Tamko la Shura ya Maimamu Tanzania

Tamko la Shura ya Maimamu Tanzania

Kazi kweli nao hawa ....hii serekaliilishaunda tume hata moja yenye majibu kweli.....wameingia LADY'S room
 
mbona huo ni msimamo mzuri, iundwe tume huru ya uchunguzi then majibu ya uhakika yatapatikana.
Je mlitaka watangaze maandamano kesho nchi nzima au?
 
Tume kwenye serikali ya kikwete? Mbona hakuna kitakachochunguzwa,tume itaundwa lakini majibu hayatapatikana kamwe,huyu ndio Luten colonel Jakaya Mrisho Kikwete.
 
Shura hii ya maimamu imeiomba serikali ya Tanzania kuunda tume kuchunguza tukio la Seikh Ponda bila hivyo watapoteza imani na serikali.

Je! Kuna siku hao maimamu walitangaza kuwa wana imani na serikali!?
Au basi tu wameamua kuongea!
 
Shura hii ya maimamu imeiomba serikali ya Tanzania kuunda tume kuchunguza tukio la Seikh Ponda bila hivyo watapoteza imani na serikali.

Tume!? Mbona ulaji mwingine kwa serikali ya JK,lini tume ilitoundwa kwenye serikali ya Jk ikaja na majibu? Ya mwangosi kimya? Ulimboka ni majanga,Kibanda ndio basi tena,Milipuko Miwili ya mabomu Arusha hakuna kitu,Kuawawa kwa Padre Mushi kule zanzibar hakuna lolote, kumwagiwa tindikali kwa sheikh Soraga huko Znz hakuna majibu,unategemea tume itakayoundwa kwa ajili ya sheikh ponda itakuja na majibu? Labda siyo serikali sikivu ya Jk.
 
Kumbe bado wanaiman na serikali mpaka sasa Aisee wana moyo kweli.

Naona watu mlingojea shekh issa kundecha akurupuke na kutangaza maandamano..

Imekula kwenu..
 
Msitegemee Kikwete kuunda tume. Mbinu za kumpiga aunde yeye, afu tume ya kuchunguza aunde yeye wapi na wapi?
 
Shura hii ya maimamu imeiomba serikali ya Tanzania kuunda tume kuchunguza tukio la Seikh Ponda bila hivyo watapoteza imani na serikali.

CDM walisema mkapuuza. Ufanyike si uchunguzi wa tukio la Poanda, bali utendaji mzima wa jeshi la polisi nchini. Kwa maana kumekuwepo na matukio mengi ya uonevu, yasiyofuata sheria.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI

​
[TABLE="class: wsite-multicol-table, width: 2008"]
[TR="class: wsite-multicol-tr"]
[TD="class: wsite-multicol-col"]



AGOSTI 10, 2013.
​
[/TD]
[TD="class: wsite-multicol-col"]
JESHI LA POLISI TANZANIA
DAR ES SALAAM
​
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]



1. MNAMO TAREHE 10, AGOSTI ,2013 MAJIRA YA SAA 8 MCHANA, MAENEO YA SHULE YA MSINGI KIWANJA CHA NDEGE MANISPAA YA MOROGORO, KULIFANYIKA KONGAMANO LA BARAZA LA EID LILILOANDALIWA NA UMOJA WA WAHADHILI MKOANI MOROGORO. DAKIKA KUMI KABLA YA KONGAMANO HILO KUMALIZIKA ALIFIKA SHEKHE PONDA ISSA PONDA AMBAYE ALIZUNGUMZA KWA MUDA MFUPI.

2. KONGAMANO HILO LILIFUNGWA MAJIRA YA SAA 12:05 JIONI AMBAPO WATU WALIANZA KUTAWANYIKA, BAADHI YAO WAKIWA WAMEZINGIRA GARI DOGO ALILOKUWA AMEPANDA SHEKHE PONDA. BAADA YA KUTOKA KATIKA ENEO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIZUIA GARI HILO KWA MBELE KWA NIA YA KUTAKA


KUMKAMATA SHEKHE PONDA AMBAYE MPAKA SASA ANATUHUMIWA KWA KOSA LA KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI SEHEMU MBALIMBALI HAPA NCHINI YENYE MLENGO WA KUSABABISHA UVUNJIVU WA AMANI.

3. BAAADA YA ASKARI KUTAKA KUMKAMATA, WAFUASI WAKE WALIZUIA UKAMATAJI HUO KWA KUWARUSHIA MAWE ASKARI. KUFUATIA PURUKUSHANI HIYO, ASKARI WALIPIGA RISASI HEWANI KAMA ONYO LA KUWATAWANYA.

4. KATIKA VURUGU HIZO, WAFUASI HAO WALIFANIKIWA KUMTOROSHA MTUHUMIWA. HIVI SASA IMETHIBITIKA KUWA SHEKHE PONDA YUKO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI AKITIBIWA JERAHA KATIKA BEGA LA MKONO WA KULIA LINALODAIWA ALILIPATA KATIKA PURUKUSHANI HIZO.

5. KUFUATIA TUKIO HILO, TIMU INAYOSHIRIKISHA WAJUMBE KUTOKA JUKWAA LA HAKI JINAI IKIONGOZWA NA KAMISHINA WA JESHI LA POLISI CP ISSAYA MNGULU IMEANZA KUFANYA UCHUNGUZI WA TUKIO HILO.

6. AIDHA, JESHI LA POLISI LINATOA WITO KWA WANANCHI KUWA WATULIVU WAKATI SUALA HILI LINASHUGHULIKIWA KISHERIA.

Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.​
 
Ni msimamo mzuri sana, waswahili wanasema "mpe mchawi mtoto akulelee"
 
Kwenye taarifa ya habari ya channel 10 saa moja usiku wamesema serikali imeunda tume ya kuchunuza suala la Ponda
 
Ni mwendawazimu tu ndiye anaweza kuwa ana imani na jeshi la polisi hadi sasa...
By the way, ni wazi polisi itaunda tume ikiongozwa na inspekta Chagonja... Then subirieni majibu yake.... Mtaambiwa Ponda alijeruhiwa na kitu chenye ncha kali kilichorushwa kutoka kwenye kundi la waumini waliokuwa wakiandamana nae...
 
Teh teh, eti iundwe tume, chini ya serikali sikivu ya jk inawezekana? Chezea polisccm wewe?
 
Back
Top Bottom