Tamthiliya ya Dolce Amore

Dim Ray

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
318
247
Habari zenu wana Jf matumaini yangu muwazima wa afya. Matumaini yangu mapambano dhidi ya Corona yanaendelea vizuri.
Kipindi hiki cha almost a week muda ninaokuwa free nimeamua kuingia kwenye movie store yangu .Nimeibuka na tamthiliya ya kifilipino inayoitwa Dolce Amore, ni love story moja matata. Inamuhusu binti (Serena) aliyekuwa adopted na tajiri wa Italy baada ya wazazi wake kuteketea kwenye vita huko kwenye nchi ya Askovia. Anaishi na familia hiyo ya kitajiri kwanzia alipokuwa na umri wa mtoto mchanga mpaka anapokuwa mkubwa, lakini maisha yake yanakuwa ya mzigo ingawa sio sana kwani mama yake (Luciana ambaye ni mke wa Roberto aliyemu 'adopt' Serena) anamchukia na baada ya pilika pilika nyingi mwishowe kampuni ya Mr Roberto inakaribia kuanguka na ndipo hapo, bi Luciana anapoamua kumtumia Serena aingie kwenye mahusiano na mtoto wa tajiri(Gian Carlo) ili kampuni inusurike. Lakini ni kwamba Serena anampenda rafiki yake wa zamani ( Pen pal) kwa jina la Simon Tenten, bahati mbaya ni kwamba mapenzi yao yanapumulia mashine kwakuwa Simon ni masikini na anapitia matatizo makubwa. Kiukweli ni tamthiliya nzuri.
 
Back
Top Bottom