Tancut Almasi - Mama

Tancut Almasi - Mama

Je naweza kupata nyimbo yao inayoitwa safari sio kifo.
 
Ipo nyingine inaitwa Ima.
Baadhi ya mashairi yake,
''Ima ni kazi inayotutenganisha, na kazi ndiyo baba wa maisha yetu imaaa, siyo rahisi imaa, nikusahau imaaa, ima iyoleleee mamaa, mwenzio usingizi sipati kwa ajili ya kukuwaza aaa''

Nautafuta sana huu wimbo siajweza kuupata.
 
Nimekutana na huu wimbo umenikumbusha mbali sana, wote wenye mapenzi na mama zao sikilizeni huu wimbo. sauti nzuri za Kyanga Songa na Kasaloo Kyanga wa Tancut Almasi wimbo Mama, pata burudani.....kwa hisani ya wanamuziki wa Tanzania, hongera Mzee Kitine.

<img style="visibility:hidden;width:0px;height:0px;" border=0 width=0 height=0 src="http://c.gigcount.com/wildfire/IMP/...YzU4NTQ2NGJiZWZj/NzMzZDY3MDAxMGVmJm9mPTA=.gif" />
<embed type="application/x-shockwave-flash" src="http://cache.reverbnation.com/widgets/swf/40/pro_widget.swf" height="300" width="280" align="top" bgcolor="#ffffff" loop="false" wmode="opaque" quality="best" allowScriptAccess="always" allowNetworking="all" allowFullScreen="true" seamlesstabbing="false" flashvars="id=artist_1015151&posted_by=artist_1015151&skin_id=PWAS1003&background_color=EEEEEE&border_color=000000&gig_lt=1291733945391&gig_pt=1291733955057&gig_g=2" /><br />
<img style="visibility:hidden;width:0px;height:0px;" border=0 width=0 height=0 src="http://www.reverbnation.com/widgets/trk/40/artist_1015151/artist_1015151/t.gif" />

Heshima kwako kakuruvi,

Mkuu umenikumbusha mbali sana hawa jamaa walikuwa juu sana enzi hizo kuna nyimbo yao moja naitafuta sana sijui kama unaweza kuiweka hapa tuifaidi vizuri.

Uzuri wangu ni wakuzaliwa nao
Pesa ya kutumia ninayooooo
Gari nzuri ya kumbea ninayooo
Nyumba nzuri ya kulala ninayooo
 
Nakwenda safari, safari yenyewe ya masafa marefu
Najua hapa unabaki watasema mengi, pia wabaya wetu mama watafurahi
Lakini usisikie yao mama watoto
Nakwenda kutafuta maisha ya watoto wetu mama
Nitarudi kwa mapenzi ya Mungu
Tutaonana kwa mapenzi ya Mungu

iyeye o mama iyeye
Safari sio kifo mama watoto
Subiri nitarudi mpenzi ee

Nikirudi mama nitakuletea zawadi
Nikirudi mama unipokee kwa mikono miwili ee

http://www.angelfire.com/linux/tizedboy/tancut.htm#[Mwanzo]
 
Heshima kwako kakuruvi,

Mkuu umenikumbusha mbali sana hawa jamaa walikuwa juu sana enzi hizo kuna nyimbo yao moja naitafuta sana sijui kama unaweza kuiweka hapa tuifaidi vizuri.

Uzuri wangu ni wakuzaliwa nao
Pesa ya kutumia ninayooooo
Gari nzuri ya kumbea ninayooo
Nyumba nzuri ya kulala ninayooo

Mimi nalia, nalia mie ooo,
mimi najuta, najuta mie oo,
najiuliza mama oo,
ni kosa gani mama mwenyezi Mungu nililomfanyia,

Uzuri wangu ni wa kuzaliwa naoo,
Pesa ninayo oo ya kutumia aa,
gari la kutembelea ninaloo,
Nyumba nzuri ya kulala ninayo mamaa x2

(chorus)

Kinachonisikitisha, nikuona kwamba nakosa mumee,
wa kunioaa, mamaa,
nami nisikie kama wenzangu waliobahatika kuolewaa
Iyooo (mama iyo lele) Iyoo

hata wa kunipa jambo jamani njiani sipati,
hata wa kunisabahi mimi sipatii,
mikosi gani nilizaliwa nayo mie mwenzenu masikini oo,
mama iyo lele (iyooo)
kajubi mukajanga (iyoo)
miki sesa (iyoo)
erasto oo (iyoo)
nawe nawe (iyoo)

Kinachonisikitisha ni kuona kwamba nakosa mume,
wa kunioaa, mamaa,
nami nijisikie kama wenzangu waliobahatika kuoleewaa
iyooo, mama iyo lele, iyooo

...Kwa kweli miaka hiyo ya 80 katikati hadi mwisho hawa jamaa wa 'fimbo lugoda mangala dance' walikuwa juu sana!
 
