Tamko la Rais Kikwete juu ya Tukio la Arusha

Tamko la Rais Kikwete juu ya Tukio la Arusha

n00b

Platinum Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
1,030
Reaction score
2,737
Taarifa kutoka Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha. Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa. Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake.

Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali na vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili. Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma. Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine, uwe na chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi yetu. Kamwe hatutakubali kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake. Rais anaamini kuwa Serikali, kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu hao watapatikana na kuadabishwa ipasavyo.

Aidha, Rais Kikwete anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wafiwa na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo. Anaungana nao katika machungu na msiba. Rais pia anawaombea wote walioumia katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa.

Rais Kikwete vilevile anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na shughuli yao muhimu ya uzinduzi wa Kanisa lao.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU,
DAR ES SALAAM
5 Mei, 2013
 
Hata mauaji ya Padri Mushi aliyapokea kwa masikitiko, Kujeruhiwa padri Mkenda alipokea kwa masikitiko, kuchomwa moto makanisa amepokea kwa masikitiko!! Sijui nini ambacho hajapokea kwa masikitiko, labda alichopokea kwa furaha ni ile Video ya Ustaadh Ilunga ya mauji ya sheikh Rogo inayohamasisha kuua wakatoliki.

Kikwete matamko yako tumeyachoka sasa ni wakati wa kuchukua hatua za kukomesha mauaji, la sivyo wakristo tutaamua kujilinda wenyewe dhidi ya maadui zetu
 
eti kapokea kwa mshtuko na masikitiko wakati kwenye picha za ziara anachekelea tu, au ndo kazipata taarifa saa hizi?
 
HALINA UZITO,
sitaki kuamini kama ni tamko la mkuu wa nchi!
 
Anajua chanzo cha hili!mbegu iliyopandwa na kulelewa na kina ilunga,yeye na wana ccm wenzake kama wasira na pinda inaanza kuchanua sasa.matunda bado!
 
Lile la kuuawa kwa father kule Zanzibar alikuwa hayupo, yuko safarini akatuma huyo msemaji wake kwa maneno hayo hayo, sijui alikuwa naenda wapi vile!!! Likatokea, serikali ikacheza sarakasi na mchezo umeisha, eti tumesahau. Na hili nalo katuma ujumbe na ahadi zile zile!!! Yaani vipaumbele vya Mr. President ni misaada kutoka kwa hao waasisi wa biashara ya utumwa, inauma sana.

Mimi kwa mtazamo wangu, Mr. President hayuko serious eti ana uchungu, kama angekuwa na uchungu angegeuza akaahirisha safari, hasa ukizingatia tukio la leo linaandika historia mpya katika nchi hii. Badala yake yuko anachekacheka na waarabu
 
Dhaifu Matamko

hata mauaji ya padri mushi aliyapokea kwa masikitiko, kujeruhiwa padri mkenda alipokea kwa masikitiko, kuchomwa moto makanisa amepokea kwa masikitiko!! Sijui nini ambacho hajapokea kwa masikitiko, labda alichopokea kwa furaha ni ile video ya ustaadh ilunga ya mauji ya sheikh rogo inayohamasisha kuua wakatoliki.

Kikwete matamko yako tumeyachoka sasa ni wakati wa kuchukua hatua za kukomesha mauaji, la sivyo wakristo tutaamua kujilinda wenyewe dhidi ya maadui zetu
 
Jamaa huyu huwa sina muda wa kumsikiliza sababu najua atakua anachecheka wakati watu wamekufa sababu ya jambo ambalo si geni kwa sasa! Kwann hasemi amechukua hatua gani makanisa kuchomwa, padri kuuwawa, leo anatoa tamko la hadithi bila kubainisha ni hatua gani zimechukuliwa kwa wahusika wa matukio ya mwanzo
 
Dunia nzima inapambana kuutokomeza uhalifu wa namna hii. Tushirikiane na serikali kwa pamoja ili tuutokomeze huu uhalifu.
 
kikwete kuendekeza udini kwenye kampeni za mwaka 2010 ndio zimefanya nchi ifike hapa ni muasisi wa udini nchini ajabu anatoa matamko badala ya kurudi nyumbani anataka wafe wangapi ndio asituke tunamuuliza anahesabu maiti ziwe ngapi ndio atasituka
 
Alitakiwa kukatisha hiyo ziara yake huko Kuwait na kurudi nchini haraka sana na kuungana na taifa zima katika hiki kipindi kigumu na sio kutoa matamko!:angry::angry:

Mkuu hata sijamuona mtu wa kukatisha ziara, kwa lipi hasa? anajua akisema amepokea kwa uchungu na mshtuko basi inatosha...........pia amewaagiza jeshi la Polisi kumsaka au kuwasaka na kuwaadabisha hao watu......kha! ningekuwa Rais hayo maneno hata nisingeyasema tena maana Raia wangeniona kituko..........hivi ni mara ya ngapi anarudia hizo sentensi?
 
Back
Top Bottom