Tamko la kamati kuu ya CHADEMA kuhusu mchakato wa katiba

Hujui maana ya ukabila. ndio maana unaongea pumba.Nenda Dodoma kwa waongea pumba wenzako mkavuane magamba.
 
Hivi msomi haswa, anaandika hivi:

"kimepokea na kujadili kwa kina taarifa ya majadiliano"

Hivi magwanda mlikuwa mna "taarifa ya majadiliano"? ndiyo ipi hiyo?

Na hapo ndio sijaenda hata kwenye taarifa. Daaahhh, nawaonea huruma sana, hebu someni vizuri kabla hamjaanza "upiganaji" wenu na mimi. Maana kupigana mimi hamniwezi. Bora tubaki kubishana kwa hoja. Haya niambieni ni ipi hiyo taarifa ya majadiliano?

Ndiyo, Kamati Kuu imepokea taarifa ya Sekretariat kuhusu majadiliano ya muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba Bungeni. Kipi cha ajabu? Ulitaka na wewe upewe hiyo taarifa?
 
CDM wametilia sana msisitizo kuhusiana na hilo la kofia ya Mh Rais, ile ya uenyekiti wa CCM...Na hapo ndipo kwenye tatizo kubwa kabisa kama ni kweli ataachiwa afanye hivi anavyotaka kufanya.

Itakuwa haina maana kabisa ya kusema ni katiba ya wananchi.

Itakuwa ni katiba ya CCM,period.
 
Mimi ninashindwa kuwaelewa hawa wanaoshabikia ccm, post zao nyingi hazina hoja za msingi. Eti cdm ni chama cha ukabila, cdm chama chama cha kidini,huku nikuoyesha kwamba nyie ni masikini wa wafikra.Jibuni hoja kwa kuijenga nchi yetu sio kuibomoa.
 
Akiongea baada ya wabunge wa chadema kutoka nje alisema Rais wetu mpendwa "Mtatoka mtaenda mtarudi kwani mimi ndio Rais wenu hamna mwingine wa kumpelekea matatizo yenu ila ni mimi" alisema Rais kikwete. je kwa chama cha demokrasia na maendeleo kuunda kamati ndogo ili kwenda kumuona Rais kikwete je kwanza wamemtambua? je wataacha mchezo wao wa kitoto kutoka bungeni Rais anapohutubia utakoma? je watakubali maneno ya Rais kuwa mtakwenda mtarudi Rais wenu ni mimi?
Taifa tayari limekwama,wasipojaribu kufanya naye kazi itakuwa ni kuwasaliti watanzania ambao tayari wanasota.

However mwishowe wananchi watachagua yupi mkweli na yupi si mkweli.

Pia kwenye hili la katiba hakuna cha hivyo vyama vyenu mnavyovipigia debe.

Hakuna kifungu cha katiba chenye kutakiwa kuitambuwa haki ya mwanchama wa chama cha kisiasa kwanza kabla ya haki ya raia.
 
Nahisi CHADEMA wanataka wamuone rais wampe list ya vitu wanavyoona vinatakiwa kuwepo kwenye muswada na ikitokea rais akakataa them watakuwa na nguvu zaidi ya mbele kwa wananchi. Inawezekana mkutano wa Dr Slaa,Salim na Warioba ulisaidia kwenye hili. CCM wasipokaa sawa wanaweza kujikuta on the loosing end maana wakikataa mapendekezo ya chadema ni shida na wakikubali mapendekezo hayo itaharibu 'ego. A catch 22 situation.

Ila kwa maoni yangu na kwa moyo safi kabisa, kama hii nchi ilikuwa na visionary leadership na niseme urais wa kitaifa badala ya ki-chama, kabla hata Celina Kombani na Werema hawajaandaa draft rais wa nchi alitakiwa akutane/akae chini na viongozi wa vyama vikuu vya upinzani (i.e CHADEMA, CUF & NCCR Mageuzi) wakubaliane TORs/mambo ya msingi. Katiba ni jambo la kitaifa sioni ni kwa vipi chama kimoja kinaamua kujibebesha mzigo nyeti kama muswada wa katiba. Huu ni udhaifu mkubwa kwenye uongozi wa juu wa nchi hii. Ni vizuri viongozi wetu waanze kujenga utamaduni wa kutambua mambo nyeti ya kitaifa na kuhakikisha haya mambo yanakuwa above party politics.

