Tamko la TYP juu ya MCC

Tamko la TYP juu ya MCC

Much respect MMM! Tangu juzi nawambia watu point hiyo hiyo ya kujibebisha kwa wazungu kuomba misaada. Ndio maana Mapunga yamejaa mjini hujawahi kuona, ashakum si matusi aisee nenda Znz ukajionee mwenyewe watoto wa kiume walivyoharibiwa. Yaani kuna project ya ujenzi inafanyika Pemba, vibarua wa kubeba zege na tofali wamekosekana imebidi mkandarasi afate vijana Tanga na Dar. Wao kazi yako kukaa maskani tu kusubiri misaada toka kwa ndugu na jamaa walioko ughaibuni ambao naamini pesa wanazipata kwa kufanya kazi. Wabongo tuamke jamani, slope hazifai
Ona Huu unafiki. Tuainishe hapa Maeneo ambayo tunasaidiwa na Hawa Wazungu kama Mtaendelea kukumbuka Shuka Asubuhi?

Mngekua hamtaki Hii misaada mngeacha kuomba na Mngesimama kuikosoa Serikali, Sio mpaka tunyimwe Baada Ya Kuomba Ndio Mjifanye Hamtaki Utegemezi.
 
Povu linatoka kwa sababu tulishatamanishwa halafu sababu za kutukosesha hizo pesa ni za ziko ndani ya uwezo wetu kuzitmiza lakini watawala hawajali.
Kwani uwezo wetu wa kufikiri unaishia hapa? Hivi kweli Nchi Haiwezi kutafuta trilioni moja mpaka Tutoe mapovu namna Hii?
 
safi sana

Yaani watanzania tulivyo wapuuzi tunasubiri wazungu waje watusaidie kuweka mashinikizo katika maeneo tunayogandamizwa
 
410a9d601e42e1353daf5b02a3594d97.jpg

TAMKO LA TYP JUU YA HATUA ILIYOFIKIWA NA BODI YA MCC KUSITISHA MISAADA YOTE NCHINI

Tanzania Youth Patriots (TYP) Imepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa ya Maamuzi ambayo Bodi ya MCC Imeyafikia hivi karibuni, ni dhahiri shairi kuwa hata kama tunaweza kupata fedha za kujihudumia kwenye maeneo ambayo awali walikuwa wanatusaidia ni wazi kwamba tutatetereka kidogo hata kuweza kusimama kwa Miguu yetu miwili kwa Ukamilifu.

Ikumbukwe kuwa Sababu zilizopelekea Wahisani wetu Kufikia uamuzi huo zimetokana na Masharti ambayo yamewekwa kama Vigezo kwa Nchi Husika kutimiza ili iweze kunufaika na Hisani hiyo. Kuzingatia Demokrasia na Uhuru wa Watu kutoa Maoni Yao Nchini vimekua Chanzo Cha Wahisani Hao Kufikia Maamuzi ya Kusitisha Kabisa Msaada wote ambao ulikuwa unafikia Takribani Trillioni 1. 4 za Kitanzania.

Kwa Tafsiri iliyopo Katika Jumuiya za Kimataifa hasa Marekani na Ulaya, Sheria mpya ya Uhalifu wa Mitandao imeonekana Ikikandamiza Uhuru wa Watu kutoa Maoni Yao kwa Uwazi na Maamuzi ya ZEC Kufuta Kabisa na Kurudia Uchaguzi wote Visiwani Zanzibar pia imeonekana ni Hatua ya Kukandamiza Demokrasia kwa Wazi.

TYP inatoa Wito kwa Serikali Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuona sasa ni Aibu kwa Nchi yetu kwa Mara ya kwanza Kwenye Karne Hii ya Ishirini na Moja kuwekewa Vizuizi vya Kiuchumi ili Kusimamia Kile ambacho Dunia na Watanzania wengi kwa Ujumla wanaamini ndio Haki.Sisi Kama Taifa Huru Linaloheshimu Misingi ya Haki na Demokrasia hatutangojea Shinikizo kutoka Nje litusaidie kuchukua Maamuzi sahihi kwa Mustakabari wa Taifa Letu na Watu wake Kwa Ujumla.

Tunaitaka Serikali kupitia Wizara Husika isimamie Mara moja Marekebisho ya Sheria Hii ya Uhalifu wa Mitandao na kuwasilisha Muswaada Bungeni mapema katika Vikao Vijavyo vya Bunge ili Kusimamia Misingi ya Uhuru wa watu kutoa Maoni yao Kama tulivyowashiriki wake. Hali kadhalika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Vyama Vya Siasa Husika na Jumuiya Mbalimbali kwa Pamoja vikae Chini kuhakikisha Suluhu ya kuleta Umoja kupitia Mchakato wa Maridhiano baina ya Pande Kuu Mbili zinazovutana unaleta Muafaka.

Ni rai yetu kuwa Serikali yetu Sikivu na yenye kutenda haki kama inavyojipambanua kupitia kwa Mh Rais John Pombe Magufuli itafanyia kazi Maoni yetu na ya wadau wengine juu ya suala hili Lililochukua taswira ya Kidiplomasia.

Imetolewa na :-

Idara ya Habari na Mahusiano

TYP Taifa.

Hizi hela naona kila mda zinazidi kuongezeka.
 
eti watanzania wanataka misaada bila masharti...Pumbaaaauf.....hamjui kuwa hiyo ni kodi ya wananchi wa nchi za watu?

Kama hamtaki mjitenge msitegemee msaada kutoka popote pale.....ujinga kabisa
 
Hopeless observations, uchaguzi umeshaisha ilihali wajinga wakijiweka kando, leo hii maridhiano yatatokea wapi tena. Wao ni hasa wabembelezwe kama mtoto mdogo aliyejisaidia kisha mama anataka amtawaze....acheni ujinga. Fanyeni kazi mjenge familia zenu na sio kujipendekeza kwa wazungu...mtapelekwa Mombasa bure shauri yenu

shughulikieni haya mambo

1.Rekebisha sharia ya Cybercrime
2.Rudini kwenye matokeo halali ya Uchaguzi Zanzibar 25 oct 2015

Kuwatukana TYP haisaidii...Hawa wameongelea kiini cha tatizo...sio Unafiki wenu
 
410a9d601e42e1353daf5b02a3594d97.jpg

TAMKO LA TYP JUU YA HATUA ILIYOFIKIWA NA BODI YA MCC KUSITISHA MISAADA YOTE NCHINI

Tanzania Youth Patriots (TYP) Imepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa ya Maamuzi ambayo Bodi ya MCC Imeyafikia hivi karibuni, ni dhahiri shairi kuwa hata kama tunaweza kupata fedha za kujihudumia kwenye maeneo ambayo awali walikuwa wanatusaidia ni wazi kwamba tutatetereka kidogo hata kuweza kusimama kwa Miguu yetu miwili kwa Ukamilifu.

Ikumbukwe kuwa Sababu zilizopelekea Wahisani wetu Kufikia uamuzi huo zimetokana na Masharti ambayo yamewekwa kama Vigezo kwa Nchi Husika kutimiza ili iweze kunufaika na Hisani hiyo. Kuzingatia Demokrasia na Uhuru wa Watu kutoa Maoni Yao Nchini vimekua Chanzo Cha Wahisani Hao Kufikia Maamuzi ya Kusitisha Kabisa Msaada wote ambao ulikuwa unafikia Takribani Trillioni 1. 4 za Kitanzania.

Kwa Tafsiri iliyopo Katika Jumuiya za Kimataifa hasa Marekani na Ulaya, Sheria mpya ya Uhalifu wa Mitandao imeonekana Ikikandamiza Uhuru wa Watu kutoa Maoni Yao kwa Uwazi na Maamuzi ya ZEC Kufuta Kabisa na Kurudia Uchaguzi wote Visiwani Zanzibar pia imeonekana ni Hatua ya Kukandamiza Demokrasia kwa Wazi.

TYP inatoa Wito kwa Serikali Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuona sasa ni Aibu kwa Nchi yetu kwa Mara ya kwanza Kwenye Karne Hii ya Ishirini na Moja kuwekewa Vizuizi vya Kiuchumi ili Kusimamia Kile ambacho Dunia na Watanzania wengi kwa Ujumla wanaamini ndio Haki.Sisi Kama Taifa Huru Linaloheshimu Misingi ya Haki na Demokrasia hatutangojea Shinikizo kutoka Nje litusaidie kuchukua Maamuzi sahihi kwa Mustakabari wa Taifa Letu na Watu wake Kwa Ujumla.

Tunaitaka Serikali kupitia Wizara Husika isimamie Mara moja Marekebisho ya Sheria Hii ya Uhalifu wa Mitandao na kuwasilisha Muswaada Bungeni mapema katika Vikao Vijavyo vya Bunge ili Kusimamia Misingi ya Uhuru wa watu kutoa Maoni yao Kama tulivyowashiriki wake. Hali kadhalika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Vyama Vya Siasa Husika na Jumuiya Mbalimbali kwa Pamoja vikae Chini kuhakikisha Suluhu ya kuleta Umoja kupitia Mchakato wa Maridhiano baina ya Pande Kuu Mbili zinazovutana unaleta Muafaka.

Ni rai yetu kuwa Serikali yetu Sikivu na yenye kutenda haki kama inavyojipambanua kupitia kwa Mh Rais John Pombe Magufuli itafanyia kazi Maoni yetu na ya wadau wengine juu ya suala hili Lililochukua taswira ya Kidiplomasia.

Imetolewa na :-

Idara ya Habari na Mahusiano

TYP Taifa.

HIVI MIMI NJIULIZA, WANANCHI TUKIDAI HAKI ZETU HIZI, SI NDIO KITANUKA ZAIDI?
 
Hao baba zenu Marekani wanawafunga watu bila kuwahoji Guantanamo,Snowden na Julian wa Wikileaks leo wamekimbia nchi kwa sheria za cyber crime,je unajuwa kuwa Symbion ni Richmond ambayo US wameficha uozo wao?..kama ni msaada wakate tu,leo wanajipanga jinsi ya kumkata Triump....fungukeni akili madogo...hivi hamjui kwamba us kupitia luwasa wameshindwa uchaguzi,2015?..wacha kutumika ukiwa kijana.
Kwahiyo we uwezo wako wa kufungua akili ndo huu...ficha upumbavu wako.
 
Kwani uwezo wetu wa kufikiri unaishia hapa? Hivi kweli Nchi Haiwezi kutafuta trilioni moja mpaka Tutoe mapovu namna Hii?
Asilimia 90 ya makusanyo inatumika kwa uendeshaji ikiwemo mishahara pia kuna deni la trillion 40 linatakiwa kulipwa
Magu atatoa wapi trillion isiyo na kazi
Miaka mitano sasa bajeti ya maendeleo haijawahi kutolewa zaidi ya 20%
 
Ni punguani pekee atakayekubaliana na serikali ya CCM katika hili. Sijui walifikiri nini? kuwa pamoja na EU na Marekani kuonya kuhusu ukiukwaji wa haki za msingi katika sheria ya mtandao na uchaguzi wa Zanzibar, wao waliona wako sawa tu. Eti Zanzibar ina katiba yake, huku nyuma CCM haiwajibiki kwa katiba hiyo!! Lo, aibu kubwa. Hili litatuumiza sana, na hakika hili litaangusha kwa zaidi ya 60% manufaa tuliyotegemea kutoka kwa serikali ya Pombe Magufuli. Laiti angechukua hatua, hakika nchi ingekuwa ya asali na maziwa chini ya uongozi wake.

Kwa uchungu mkubwa sasa tunasubiri rungu la EU, sijui watatuacha vipi.

Vita ni vita, lakini unapokuwa na vita ya ndani na nje, aghalabu kama utatoka salama. Nakupa pole sana rais wetu katika hili.
 
Talk is Cheap, wataona impact yake hii Hela soon... saiv wanatafuta Cheap Popularity
 
shughulikieni haya mambo

1.Rekebisha sharia ya Cybercrime
2.Rudini kwenye matokeo halali ya Uchaguzi Zanzibar 25 oct 2015

Kuwatukana TYP haisaidii...Hawa wameongelea kiini cha tatizo...sio Unafiki wenu

Hakuna kitakachobadilishwa na nchi itasimama nakutoboa, kwanza Waziri wetu wa fedha ameshasema kwamba hiyo fedha ya MCC hazikujumuishwa kwenye bajeti ya ijayo hivyo ina maana miradi itaendelea kama kawaida na hata jana Waziri wetu Nishati ametoa wito kwa kandarasi kufanya kazi kwa haraka kusambaza umeme!
 
lakini mkumbuke hata wao wana uchungu na ela zao ndio maana wanatupa kwa masharti na hata kama ni wewe sidhani kama utaridhika kwa kumpa mzazi ela badala ya kufanya cha maana nyumbani yeye anaenda kulewea tu
 
Hakuna Nchi Huru inayoamuliwa Mambo yake LKN Makubaliano ya Kimataifa kama wewe ni Nchi Shirika ukienda Kinyume Basi wenzako hawana Budi bali kukuonyesha kwa Vitendo ili Ikusaidie kubadilika. Kwa Nchi maskini kama Yetu tegemea Vikwazo vya Kiuchumi... Hii yote ni Catalyst Uamuzi ni wetu Mkuu!!
Msemo wa 'hii Nchi Masikini' siupendi na sijui hasa kwa nini! kuna mambo hayahitaji elimu ya juu sana kuyaelewa, hivi tulipokuwa tunahubiriwa mabadiliko, watu walidhani mabadiliko gani? ili uje kuwa na msimamo wa kushughulikia mikataba mibovu kwanza lazima wahisani watambue unatambua thamani ya rasilimali ulizonazo! wacha watunyime misaada leo ili tupate nafuu ya kusimamia vya kwetu taratibu! tuna kila kitu cha thamani zaidi ya misaada wanayotunyima leo, tushirikianeni kusimamia na kukataa ubadhilifu na ufisadi hasa tunapokuwa na kiongozi wa juu anayeonekana kuchukizwa na hali hiyo!
 
Hakuna kitakachobadilishwa na nchi itasimama nakutoboa, kwanza Waziri wetu wa fedha ameshasema kwamba hiyo fedha ya MCC hazikujumuishwa kwenye bajeti ya ijayo hivyo ina maana miradi itaendelea kama kawaida na hata jana Waziri wetu Nishati ametoa wito kwa kandarasi kufanya kazi kwa haraka kusambaza umeme!

hahahahahhahahahahahhahahahahahaha
 
Hatuongelei Ubadhirifu na Ufisadi wala Kujua Thamani ya Rasirimali tulizonazo. Kuna Hela Za MCC tuliomba Tukanyimwa. Huo ndo mjadala.

Kujitegemea tunakokuongelea Ndio huku, Kuendelea kufanya mambo ya Ajabu kwenye Demokrasia yetu mpaka Dunia inatushangaa.
 
hata sijawaelewa maana hata hapo umeshatoa mawazo yako. Lakini utaishi kwa kutegemea msaada wa baba wa jirani mpaka lini. Matamko mengine yanatuwekea uzembe wa kufukiria, am still loading.....
 
Hivi tunapokosea mambo yetu ya ndani kimbilio pekee liwe WAFADHILI wakate misaada!? Wapinzani wa Ghadafi pia walijidanganya pia wakadhani USA ndo bwana yao, leo hata wao wanaikimbia nchi yao!

Nasikitishwa sana na vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa kushabikia vijimisaada kana kwamba nao ni wazee wanaosaidiwa huko makambini!

Ndo maana huwa sishangai vijana wengi sasa hivi mmekuwa MASHOGA na WASAGAJI! Yote hii ni matokeo ya UVIVU na kupenda kupanda ndege!

Endeleeni KUBONG'OA - By MMM
ubongo wako una funza!
 
Back
Top Bottom