Honey Faith
JF-Expert Member
- Aug 21, 2013
- 15,782
- 11,841
Inaonekana wanaume/wavulana wa dar hii imewagusa maana kila siku thread za kujisafisha.Poleni na karibuni kanda ya ziwa tuwafunze ujasiri.😀😀😀
View attachment 216765
hawa ndo wanaume bhana chezea panya road wanaume wote dar walienda kulala mapema bila kupenda mbona siku ya tukio mlijifungia ndani.
wakati mna zozana kuhusu panya road na wanaume dsm.. wenzenu wanawaapisha wenyekiti wasio shinda na wana escrow wanachukua tu ela za safari kwenda mikoani na kiporo kina chacha.
Kill 3 hakuna aliyejifungia ndani huo ni uzushi tu si kweli
Hahahaaaa ila kweli wanaume wa Dar wametuaibisha sana, kasoro kaka zangu wa kitunda tu. Kuna mtu jana alisema wanaume wa Dar wanakula chips kwa toothpick hahahaaaa.
Unategemea kipanya road kikija, atafanyaje zaidi ya kutimua mbio au kulitelekeza gari, hahahahaaaa.
Catalunia mmepakimbia mpaka mkaondoka na change ya watu! Sasa hivi ndo umepata nguvu ya kuongea wakati juzi mpaka mliacha hata magari yenu kisa panya road! Wanaume Wa Darisalaama!!
Baada ya kimya kidogo Ndugu zangu wote wanaume tunaoishi katika jiji hili la Dar es salaam, tumeshuhudia vibweka vya aina yake toka kwa baadhi ya vijana wanaojiita eti wanaume toka huko kanda ya ziwa kutulaani kwa kukimbia eti kuogopa panya road, niseme ukweli kwa niaba ya wanaume wote tuishio hapa hakuna aliyekimbia zaidi ilikua ni kuwatuliza kina mama watoto na wazee kutokana na woga walioingia na kuhofia kujeruhiwa na hao vijana panya road, sisi tulikua mstari wa mbele kuwangoja kwenye maeneo yetu ili pindi wakipita tuwashughulikie kisawasawa na si kukimbia kama baadhi ya vijana wa kanda ya ziwa walivyodai, na siku ile hatukulala hadi tulipohakikisha usalama umetulia na hali imekua shwari kabisa. Nawakaribisha wanaume wenzangu wa dar kutoa ya moyoni kwenu hapa dhidi ya udhalilishwaji huu. Matusi na lugha chafu si msingi wa hoja hii karibuni
kiukweli ujasiri ni asili tu ya mtu... mi mkuria na badala ya kuwakimbia nilikuwa nawafuata walipo unfortunately sijakutana nao. sijui ni nini kilikuwa kinanisukuma kuwatafuta hawa vibaka but nilijishtukia niko magomeni frm moroko thru mwanyamala na vitongoji vyake vyote!!