidi kuwaunganisha watu na kubanya mianya ya upotevu wa pesa. Unaifaham ishu ya kiwanda cha cement, kampuni ya simu na mashirika mengine yaliyokuwa hayalipi ankara zao. Accounting practices kwa Tanzania zimebadilika tokea mwaka 2004 kwahiyo hapo sijaona hoja ya kucritisize performance. Hata zile ambazo on going changes zinakuwa reflected kwene notice za financial statements zinakagulika labda njoo na lingine kwa hapo.Zitto
mbona uko shallow hivyo? Hiyo hasara iliyopunguzwa uliomba kupata detailed schedule kujua ni ongezeko la Revenue au kupungua kwa gharama za uendeshaji kabla ya conclude?Kwa mfano kama malipo ya Richmond yalisimamishwa na unacompare vipindi hivyo viwili lazima utaona tofauti.je bei ya umeme iliongezwa? kwenye uhasibu tunaita analytical Review sio unakurupuka tu nakusema ooh hasara imeshuka kwa hiyo rashid ni mkurugenzi mzuri jiulize what were the factors leading to that?je accounting procedures zimebadilishwa.. kwa mfano unaweza kukuta kuna vitu vilikuwa vinakuwa expensed sasa viko capitalized wher u just charged depreciation in the PL kwa bottom line number inaonekana nzuri,kuna mambo mengi ....inabidi ujue accounts...... Yani mtu anahusika kuchannel pesa za rada unamwita best CEO .. anyway haishangazi sasa ... waarabu wa pemba hujuanan kwa vilemba...
hebu thibitisha na habari za mwanahalisi zithibitshe kwa kutueleza namba ya toleo la gazeti. Habari zilizopo mpaka sasa ni zilizotolewa na Raiamwema kwa vithibitisho kwa EPA kuanza mwaka 2000. Ni kweli kulikuwa na debt conversion schemes etc. Thibitisha ufisadi uliotokea huko na tutakubaliana nawe badala ya kutoa sweeping statements.
Halafu tutaenda nyuma kuanzia kwa Mzee Mtei mpaka kina Nyirabu, Rutihinda nk ili kuona hizi schemes zilikuwaje. Pia tutaangalia wakati Benki Kuu inaungua ilikuwa ni nini nk. Yaani tuanze toka wakati wa Mwalimu akiwa Rais na hatua alizochukua, kwa mfano kwa kuungua Benki Kuu. Tusiwe na memory ndogo kwa ajili ya kumhukumu mtu.
On RADAR - nimesema hili ni suala la mahakamani na tushinikize wanaotajwa wapelekwe mahakamani na mahakama ndio pekee zenye mamlka ya kusafisha mtu au kuhukumu. Ingawa najua zitakuja hoja za uhuru wa mahakama nk - maana hata mimi suala la Zombe liliniacha hoi licha ya kuheshimu uhuru wa mahakama.
katika financial reporting, hizo zinaitwa "headline figures" na kazi yake ni ku paint picha nzuri
mpaka ma analyst waone full anual report ndio itajulikana ni nini kimefanyika
kama lukule alivyosema hiyo hasara labda ni kutokana na mkataba wa richmond (na yeye ni mmoja wa wafaidika), na kupungua kwa hasara kunatokana na mkataba kusitishwa. kama ni hivyo, basi hiyo siyo kazi yake bali ni wanasiasa
"taifa litaingia gizani kama mitambo isiponunuliwa" kweli the best ceo hana mipango mingine yeyote ya kulinusuru tanesco zaidi ya generator za dowans
je hizo bil 400 kafanyia nini
Andrew Chenge alijiuzulu kabla ya kufikishwa mahakani ili kupisha uchunguzi huru ufanyike kwa kosa hili la rada, inakuwa vipi iwe tofauti kwa Rashid?
Zitto
mbona uko shallow hivyo? Hiyo hasara iliyopunguzwa uliomba kupata detailed schedule kujua ni ongezeko la Revenue au kupungua kwa gharama za uendeshaji kabla ya conclude?Kwa mfano kama malipo ya Richmond yalisimamishwa na unacompare vipindi hivyo viwili lazima utaona tofauti.je bei ya umeme iliongezwa? kwenye uhasibu tunaita analytical Review sio unakurupuka tu nakusema ooh hasara imeshuka kwa hiyo rashid ni mkurugenzi mzuri jiulize what were the factors leading to that?je accounting procedures zimebadilishwa.. kwa mfano unaweza kukuta kuna vitu vilikuwa vinakuwa expensed sasa viko capitalized wher u just charged depreciation in the PL kwa bottom line number inaonekana nzuri,kuna mambo mengi ....inabidi ujue accounts...... Yani mtu anahusika kuchannel pesa za rada unamwita best CEO .. anyway haishangazi sasa ... waarabu wa pemba hujuanan kwa vilemba...
