Tamko la waumini wanaopinga Parokia ya Kawe kuendeshwa kinyume cha taratibu za Kanisa Katoliki

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
PAROKIA YA MT. MIKAELI KAWE, DAR ES SALAAM
Tamko la waumini wanaopinga Parokia ya Kawe kuendeshwa kinyume cha taratibu za Kanisa Katoliki
Tarehe 04 Novemba 2019

1572946466313.png

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam, Juda Thaddeus Ruwaichi, ambaye ndiye Askofu mwenye mamlaka na Paroko wa Parokia ya Kawe, Padre Nicholas Bahati Kundy

Ndugu wanahabari,

UTANGULIZI


Tangu mwaka 2011, Parokia ya Mtakatifu Mikaeli ya Kawe, jijini Dar es Salaam, imekumbwa na mgogoro unaohusisha paroko kwa upande mmoja na walei kwa upande mwingine. Waumini wengi tunapinga utaratibu unaotumiwa na Paroko Nicholas Bahati Kundy kuendesha. Yeye anaendesha parokia kana kwamba ni kampuni ya biashara inayotafuta faida kubwa na bila kujali ubora wa huduma za kiroho kwa waumini.

Tayari tabia hii imesababaisha hasira kubwa kwa waumini mpka kufikia hatua ya Padre Nicholas Bahati Kundy kuzuiwa kusoma misa mara mbili.

Mara ya kwanza, Padre Nicholas Bahati Kundy alizuiwa kusoma misa tarehe 19 Mei 2019. Waumini walitumia mbinu hii kufikisha ujumbe wao kwake. Polisi waliitwa, wakaingilia kati, hali ikatulia, na hatimaye akapata fursa ya kusoma misa, lakini kwa kuchelewa.

Mara ya pili, waumini wenye hasira walimzuia Padre Nicholas Bahati Kundy kusoma misa tarehe 06 Oktoba 2019. Siku hiyo, misa ya kwanzana misa ya pili ilisomwa na Padre mgeni aitwaye Kisoko, wakati misa ya tatu, ilifutwa. Padre Nicholas Bahati Kundy hakujitokeza kabisa kusoma misa yoyote kwa sababu ya hofu na misukosuko kutoka kwa waumini wanaopinga mwenendo wake.

Matukio haya yamekuwa yanaripotiwa katika vyombo vya habari mbalimbali, vikiwemo vyombo vya Kanisa Katoliki, katika namna ambayo haitoi picha halisi kuhusu chimbuko la mgogoro huu. Hivyo, tumeona ni muhimu na lazima kutoa ufafanuzi mfupi ili kuweka kumbukumbu sawa.

SABABU ZA MGOGORO


Kuna sababu nyingi zinazozalisha mgogoro kati ya waumini na Padre Nicholas Bahati Kundy. Kubwa ni kama ifuatavyo:

Mosi, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kufichua hadharani siri za sakramenti ya kitubio. Kwa mfano, aliwahi kufichua siri za kitubio za mzee Francis Katambi katika kikao cha Mashauriano parokiani, jambo lililozua mtafaruku mkubwa. Mpaka leo mzee Francis Katambi hawezi kwenda kufanya kitubio kwa Paroko. Tabia hii ni kinyume cha sheria za Kanisa Katoliki toleo la mwaka 1983.


Pili, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kufuta chaguzi za Jumuiya Ndogo Ndogo pale wanapochagiliwa waumini ambao yeye hawapendi. Aanapofanya uamuzi huu hatoi sababu kwa waumini. Hivyo, waumini humgomea. Migogoro ya hivi karibuni inatokana na sababu hii. Amefuta uchaguzi katika Jumuiya nne zikiwemo Jumuiya ya Mt. Stefano na Mt. Martin Deporres. Alipoagiza uchaguzi urudiwe waumini wakakataa kwa hoja kwamba wao wamekwishamaliza kufanya uchaguzi wa viongozi wanaowataka. Tabia hii ni kinyume cha ibara ya tisa (9) ya Katiba ya Halmashauri ya Walei Katoliki, toleo la mwaka 2003.

Tatu, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kuendesha shughuli za Parokia bila kushirikisha vyombo vya ushauri vilivyo chini ya Halmashauri ya Walei, kama vile Kamati Tendaji. Kwa mfano, alisaini mkataba na kusimamia ujenzi wa Ukumbi wa Mkitano wa Parokia bila kushirikisha kikao chochote cha Kamati Tendaji. Hata Katibu wa Halmashauri ya Walei, Mzee Makwabe, ambaye ni mtendaji mkuu wa Parokia, hakushirikishwa. Mwenendo huu ni kinyume cha matakwa ya Katiba ya Halmashauri ya Walei Katoliki, toleo la mwaka 2003.

Nne, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kutumia sadaka ya Parokia kinyume cha bajeti ya Parokia iliyopitishwa na Kamati ya Uchumi na Fedha ya Parokia. Kwa mfano, mara kadhaa, fedha inayopelekwa benki kila siku ya Jumanne inakuwa ni pungufu ya makusanyo yaliyopatikana siku ya Jumapili iliyotangulia. Akiulizwa na Kamati Tendaji, jawabu lake ni kwamba, “mimi ndiye bosi wa Parokia, naweza kusonga mbele bila kuwasikiliza walei, sio lazima niombe ushauri kwa walei, kwani mwisho wa siku mimi Paroko peke yangu ndiye nawajibika kwa Askofu wa Jimbo.” Tunaona kuwa, mwenendo huu ni kinyume cha matakwa ya Katiba ya Halmashauri ya Walei Katoliki, toleo la mwaka 2003.

