Tamko la TPN: Ni uzalendo au ukada? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la TPN: Ni uzalendo au ukada?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sophist, Feb 2, 2012.

 1. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,083
  Likes Received: 1,729
  Trophy Points: 280
  Tafadhali jisomee mwenyewe msimamo wa TPN kuhusiana na mgomo wa madaktari hapa nchini. Viongozi wa TPN wamesukumwa na uzalendo au ukada?
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Hili si tamko...Hamna kitu hapo, halina uzito wowote. An Empy Basin
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Nimesoma na nimekuwa disappointed kwa kiasi. Hawapendi kuudhi.
   
 4. Steven Robert Masatu

  Steven Robert Masatu Verified User

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 2,393
  Likes Received: 728
  Trophy Points: 280
  again.....
   
 5. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  kama haya ndiyo maoni ya wanachama wao basi bado tunayo safari ndefu sana kutoka hapa tulipokwama! mbaya zaidi eti haya ni maoni ya wasomi. kama siyo kutafuta ubunge wa viti maalumu CCM ni nini hii? aibu!
   
 6. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Utumbo mtupu
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Jukumu la kutoa huduma za afya (kwa watanzania wote) liko kwa serikali. Hilo tuelewe. Madaktari wanafanya kazi kwa makubaliano (contract) na serikali lakini hili halimanishi hata kidogo kuwa madaktari ndio wenye jukumu hilo. Na makubaliano hayo kila mmoja ana wajibu wake: Madaktari watoe ujuzi wao (huduma) na serikali igharamie huduma hapa ikimaanisha vitendea kazi, pamoja na mishahara.

  Je, kila upande umetekeleza wajibu wake kama walivyokubaliana? Hivi ukingia mkataba na mkandarasi akujengee nyumba na ukaahidi kuwa utaleja saruji, matofali, mabati, na ikatokea hukuleta utamlaumu huyo mkandarasi kama hakujenga nyumba? Hospitali hazina dawa, hazina vifaa, wanategemea nini? Yeyote anayebisha kuwa hospitali zetu hazina vifaa aseme ni kwanini wakubwa wanaenda India? Tanzania inaongoza Afrika nzima kwa kupelea wagonjwa India. Kwa utajiri gani tulio nao?

  Hii hadithi kuwa hali mbaya ya uchumi wa dunia inaathiri Tanzania kwangu mimi ni sawa na 'chekundu cheusu'. Ugumu Tanzania? Kwa vipi? posho? mashangingi? ugumu gani wakati matanuzi yako pale pale?

  Tanzania kama kweli tulikuwa na watu makini hatutakiwi kabisa kulia na mambo ya uchumi wa dunia. Tuna madini, na kipindi chote cha mdororo wa uchumi wa dunia bei ya dhahabu imezidi kupanda maana watu wanaona ndio asset isiyopungua thamani. Hivyo sisi kama tulikuwa makini huu ungekuwa msimu wetu wa kuvuna. Australia wanapeta kutokana na mchango wa madini na hawana hata nusu ya rasilimali ya madini tuliyonayo.
   
 8. n

  nndondo JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  Ni ujikombi wa mwisho sijawahi kuona, kwanza halijajadiliwa na mtu yoyote ni huyo Phares kaliandikia chumbani anatafuta lcous kwa kuliita la TPN, mimi nilikua active member wa TPN tangu enzi za Mtsimbe lakini sikuwahi kuona uchafu kama huu, tangu leo nimejitoa. Hivi kuna mtu anaweza kujiita professional katika nchi yoyote ikiwemo ndogo kama Gambia akaandika ushuzi kama huo? Phares Magesa ajiuzulu mara moja toka TPN ama sivyo abaki na TPN yake peke yake, hatuwezi kutumiwa na wagombea ubunge wa magamba kusukuma agenda zake, pu pu pu huu ni udhalilishaji wa hali ya juu sikutegemea kuuona katika maisha yangu yote. Sasa hivi tunataka TPN iitishe uchaguzi mara moja kujadili haya huku ni kuwazalilisha madaktari kwa maslahi binafsi, mnafiki mkubwa. Naomba binafsi kutoa pole kwa madaktari waliozalilishwa na kuomba member wote wa JF ambao ni member wa TPN wasiokubaliana na msimamo huu waunge mkono hapa kuonyesha kwamba sisi kwetu uzalendo ndio uko mbele kuliko matumbo yetu.
   