Kaka nimesema pia kuwa tuna viwango tofauti tunavyoweka kwa wanasiasa na watendaji. Nadhani kama kungekuwa na shinikizo kwa Rashidi kama lililokuwepo kwa Chenge angejiuzulu tu.
Lukule,
kusema nimekuwa shallow ni kunionea tu. Labda useme ninajengea hoja taarifa ambazo sio sahihi nk. Ripoti za fedha ninazo semea hapa ni ripot zenye nyaraka zote kabisa na zilizochambuliwa na wataalamu. Wakaguzi wa TANESCO ni PwC, ambalo ni shirika lenye heshima kubwa katika kazi ya ukaguzi. Kama wao walikuwa shallow na baadaye CAG naye akawa shallow katika ripoti yake basi nitakubaliana nawe.
Nashauri tujadili kwa hoja sio hisia tu kwa kuwa fulani hampendi mtu fulani.
Nimesema hoja ya Radar na hoja tofauti na sijaona hoja hii imeathiri vipi kazi za huyu bwana pale TANESCO. Kwa maoni yangu, narudia maoni yangu na wala silazimishi mtu yeyote akubaliane nami, Rashidi ni mmoja wa maCEO bora kabisa katika Mashirika yetu ya Umma Tanzania.
Gharama zimepungua sana.
Gharama za hovyo hovyo zimeshushwa na zinaendelea kushushwa. Ninadhani nipo priviledged kuwa na taarifa hizo zote. Mafanikio makubwa yaliyopatikana yanatokana pia na kupunguza gharama. Juhudi za kuongeza mapato zimeongezeka zaidi.
Kumalizika kwa mikataba ya Aggreko na makampuni mengine ya kuzalisha umeme pia kumesaidia. IPTL bado gharama zinalipwa katika escrow account iliyopo Benki Kuu na hivyo bado TANESCO hawajaweza kupunguza gharama hii. Majadiliano na IPTL yakiisha na gharama mpya za capacity charge kuamuliwa, itasaidia zaidi.
Sasa nawe unakosea kuconclude kuwa sijui kama ni gharama au mapato kiasi cha kusema nimekuwa shallow. Jenga hoja yako, sio lazima utumie maneno kama hayo. bring facts na tujadiliane kwa facts kuhusu TANESCO kati ya mwaka 2006 na 2009
Kwa maoni yangu, narudia maoni yangu na wala silazimishi mtu yeyote akubaliane nami, Rashidi ni mmoja wa maCEO bora kabisa katika Mashirika yetu ya Umma Tanzania.
Mh Zitto, hili unalosema inawezekana ni kweli. Lakini kama tunataka kuangalia performance yake si vema kuangalia vitabu (audited accounts) peke yake. Je Tanesco ilikuwa na objectives gani katika kipindi tunachozungumzia? Were the objectives reasonable? Je wame'achieve' kwa kiasi gani hizo objectives?
Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa kama jana ulitembea km 5 kwa saa na leo ukatembea km 6 kwa saa kwa hakika performance ya leo ni bora kuliko ya jana (as per the audited accounts!). Lakini kama jana uliahidi (targets, objectives) au 'tulitegemea' kuwa leo ungetembea km 20 kwa saa halafu actually ukatembea km 6 kwa saa, then performance yako ni mbovu kabisa!
Zitto,
Nakukubali sana pale unapolitetea kwa nguvu zako zote jambo ambalo unaliamini kuwa its right, nakushauri sometimes upime utetezi wako kwa public opinion trend usijefika mahali ukaonekana " An Enemy of The People"
Hapa utaona kupungua kwa Gharama ni kutokana na kuisha kwa Mikataba au kusimamishwa kwa Mikataba mibovu na Sio Efficiency ya CEO.Gharama zimepungua sana.
Gharama za hovyo hovyo zimeshushwa na zinaendelea kushushwa. Ninadhani nipo priviledged kuwa na taarifa hizo zote. Mafanikio makubwa yaliyopatikana yanatokana pia na kupunguza gharama. Juhudi za kuongeza mapato zimeongezeka zaidi.