Mkuu, ushauri wako ni mzuri, lakini nafasi hy mbona waliikana bungeni? Leo ndo wameona wapeleke mapendekezo kwa rais kama c udhaifu ki siasa ni nn? Baada ya uchaguzi walisema hawamtambui kama rais bali mwenyekiti wa ccm, leo wanasema wanaunda kamati ya kuonana na kikwete kama rais na c mwenyekiti wa ccm,, jamani hawa kweli? Hata tukiwaangalia usoni mwao kweli ni viongozi wa taifa? ningependa kama kweli wana nia njema wangeungana wengine ambao wanaona jambo hili halikwenda vizuri mfano akina kibamba na wanaharakati wengine wakayatatue pamoja na Mh Rais. Itatusaidia sana katika kusonga mbele. Wakati wa kubishana kwenye mambo ya msingi bila majibu umepitwa na time.
 
Lini na wapi CHADEMA walisema hawamtambui Kikwete kama rais wa Tanzania? Acha ushabiki wa siasa.
LINI?! Ni baada ya General Election 2010, WAPI?! mbele ya waandishi wa habari including BBC Swahili service!!!! Hata hivyo, Dr. baadae alikula matapishi yake kwa kutangaza kumtambua rais kwavile eti "ni rais kwa mujibu wa sheria", sasa sijui kuna rais kwa mujibu wa nini cjui!!!!
 
Bishaneni,lumbaneni, zodoaneni, fokeaneni, tapikishaneni, umbuaneni, lkn ukweli unabaki kwmba Tz political parties serious HAKUNA! Ccm ni ze-commedy, Cdm ni Futuhi, Cuf ni mizengwe, Nccr Fataki-ngonjera, acha mi n'lale !
 
Acha ncheke ucku huu, nimekukubali jajment yako.
 
Ni rais kwa sababu ametangazwa na kuapishwa kuwa rais lakini kafikishwa hapo baada ya matokeo kuchakachuliwa! Hiyo hata mbishe kiasi gani ndio ukweli wenyewe! Kumalizia tu nakurudishia kuwa wewe sio tu kuwa ni kiazi bali ni gimbi kabisa! Ubongo wako umekauka kama gamba la kobe!

Wakati CCM waliamua kuunda tume na kuchunguza ni kwanini chama kinapoteza mvuto hususani kwa vijana, nyie mnaishia kuishi kwenye hoja nyepesi nyepesi zisizo na mashiko yoyote yale!!! Wakati REDET na Synovate wanatoa kura za maoni, mkaishia kukejeli na kuunda NGO yenu ambayo nayo ikatoa maoni yaliyoonesha eti Dr. Slaa angeshinda!!! Ingawaje CDM wanajigamba kuna wasomi lakini hawaendeshi mambo yao kisayansi na kuishia kwenye nadharia. Badala ya kujiuliza na kufanyia kazi ukweli kwamba ni kwanini CDM ukanda wa pwani hawakubaliki, mavuvuzela wa CDM waliopo JF wanaishia kuwakashifu watu wa pwani kwamba hawakusoma ndio maana hawaitaki CDM.....shallow analysis from shalowest thinkers!! Na kama watu wa pwani hawaitaki CDM kv hawana elimu basi inawezekana ndio maana walishindwa uchaguzi 2010 kv majority of Tanzanians hawana elimu.....sasa suala la kuibiwa kura hapo linatoka wapi?! Lazima mkubali kwamba huwezi kushinda urais ikiwa coverage yenu ni ndogo.....NASISITIZA, ukisikia sehemu fulani CDM ina nguvu, manake ni kwamba eneo hilo huwezi kubashiri kwa 100% kwamba chama fulani kitashinda. In contrast, ukisikia mahali fulani CCM ina nguvu, fahamu kwamba hapo CCM watashinda kwa kishindo. Hizi ni facts ambazo CDM wanapaswa kuzifanyia kazi kisayansi na sio kuleta porojo zisizo na maana. CDM mlishindwa kwa halali kabisa kv hamna coverage ya kutosha ukanda wa pwani na mashariki kwa ujumla, hamna coverage ya kutosha ukanda wa kati (Dom,Singida, na Tabora). Na hata huko waliko na coverage ya kutosha, unakuta ni kwenye baadhi ya wilaya tu kama sio majimbo! Mfano mzuri ni Arusha ambako magwanda wa JF wengi wanaamini ni ngome ya CDM ingawaje ukifanya analysis vizuri utagundua sivyo unless kama unaiangalia Arusha kama mji na sio mkoa!!!! So, utashinda vipi urais katika mazingira kama hayo?!
 