Tano, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kutoa huduma ya sakramenti ya ndoa kwa kutoza gharama kubwa zaidi kuliko viwango vilivyopitishwa na Kamati Tendaji ya Parokia, yaani shilingi 136,000/= pekee. Kwa mfano, mtoto wa muumini mmoja aitwaye Mzee Masanja alitakiwa kulipa shilingi 370,000/= kama sharti la ndoa yake kufunguwa. Paroko Kundy aliposafiri, padre msaidizi aitwaye, Padre Sentaro, alifunga ndoa hiyo kwa gharama ya shilingi 50,000/= pekee. Kwa ufupi, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa anatoa huduma ya sakramenti ya ndoa kama huduma ya kibiashara.


Na sita, Padre Nicholas Bahati Kundy amekuwa na tabia ya kushindwa kutoa huduma ya misa ya mazishi kwa waumini wake pasipo sababu za msingi. Kwa mfano, muumini aitwaye Lucy Mduda alipofariki hakupata huduma ya misa ya mazishi. Mazishi yaliendeshwa na Mzee Mgila kwa kutumia uzoefu wake kama Katekista mstaafu.

Haya malalamiko yetu yamefafanuliwa kwa kina katika barua yetu kwenda kwenye Ofisi ya Askofu Mkuu Jimboni, iliyowasilishwa tarehe 07 JUni 2019. Tunaambatanisha barua hii kama “Kiambatanisho A.” Aidha, malalamiko haya yalifafanuliwa zaidi kwenye barua za ushahidi zilizoandaliwa kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Walei Jimbo, Padre Vitalis Kasembo. Tunaambatanisha barua hizi kama “Kiambatanisho B.”

HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Tayari malalamiko haya yamefikishwa katika ngazi za juu za uongozi wa Jimbo. Kiongozi wa Dekania na Paroko wa Mwananyamala, Padre Penedict, alikuja na kutusikiliza. Baadaye, Mkurugenzi wa Baraza la Walei Jimbo, Padre Vitalis Kasembo alikuja pia. Hivi karibuni, tulikutana na Askofu Mkuu, Juda Thadeus Ruwaichi na kuongea naye.

Kadiri tunavyosubiri kukutana na viongozi wa Jimbo, ndivyo mahusiano kati ya waumini na Paroko yanavyozidi kudorora. Mfano, kila mara viongozi wa kwaya na Jumuiya Ndogo Ndogo wanaondolewa madarakani. Tunaona kwamba, uongozi wa Juu wa Kanisa unakuwa tayari kusikiliza lakini hauna haraka ya kutoa majibu kwa hoja zetu. Mara ya mwisho, tulikuwa na miadi ya kuonana tena na Askofu Ruwaichi juzi tarehe 01 Novemba 2019. Masisita walitwambia kwamba hayupo na hakuna siku mbadala aliyoitaja kwamba tunaweza kumwona. Ni kama tumetekelezwa.

WITO KWA UONGOZI WA JIMBO

Hivyo, tunapenda kutumia fursa hii kumfahamisha Askofu Juda Thadeus Ruwaichi kwamba, bado tunayo nia ya kuonana naye ili tuweze kupatiwa majibu ya hoja zetu. Hatupendi kuona fedha inateka dini ndani ya Kanisa Katoliki.

Taarifa hii imeshuhudiwa na:

SAMWEL MGILA
Mwenyekiti wa Kamati ya Ufuatiliaji
Simu: 0652763968

DAVID KULWA
Katibu wa Kamati ya Ufuatiliaji
Simu: 0747508633

Tamko--Kawe 2.png
Tamko--Kawe 1.png
 

Attachments

  • TAMKO LA WAUMINI--FINAL.doc
    46.5 KB · Views: 5
Tabia yake ya ulevi na kula wanakwaya mbona ujahianisha mkuu...
Anaogopa kuwaleta mashahidi walioliwa wengine waweza kuwa wake za watu wakakataa kutoa ushirikiano.

Kuhusu swala la kupeleka pesa benki pungufu hapo kuna maneno waweza kuta hazili peke yake hizo pesa alizokata waweza kuta wanagawana na vigogo kwenye ofisi ya Jimbo ndio ndio maana anakuwa jeuri.Akishakata na wao anawakatia Chao
 
Ingawa mimi si mkatoliki ila hii njia uliyoitumia kuweka hadharani hivi huu mgogoro siyo sahihi labda kama mngetumiana wakatoliki wenyewe, Jaribuni kutatua migogoro yenu wenyewe ndanindani kwa ndanindani pasi na kuonyesha watu wa nje ambao wengi badala ya kuwasaidia watawadhiaki na kuwakashfu na hivyo lengo kutofikiwa

Nina imani malalamiko yenu viongozi wenu wanayashughulikia kama mlishawaeleza kuweni na subira majibu au hatua wakati mwingine zinachukua muda kulingana na tatizo husika
 
Hivi Ruwaichi alisharudi?na kupata nafuu?naona apo mlivyomkosa tarehe moja ,mkahisi mmetelekezwa
 
Anaogopa kuwaleta mashahidi walioliwa wengine waweza kuwa wake za watu wakakataa kutoa ushirikiano.

Kuhusu swala la kupeleka pesa benki pungufu hapo kuna maneno waweza kuta hazili peke yake hizo pesa alizokata waweza kuta wanagawana na vigogo kwenye ofisi ya Jimbo ndio ndio maana anakuwa jeuri.Akishakata na wao anawakatia Chao

Sad jamaa ameiga za viongozi wa chama chako.
 
Wakatoriki nao wamekuwa kama walokole. Migogoro kibao. mmetia aibu. lakini bado ni kanisa stable kama wakitatua migogoro hii mapema mapema.
 
Back
Top Bottom