Joshua Haji
Senior Member
- Nov 4, 2011
- 108
- 20

TAMKO LA TYP JUU YA HATUA ILIYOFIKIWA NA BODI YA MCC KUSITISHA MISAADA YOTE NCHINI
Tanzania Youth Patriots (TYP) Imepokea kwa Masikitiko Makubwa Taarifa ya Maamuzi ambayo Bodi ya MCC Imeyafikia hivi karibuni, ni dhahiri shairi kuwa hata kama tunaweza kupata fedha za kujihudumia kwenye maeneo ambayo awali walikuwa wanatusaidia ni wazi kwamba tutatetereka kidogo hata kuweza kusimama kwa Miguu yetu miwili kwa Ukamilifu.
Ikumbukwe kuwa Sababu zilizopelekea Wahisani wetu Kufikia uamuzi huo zimetokana na Masharti ambayo yamewekwa kama Vigezo kwa Nchi Husika kutimiza ili iweze kunufaika na Hisani hiyo. Kuzingatia Demokrasia na Uhuru wa Watu kutoa Maoni Yao Nchini vimekua Chanzo Cha Wahisani Hao Kufikia Maamuzi ya Kusitisha Kabisa Msaada wote ambao ulikuwa unafikia Takribani Trillioni 1. 4 za Kitanzania.
Kwa Tafsiri iliyopo Katika Jumuiya za Kimataifa hasa Marekani na Ulaya, Sheria mpya ya Uhalifu wa Mitandao imeonekana Ikikandamiza Uhuru wa Watu kutoa Maoni Yao kwa Uwazi na Maamuzi ya ZEC Kufuta Kabisa na Kurudia Uchaguzi wote Visiwani Zanzibar pia imeonekana ni Hatua ya Kukandamiza Demokrasia kwa Wazi.
TYP inatoa Wito kwa Serikali Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuona sasa ni Aibu kwa Nchi yetu kwa Mara ya kwanza Kwenye Karne Hii ya Ishirini na Moja kuwekewa Vizuizi vya Kiuchumi ili Kusimamia Kile ambacho Dunia na Watanzania wengi kwa Ujumla wanaamini ndio Haki.Sisi Kama Taifa Huru Linaloheshimu Misingi ya Haki na Demokrasia hatutangojea Shinikizo kutoka Nje litusaidie kuchukua Maamuzi sahihi kwa Mustakabari wa Taifa Letu na Watu wake Kwa Ujumla.
Tunaitaka Serikali kupitia Wizara Husika isimamie Mara moja Marekebisho ya Sheria Hii ya Uhalifu wa Mitandao na kuwasilisha Muswaada Bungeni mapema katika Vikao Vijavyo vya Bunge ili Kusimamia Misingi ya Uhuru wa watu kutoa Maoni yao Kama tulivyowashiriki wake. Hali kadhalika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Vyama Vya Siasa Husika na Jumuiya Mbalimbali kwa Pamoja vikae Chini kuhakikisha Suluhu ya kuleta Umoja kupitia Mchakato wa Maridhiano baina ya Pande Kuu Mbili zinazovutana unaleta Muafaka.
Ni rai yetu kuwa Serikali yetu Sikivu na yenye kutenda haki kama inavyojipambanua kupitia kwa Mh Rais John Pombe Magufuli itafanyia kazi Maoni yetu na ya wadau wengine juu ya suala hili Lililochukua taswira ya Kidiplomasia.
Imetolewa na :-
Idara ya Habari na Mahusiano
TYP Taifa.