Ni offer ambayo haikustahili kutolewa kutoka CDM kwenda kwa RAis. SAsa Rais akisema hataki kukutana na hiyo Kamati ndogo CDM watafanya nini? Lakini vile vile japo wamejaribu lakini haiwezekani kumtenganisha Rais Kikwete kutoka kwenye Uenyekiti wa CCM. Kwa sababu maamuzi yoyote ambayo atayachukua kama Rais ni lazima yaende kwenye Chama chake!
MKJJ mimi nafikiri offer ya kukutana na rais si mbaya kama Mzito kabwela alivyosema hapo juu ni kuonyesha kwa wananchi na mataifa ushiriki wao katika kutafuta suluhu, na endapo mambo yatashindikana na kuamua kuchukua option ya mwisho watakuwa na cha kusema tulimshauri hakutusikiliza. Elewa Chadema si wajinga wameona wakitumia nguvu ya umma leo (ambayo CCM walikuwa wanategemea) CCM wanaweza kupata kisingizio na kwenda kwa wananchi kuwashitaki. Kitu kingine kama alivyosema MKabwela Donors kina Cameron wanaweza kuwauliza Chadema walikuwa na alternative gani nyingine iliyoshindwa. Ila mimi kama mimi hata Chadema wenyewe wanajua kuwa wanakwenda kukutana na rais kama ushahidi tu hakuna tangible solution yeyote itakayopatikana.
 
Ni kweli kutoa offer kunaonyesha kama kuna undumilakuwili flani.

Ama macho yangu?
 
Katiba: Chadema yataka kukutana na Kikwete Send to a friend
Monday, 21 November 2011 18:42
0diggsdigg

Geofrey Nyang’oro na Keneth Goliama
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeunda kamati ndogo ya watu sita kwa ajili ya kwenda kuonana na Rais Jakaya Kikwete kuwasilisha madai yake juu ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2011, uliopitishwa bungeni juma lililopita.

Kamati hiyo imeundwa katika mkutano wa dharura wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, uliofanyika Dar es Salaam juzi ili kukutana na Rais Kikwete kumjulisha kile walichoeleza kuwa upungufu wa muswada huo na kisha kumtaka atafakari kama ausaini kuwa sheria au la.

Akisoma tamko hilo kwa vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Chadema jana, Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe alisema kamati hiyo ya watu sita, inafanya taratibu za kumuona Rais Kikwete wakati wowote kuanzia sasa.

Mbowe alisema kamati hiyo itaongozwa na yeye, Katibu Mkuu Dk Willbrod Slaa, Makamu Mwenyekiti (Bara) Said Arfi na Makamu Mwenyekiti (Zanzibar), Said Issa Mohamed. Wengine ni Mshauri wa Masuala ya Siasa wa chama hicho, Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Abdallah Safari na Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu ambaye pia atakuwa katibu wa kamati hiyo wakati wa mkutano huo. “Hivi sasa taratibu za kumuona Rais zinaendelea, tutamuona wakati wowote kuanzia sasa na kumweleza mapendekezo yetu juu ya upungufu uliomo kwenye muswada wa sheria hiyo na kama atatusikiliza tutashirikiana naye akikataa tutawaeleza wananchi hatua za kuchukua,” alisema Mbowe.

Alisema ushiriki wa Chadema katika mchakato wa kuandika Katiba Mpya utategemea mazungumzo hayo akisema hiyo ndiyo fursa pekee inayoweza kutumika licha ya muswada huo kupitishwa ‘kibabe’.

“Bado kuna fursa za kisiasa na kijamii katika kujenga mwafaka wa kitaifa juu ya haja ya nia na mchakato na misingi ya Katiba Mpya, Kamati Kuu imesikitishwa na uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete badala ya kuzitumia fursa hizo amejiingiza kwenye upotoshaji uliofanywa na wabunge wa chama chake juu ya misingi na maudhui ya sheria hiyo,” alisema Mbowe na kuongeza,

“Kamati Kuu inaamini badala ya kuwaunganisha Watanzania na kujenga muafaka wa kitaifa unaohitajika katika kuandika Katiba Mpya, hotuba ya Rais Kikwete kwa wazee wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam imezidi kuwagawa wa Tanzania kwa misingi ya ushabiki wa vyama vya siasa kitendo hiki ni hatari kwa Taifa.”