Kumalizika kwa mikataba ya Aggreko na makampuni mengine ya kuzalisha umeme pia kumesaidia. IPTL bado gharama zinalipwa katika escrow account iliyopo Benki Kuu na hivyo bado TANESCO hawajaweza kupunguza gharama hii. Majadiliano na IPTL yakiisha na gharama mpya za capacity charge kuamuliwa, itasaidia zaidi.
Sasa nawe unakosea kuconclude kuwa sijui kama ni gharama au mapato kiasi cha kusema nimekuwa shallow. Jenga hoja yako, sio lazima utumie maneno kama hayo. bring facts na tujadiliane kwa facts kuhusu TANESCO kati ya mwaka 2006 na 2009
Ni lini watanzania wataamua kuwa objective na kujua kuwa matatizo yetu hayatokani na indivuduals bali mfumo mzima? Hata CEO awe malaika kama mfumo mzima wa uendeshaji shirika kwa kutegemea maamuzi ya wanasiasa hautabadilika hatafika popote. Zitto mwenyewe umesema mapema kuwa mikakati mingi ya Dr Rashid haikuweza kuzaa matunda kwa kuwa mwenye hisa ambaye ni serikali hakutoa funds. Hovyo basi hata kama Tanesco itapata the best CEO around (nami maamini wapo wazuri kuliko Dr Rashid Tanzania sema hawako tayari kufanya kazi ambayo hawatepewa kipimo cha haki) bado kwa mfumo tulio nao tutaendelea kuandika kuhusu matatizo ya Tanesco siku nenda rudi
Hapa utaona kupungua kwa Gharama ni kutokana na kuisha kwa Mikataba au kusimamishwa kwa Mikataba mibovu na Sio Efficiency ya CEO.
Angekuwa ni effective sasa hivi tunge isha kuwa na Master Plan ya 5 years, 10 years na 20 years to come.
Kuhusu mwenye hisa kutotoa Fedha za kuwekeza naweza kukubaliana na wewe, lakini yeye akiwa kiongozi wa Shirika hilo akipewa fedha za Kununua Dowans anakubali, badala ya kusema kama ni hizo hela leteni nifanye ninacho ona kina faa, otherwise awaambie kama sivyo siwezi kufanya kazi.
Jingine yeye ni mchumi tena aliye Bobea, sasa mtu unashindwa kuelewa fedha za Mkopo hata kama ni zako, unapowekeza kwenye matumizi ya ukarabati wa nyumba badala ya uzalishaji au vitu vinavyo uhusiana na uzalishaji, kama vipuri, nyaya, nguzo, meter, watu watakuona effectiveness yako ipo chini ya kiwango cha watu wenye busara watakuona unatakiwa kufuata.
good points.
kinachonipa tatizo ni jinsi watu walinvyoline up kuchukua nafasi pale TANESCO ili kufurahisha wanasiasa. Nitawapinga hao kwa nguvu zangu zote. Kuna watanzania waturi wasio na mawaa ambao wanweza kufanya kazi nzuri zaidi ya Rashidi. Kwanza Rashidi yupo katika retirement age. Tatizo hao hawapewi nafasi na wanasiasa, narudi na nieleweke, wanasiasa wanataka kujaza sttoges wao katika mashirika.
Angalia Bodi za mashirika zinazoteuliwa miezi hii inayoelekea uchaguzi halafu pima na ujuvi. Wamegoma kata kata kutekeleza hoja ya CAG kuwa wabunge tusiwe kwenye mabodi. Juzi Shamsa kateua kina Ndugai, Seleli katika Bodi ya NGORONGORO. Ndugai ni mhifadhi. Seleli? hata hivyo wote hao kwa kuwa ni wabunge wangepaswa kutokuwa wajumbe. Mbaya zaidi wote Seleli na Ndugai ni wajumbe wa kamati ya Mali Asili ambayo kisera Bodi ya Ngorongoro inawajibika kwayo. Ndugai ndo mwenyekiti. Mzee Misanga yupo bodi ya TPA na wakati huo huo ni mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu.
Jamani - mtanikosa leo siku nzima maana ninasafiri kwenda Trinidad kwenye Commonwealth. So najua kutakuwa na maswali kibao nitajibu nikifika huko.
Mdondoaji,
..of course suala la Liyumba silielewi vizuri, na ndiyo maana nikauliza maswali kuhusu nafasi ya Contractor na Project Consultant.
..kuhusu suala la Rada una maelezo gani ya kumtetea Dr.Rashidi?
..pia madai kwamba Tume ya Bunge ya Edward Oyombe Ayila ilipendekeza Dr.Rashidi achukuliwe hatua nayo una utetezi gani?