figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 28,058
- 64,206
Mwenye Msitu alifurahishwa na Uchawa wa Tandala, akampa uhuru, akamwambia fanya utakavyo hapa Msituni hakuna wa kukushitaki nitakulinda.
Tandala akaanza kuwanyonyesha watoto wa Nguchiro mmoja mmoja hadi wakafika 19.
Tandala akadhurumu Mafao ya Wanyama wengine.. Mwenye Msitu akawa anaangalia tu..
Tandala akaanza kushambulia Miradi ya mwenye Msitu kwamba anaishi gizani mara 30 kwa siku.
Sasa Tandala kalewa madaraka alopewa na Mwenye Msitu, kaamua kwenda kumtapikia bila kujali chakula na pombe kapewa na mwenye Msitu.
Sasa Tandala Wamejikusanya na Kangoni na Pongo, Wanataka Wamfukuze Mwenye Pori au Wamng'oe meno na kumfunga mdomo asipige Kelele, ikiwezekana Wamfukuze aende kwao Mashariki ya mbali.
Hawajui Mwenye Msitu anamiliki Simba na Chui. Mwenye Msitu akikasirika, Tandala Mtatoroka Msituni na Watoto wenu.
Hata kama Mwenye Msitu ni Mgeni, Tandala wanaweza kurudi India sio kwa Ugonjwa tena bali kuomba hifadhi.
Wanyama Msaidieni Mwenye Msitu kuweka Uzio kwa manufaa ya Vizazi vyenu, Vinginevyo siku itafika mtatafunwa na Uzio utajengwa hata na Nyegere.
Hatapatikana Muhuni tena wa kumfanyia fujo tena Nyegere asiweke Uzio. Msitu wa Wanyama wote. Hata mwenye Msitu atauacha aje mwingine amiliki. Tandala na timu yake hawana cha kumfanya mwenye Msitu zaidi ya Kelele. Kelele za Mlango hazimzuiu mwenye nyumba kulala