Alisema Katiba si mali ya viongozi wala wanasiasa, bali ni ya wananchi inayohitaji mchango mpana wa maoni yao juu ya kuunda sheria itakayokusanya maoni na hata kuundikwa kwake.

Alisema Chadema kitaendelea kuwaelimisha wananchi na wadau wote juu ya ubovu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na umuhimu wa kuwa na sheria bora itakayoratibu uundwaji wa tume ya kukusanya maoni.
Chama hicho kimewaagiza wabunge na viongozi wake kufanya mikutano ya ndani na ya hadhara yenye lengo la kuwaelimisha wananchi juu ya sheria hiyo na madhara yake.

Yalia na Polisi

Kamati Kuu ya Chadema pia imelaani kitendo cha Serikali kukizuia chama hicho kufanya mikutano na maandamano nchi nzima kwa kile ilichodai ni kukinyima haki ya kikatiba ya kufanya shughuli zake.

“Polisi kuzuia mikutano ya hadhara ya Chadema na maandamano ya amani ya wananchi wanaopinga mchakato uliopitishwa kuwa sheria siyo tu kwenda kinyume na haki za msingi za kikatiba, bali pia unahatarisha amani na utulivu wa nchi,” alisema Mbowe.

Aliitaka Serikali kutoa tamko la kufuta amri hiyo huku akisisitiza kuwa Chadema kitaendelea kutumia njia zote za amani zilizopo ikiwemo mikutano ya hadhara na maandamano kama ilivyoainishwa katika Katiba ya sasa.

Kwa nini waligoma?
Awali, Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, alitaja sababu saba zilizowafanywa wasusie mjadala huo ikiwamo kukiukwa kwa Kanuni za Kudumu za Bunge wakati wa uwasilishwaji muswada huo.

Alisema Kamati ya Bunge iliingiliwa kazi zake kwa kuzuiliwa kukusanya maoni katika kanda 10 kama ilivyokuwa imepanga na badala yake maoni yakakusanywa kinyume na utaratibu na kuingizwa kwenye muswada huo.
Aliishutumu Serikali akidai kuwa iliingilia mchakato huo kwa kumtumia Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Akizungumzia hatua ya wabunge hao kususa, Dk Slaa alisema kamati ilipongeza hatua hiyo akisema ulikuwa uamuzi wa kijasiri uliowafanywa wasiwe sehemu ya kupitishwa sheria mbovu.

“Kamati Kuu imewapongeza wabunge wa Chadema kwa kususia vikao vya kupitisha sheria hiyo kwani ushiriki wao ungeipa uhalali wa kisiasa na kijamii, sheria ambayo haikuzingatia nia ya haja ya dhati ya kuweka utaratibu wa kisheria utakaoiwezesha nchi yetu kupata Katiba Mpya,” alisema.

Wabunge wa Chadema na wenzao wa NCCR-Mageuzi, walisusia kikao cha Bunge kilichojadili na kupitisha Muswada wa Sheria mpya ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011.
 
Ok,

Kwahiyo CDM wanaenda kumwomba JK awashirikishe kwenye uundaji wa katiba mpya?

Mapendekezo yao JK hajayaona ama wanadhani labda presence yao itasaidia?

Ama wanadhani hajapewa taarifa za kutosha kuhusiana na msimamo wao?

Lets wait and c...
 
Mbona habari hii inapingana na ile taarifa rasmi iliyotolewa na Mbowe? je mwandishi wa habari hizi kazitoa wapi; na je imetoka kwenye gazeti gani?
 
cjapenda,, mgekuwa na niya ya dhati na uchungu wa katiba? Mgewashirikisha pia nccr ambao waliwaunga mkono, ila kuwa ninyi cdm ni wabinafsi mnapenda sifa2 mnajiendea wenyewe, na mh, rais najuwa ana busara sana sidhani kama mapendekezo yenu atayakubali maana yatakuwa na msimamo wa kichama zaidi jambo ambalo watanzania wengi tunapinga
 
Back
Top Bottom