Tamko la Umoja wa Kizazi cha kuhoji Tanzania (UTG) kuhusu suala Ben Saanane kutojulikana alipo

Inasikitisha sana kama kuna jambo linalotishia uhai wa mtu na bado watu wanaleta mzaha. Lakini mbaya zaidi ni kama mhusika au watu wanaofanya kazi naye karibu wanajua alipo na ahawatoi taarifa. Ni mbaya kupita maelezo maana ikijagundulika alikuwa amesafiri tu, au alikuwa sehemu kufanya kazi fulani, itasababisha hata siku baya likimtokea hakuna atakaye jali.maana itakuwa ni mazoea tu, mbona kipindi fulani alipoteaga kumbe alikuwa amesafiri tu...kumbe kwa hicho kipindi mtu yupo kwenye hati ya kupoteza uhai.

Tujifunze kuacha mzaha kwenye mambo muhimu haswa yanayohusu uhai wa mtu.
Kabisa mkuu na kama Chadema wana taarifa zake si waseme.hii kukaa kimya yule jamaa ana wazazi ana familia unadhani watakuwa katika hali gani endapo ndugu yao ,mwanao haonekani huku wakisikia kwamba kuna miili ya wafu imeokotwa?
Watu wanafanya mzaha lakini hili si jambo la kufanya mzaha hata kidogo.
 
Mambo kama haya si ya kuyafanyia maskhara hata siku moja. Hawa vijana wametoa hoja za msingi sana na zinahitaji kupatiwa majibu ya uhakika. Achilia mbali kupotea kwa Ben saa nane suala la Vifo vya utata vya hao watu wengine ni vya kuogofya. Naiona kagame style inataka kuingia nchini kwetu.
Mungu anawaona mkuu ..mnaficha mtu na kuua wengine alafu mnakuja hapa kusingizia serikali makini kama hiii?hii kitu itawatafuna mno
 
with all due respect wa ovyo ni hao vijana. badala ya kua objective kumsaka ben saanane wamegeuza tukio hila kama mtaji wa kisiasa wanalitumia kufanya propagamda. mtu anaweza kusema wamemficha ben saanane ili wafanye siasa. kama sivyo wamtafute kijana wa watu waache kufanya siasa na maisha yake.
Propaganda katika lile tamko ni ipi sasa? Unafikiri wangefanyaje ili waonekane wako objective kulingana na uelewa wako?
 
Wameibua hoja nzuri sana ila
1.Hapo waliposema "waTanzania wenzetu" kwenye suala la maiti zilizokutwa mtoni kuna utata.Wamejuaje kama ni waTanzania????
2.Pia hoja kwamba Beni "arudishwe akiwa mzima" ni kama vile inaushahidi kwamba kupotea kwake kunatokana na "kushikiliwa na watu Fulani" hii inaweza kuzuia uchunguzi katika mitazamo mingine(kuna uwezekano wa kupotea bila kutekwa/kushikiliwa).
 
Who is saa nane mpaka serikali iache shughuli zake za maana na kumfuatilia?JPM ana kazi nyingi zaidi ya saa nane.

Siyo Ben saa nane tu ndio serikali inajukumu la kuhakikisha maisha yake yanalindwa hata wewe serikali inajukumu la kuhakikisha uko salama kuendeleza upuuzi wako. Hilo ni jukumu la serikali.
 
Huyo HILDA NEWTON ni nani? Bilashaka ni miongoni mwa makada wazuri wa CDM

Kwa mujibu wa post yake Facebook amesema Ben yupo salama yupo South Africa

Je mmefanya juhudi kumuona ili awape details za safari yake? au ndo kutaka kuonekana kwenye media?
 
with all due respect wa ovyo ni hao vijana. badala ya kua objective kumsaka ben saanane wamegeuza tukio hila kama mtaji wa kisiasa wanalitumia kufanya propagamda. mtu anaweza kusema wamemficha ben saanane ili wafanye siasa. kama sivyo wamtafute kijana wa watu waache kufanya siasa na maisha yake.
Mbona taarifa yao inasema wamemtafuta mahosipatalini magerezani Ata ktk vituo vya Polisi?
 
Kabisa mkuu na kama Chadema wana taarifa zake si waseme.hii kukaa kimya yule jamaa ana wazazi ana familia unadhani watakuwa katika hali gani endapo ndugu yao ,mwanao haonekani huku wakisikia kwamba kuna miili ya wafu imeokotwa?
Watu wanafanya mzaha lakini hili si jambo la kufanya mzaha hata kidogo.
Chadema wana taarifa na wamemficha saa nane.
 
Kumbe Umoja huu Kiki yake ni Ben ajifiche ili mjulikane?

Maji taka
 
watu wengine wanatamka maneno yenye mizaa wakiamini kwamba waliouwawa ni wapinzani wao katika vyama. la kusikitika ni kama kweli wamezikwa bila hata kufanya juhudi za kuwatambua ni kina nani
 
Back
Top Bottom