Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA Freemaan Mbowe
amesema kamwe haongozi kundi au genge la wasaka vyeo na madaraka
ndani ya chama chake bali anaongoza kundi la watu wanaopenda mabadiliko.
Kiongozi huyo amesema binafsi hawezi kwa sasa kusema atagombea
Urais au Ubunge kwa sababu huu si muda wake hata kidogo.
Mbowe amesema mwanachama yeyote makini wa CDM kwa sasa
ni muda wa kuwaunganisha wanachama na watanzania kwa ujumla
na wala si muda wa kuwagawa kukimbilia madaraka.
Kiongozi huyo amesema ndiyo maana makamanda wote
wakiongozwa na Dr Slaa wamejichimbia vijijini
kwa kazi moja tu ya kueneza vuguvugu la mabadiliko-M4C