.. Utawaona kweli mtu na mke wake wakitembea kama baba na mwana. baadhi ya maneno kwenye wimbo wao mmoja hivi wakiponda ma sugar D

Mkuu, kweli huu wimbo ulikuwa juu mno wakati huo lakini mpaka leo hii maudhui yake yanaakisi jamii tunayoishi. kuna mistari miwili mitatu nitakuwa nimechanganya ama kusahau lakini uko hivi:

Kweli dunia mama......
Ukipenda mvulana aliye saizi yako,
ukipenda dada makamo yako,
kama we huna uwezo unajisumbua x2,

hata wazee wa leo wanaapenda kuoa,
wasichana warembo watoto dogo dogo oo,
na vijana wa leo oo wanapenda kuoa,
kina mama wenye pesa kina mama wenye uwezo,

utawakuta kweli mtu na mume wake,
wakitembeaa kama baba na mwanaee,
utawakuta kweli mtu na mke wake,
wakitembea kama mama na mwanaee,
bila kujali, bila kujali, bila kujali......

nasikitika sana nimesahau baadhi ya maneno ya wimbo huu ambao ulikuwa moto sana!
 
mkuu nakupa 5!!

Tancut almas, inanikumbusha mwaka 1990 wakati ule ndo namaliza six pale tosa, basi tulialikwa na iringa girls kwenda kwenye muziki wa tancut almas waliokuwa wakipiga pale iringa girls nasi ilikuwa kali ya mwaka tuliserebuka ile mbaya.

Nakumbuka walikuwa wana raise funds kwaajili ya kujenga madarasa ya five na six pale shuleni kwao. Basi ilikuwa ni balaa kwani kasaloo kianga na nduguye kianga songa walikuwa ni kivutio bab-kubwa.

Kwakweli umenikumbusha mbaalii kweli kweli (iringa girl's vs tosa).

iringa girl's (zoo).
 
Heshima kwako kakuruvi,

Mkuu umenikumbusha mbali sana hawa jamaa walikuwa juu sana enzi hizo kuna nyimbo yao moja naitafuta sana sijui kama unaweza kuiweka hapa tuifaidi vizuri.

Uzuri wangu ni wakuzaliwa nao
Pesa ya kutumia ninayooooo
Gari nzuri ya kumbea ninayooo
Nyumba nzuri ya kulala ninayooo

Nyimbo nilizonazo sasa za tancut ni ''samahani ya uongo'', ''mama'', ''ndoa si utumwa'' na ''almasi''

Nyimbo nilizonazo sasa za tancut ni ''samahani ya uongo'', ''mama'', ''ndoa si utumwa'' na ''almasi''

hivi mzee mwenzangu kuna verse moja inasema 'naona bora niende zambia nikamtafute monica, nimleta dsm apambane na kesi yake' ulipigwa na nani? Nakumbuka enzi hizo mtaa mzima kulikuwa na redio moja kwa mzee mmoja ambaye mtoto wake alikuwa anafanya kazi dar. So saa 1.30 tulikusanyika kwa mzee huyo ili kusikiliza michezo na taarifa ya habari!!
 
-Ndalla Kashebha.
 
Longe...twipulika!!!

"Nyongise". Mmenikumbusha luxury bar pale IRA. Mwisho mwa miaka ya 90 na mwanzoni mwa 2000, ilikuwa ikipigwa live band ya nyimbo za tancut chini ya gwiji kalala mbwembwe. Ilikuwa nzuri sana. Gwiji huyo nae hatunae. Dah!
 
hivi mzee mwenzangu kuna verse moja inasema 'naona bora niende zambia nikamtafute monica, nimleta dsm apambane na kesi yake' ulipigwa na nani? Nakumbuka enzi hizo mtaa mzima kulikuwa na redio moja kwa mzee mmoja ambaye mtoto wake alikuwa anafanya kazi dar. So saa 1.30 tulikusanyika kwa mzee huyo ili kusikiliza michezo na taarifa ya habari!!

Kasheba Ndala - Zaita Musica wimbo kesi ya khanga
 
BabaDesi nakumbuka hizi nyimbo tuliizimba sana kule kwenye DHB enzi kulikuwa na thread moja ya TIZED BOY..ili balaa watu walikuwa wanachana sana mistarii.
Jana nilikuwa nasikiliza RFA saa4 usku mpaka sita..yule bwana Baragaza alishusha ngoma zenye akili kweli nikakumbuka mbali sana alipopiga kibao cha Biashara jazz band...Kipini cha dhahabu pata kipande kidogo hiki
...Magenge mengine mabayaaa..ooho mama watoto
...watu wanapokusanyikaa..wengine hufaidika
..wengine wapoteza...wengine huwadanganya wenzaoo..kutaka maisha ya juu mamaa
 
Nilibahatika na mimi kusikiliza kipindi wimbo wa Bima Lee ''peleleza'

Peleleza peleleza, ohh peleleza uwe na hakika punguza zako hasira..........
.
Wakuu kama kuna mtu ana wimbo huu na nyimbo za washirika tanzania stars ani-pm tafadhali
 
kweli ya kale ni dhahabu. miziki ilikuwa miziki ya kweli wakati huo. vyombo vyote kazi za wanadamu, hakuna computer wala nini.
 
Jamani na mie naombeni mnitumie hizo MP3 nyimbo za Tancut almas, nazipenda sana, email yangu ni rshijaus@yahoo.com Sheshe Lutadila, mama na wifi na nyingezo zote zinazoweza kupatikana
 
vijana wenzangu wa zamani nami mnijuze hizo nyimbo za Tancut Almas zinapatikana wapi iwe tape ama CD nazihitaji sana nisaidieni jama.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom