Tamko la TYP juu ya MCC

Tamko la TYP juu ya MCC

Nchi hii imefika mahali mnikabidhi mimi PhD niweze kuwaokoa katika majanga makubwa
 
Hii Pesa ya MCC inawauma watu wengi sana yaani mpaka imekua noma kiasi hiki???

Hivi ni kweli tangia nchi hii ianze huo msaada wa MCC ndo msaada pekee Tanzania uliwahi kunyimwa na mataifa ya magharibi??

Alafu kama matatizo yetu ya ndani yanafahamika kwanini zisitumike njia za ndani za kiharakati au kufuata protokali ku-solve hayo matatizo mpaka tutumie hizo pesa za msaada kama ndo silaha ya kujikomboa toka katika matatizo hayo??

UKAWA na Wapinzani wengine pamoja na Wanaharakati kwa ujumla wana mipango ipi ya kimkakati kuhakikisha "Cyber crime law" inakua sio kandamizi na demokrasia kule Zanzibar inazingatiwa.... Hii MCC iwe ni kama chachu ila wasifanye kama ndo Ajenda muhimu kwani umuhimu wake sio mkubwa kiivyo...

Mwisho wa siku mimi naona hizi pesa za MCC zinaweza kua zilikua katika rada za wale wapigaji wetu wa misaada... watu walikua wanajipatia ulaji apa.. sasa mambo yameenda mrama inajengwa figisu figisu kana kwamba kuna jambo la kujadili sana kama taifa kuhusu iyo MCC....
 
hata sijawaelewa maana hata hapo umeshatoa mawazo yako. Lakini utaishi kwa kutegemea msaada wa baba wa jirani mpaka lini. Matamko mengine yanatuwekea uzembe wa kufukiria, am still loading.....
Tunatofautiana uelewa
 
410a9d601e42e1353daf5b02a3594d97.jpg


TAMKO LA TYP JUU YA HATUA ILIYOFIKIWA NA BODI YA MCC KUSITISHA MISAADA YOTE NCHINI

Tanzania Youth Patriots (TYP) Imepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa ya Maamuzi ambayo Bodi ya MCC Imeyafikia hivi karibuni, ni dhahiri shairi kuwa hata kama tunaweza kupata fedha za kujihudumia kwenye maeneo ambayo awali walikuwa wanatusaidia ni wazi kwamba tutatetereka kidogo hata kuweza kusimama kwa Miguu yetu miwili kwa Ukamilifu.

Ikumbukwe kuwa Sababu zilizopelekea Wahisani wetu Kufikia uamuzi huo zimetokana na Masharti ambayo yamewekwa kama Vigezo kwa Nchi Husika kutimiza ili iweze kunufaika na Hisani hiyo. Kuzingatia Demokrasia na Uhuru wa Watu kutoa Maoni Yao Nchini vimekua Chanzo Cha Wahisani Hao Kufikia Maamuzi ya Kusitisha Kabisa Msaada wote ambao ulikuwa unafikia Takribani Trillioni 1. 4 za Kitanzania.

Kwa Tafsiri iliyopo Katika Jumuiya za Kimataifa hasa Marekani na Ulaya, Sheria mpya ya Uhalifu wa Mitandao imeonekana Ikikandamiza Uhuru wa Watu kutoa Maoni Yao kwa Uwazi na Maamuzi ya ZEC Kufuta Kabisa na Kurudia Uchaguzi wote Visiwani Zanzibar pia imeonekana ni Hatua ya Kukandamiza Demokrasia kwa Wazi.

TYP inatoa Wito kwa Serikali Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuona sasa ni Aibu kwa Nchi yetu kwa Mara ya kwanza Kwenye Karne Hii ya Ishirini na Moja kuwekewa Vizuizi vya Kiuchumi ili Kusimamia Kile ambacho Dunia na Watanzania wengi kwa Ujumla wanaamini ndio Haki.Sisi Kama Taifa Huru Linaloheshimu Misingi ya Haki na Demokrasia hatutangojea Shinikizo kutoka Nje litusaidie kuchukua Maamuzi sahihi kwa Mustakabari wa Taifa Letu na Watu wake Kwa Ujumla.

Tunaitaka Serikali kupitia Wizara Husika isimamie Mara moja Marekebisho ya Sheria Hii ya Uhalifu wa Mitandao na kuwasilisha Muswaada Bungeni mapema katika Vikao Vijavyo vya Bunge ili Kusimamia Misingi ya Uhuru wa watu kutoa Maoni yao Kama tulivyowashiriki wake. Hali kadhalika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Vyama Vya Siasa Husika na Jumuiya Mbalimbali kwa Pamoja vikae Chini kuhakikisha Suluhu ya kuleta Umoja kupitia Mchakato wa Maridhiano baina ya Pande Kuu Mbili zinazovutana unaleta Muafaka.

Ni rai yetu kuwa Serikali yetu Sikivu na yenye kutenda haki kama inavyojipambanua kupitia kwa Mh Rais John Pombe Magufuli itafanyia kazi Maoni yetu na ya wadau wengine juu ya suala hili Lililochukua taswira ya Kidiplomasia.

Imetolewa na :-

Idara ya Habari na Mahusiano

TYP Taifa.

Ninatamani muende mbele kidogo na kuilazimisha serikali ya ccm kuanza mara moja mchakato wa upatikanaji wa ktiba ya wananchi kuanzia pale ilipoishi tme ya Warioba. Bunge la katiba lisiundwe na wabunge wa bunge la JMT bali liwe maalumu lenye uwaklishi ulio sawia katika makundi yote. Kam akila kundi linawakilishwa na watu wawili basi kila chama cha siasa kiwakilishwe na watu wawili tena ikiwa ni lazima vyama viwakilishwe.

Upofu wa katiba ndiyo umetufikisha hapa tulipo. Bila marekebisho ya katiba, yote mengine ni danganya toto. Katiba ndiyo inatoa mwanya kwa watu binafsi kubinafsisha nchi na maslahi ya raia kwa kivuli cha mamlaka ya kikatiba.

Tena waambieni ccm wakome ku brainwash watu kwamba eti kunyimwa misaada ni kujitegemea. Kujitegemea kunakujaje bila kuratibiwa kwa mipango mahsusi yenye mrengo huo? Wakati wanaahidi kuyatolea ufafanuzi hayo majanga ya democrasia na matumizi mabaya ya sheria gandamizi, hawakujua kwamba wanakiuka Demokrasia na kunyanyasa raia ili wajitegemee? Kwa nini hawakujibu pale pale kama ndilo lilikuwa lengo?

Ok. tuseme walikuwa wanaandaa majibu, kama majibu ndiyo haya wanayotumia ku wa brainwash Watanzania majuha, kwa nini hawakuyawasilisha kwenye MCC kama walivyohitajika? Ccm ituondolee upumbavu.

Tanzania si mali ya ccm ni ya Wananchi. Mwisho wa uvumulivu wa Wantanzania dhdi ya utawala dharimu wa ccm sasa umefika.

Sseiakli ya ccm inatakiwa kulazimishwa kufuata uongozi wenye maslahi kwa Watanzania na si upumbavu wa kuwatumia Watanzania kwa maaslahi ya watawala. Period!.
 
Back
Top Bottom