 9. n

  nmiku Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 41
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mimi sikubaliani na statement kuwa uchumi wa dunia umedorora kwa hiyo hata sisi hali mbaya tuliyonayo ni katika mwingiliano uliopo! Ni tegemeo langu kungekuwa na management nzuri ya resource tulizonazo tungekuwa tunaandika nne! Tatizo ni mismanagement iliyopo kutoka juu mpaka chini-corruption. Hata mwananchi ukishiriki kwa kujituma kwa nafasi yako uliyonayo katika jamii na unachozalisha kinakuwa-mismanaged tutafika? Kama madaktari wanajituma kwa uwezo wao wote wakiishi maisha magumu wakaona hao waheshimiwa wanajiongezea posho mara 5 kwanini nao wasidai nao waongezewe waweze kujikimu na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi?
   
 10. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sio ukada,ni uoga na kutokujiamini!
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ulambaji miguu ya watawala; OPPORTUNISM!!!
   
 12. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mimi ndio maana siwezi kujiunga na vikundi vya kipuuzi kama hivi!!!
   
 13. v

  valour Senior Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Well said!
   
 14. v

  valour Senior Member

  #14
  Feb 3, 2012
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 167
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  In God's economy...
  - There is NO recession
  - There is NO financial crisis
  - There is NO shortage of jobs.

  Kwa nchi kama hii yenye rasilimali nyingi, tungeweza hata kuwapa allowance wazee. Nani kasema kama kuna shida ya pesa sote lazima tuwe nayo. Kuna watu bongo hii hii hawaibi sio mafisadi wala nini lakini shida hawana kwasababu hawaishi kwa kushindana. Ukitaka kujua nchi hii inafuja pesa angalia mashangingi ya mawaziri, manaibu, wakuu wa idara, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, Government agencies. Angalia per diem zao not less than $300 per day. Misafara ya wakuu nje ya nchi. Yaani basi tu. Mkulo anadiriki kusema kuwa serikali inatumia billioni 360 kwa posho kati ya hizo 14 billioni ni kwa wabunge peke yake. Na anaongea bila kumun'gunya. Jamani hawa watu wanalipwa mishahara. Huwa nashindwa kuelewa the so called 'posho' sijui zilianza lini na kwa nini?

  Leo unaombwa pesa kidogo tu tena kwa ajili ya kuwahudumia wapiga kura wako unajibu siasa. Hilo tamko la TPN lilitakiwa liende shule kabisa.
   
 15. bona

  bona JF-Expert Member

  #15
  Feb 3, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  he is just another opportunist like kibonde! kwa matamko kama haya unaweza pata picha kwa nini nchi yetu haiendelei hivi huyu anaweza akajibu swali kwa nini nchi hii ina kila kitu ambacho a country would wish to have ili i develop lakini ni sisi tu ndio hatuendelei!
   
 16. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #16
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Ndo maana hivi vyama vingine huwa hatuna papara ya kujiunga navyo. Afadhali niwe mwanachama au shabiki wa Akudo au Twangapepeta nijue moja.Havina agenda ya kweli hata kidogo. Ni kula tu na ujanja ujanja wa watu wachache. Ukiona hivyo jua tayari kuna pandikizi....
   
 17. C

  Chibaby Member

  #17
  Feb 3, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Moja kati ya madai ya madaktari ni kumtaka KM kujiuzuru, je mdororo wa uchumi unaingia vipi katika hili? Hata kupatiwa audience na viongozi mnasingizia hali ya uchumi??? Jamani wachumi tunaomba kuelimishwa kidogo hapo.
   
 18. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #18
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Hawa ni professionals gani? Basketballers?
   
 19. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #19
  Feb 3, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Si muda tutasikia Bwa Phares Magesa anatangazwa kuwa Katibu Mkuu, ama barozi, ama anateuliwa kuwa mbunge
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Night club owners labda!wanaojiita wasomi Tanzania wameiharibu sana nchi hii. Ni wabinafsi mno wasiojari watu wengine wanashida kiasi gani!
   
Loading...