Tamko la Jumuiya ya Madaktari Tanzania

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
wakuu hii ni ile jumuiya ya madaktari iliyokuwa ikitoa matamko ya migomo hapo awali.

KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA
TAARIFA KWA UMMA JUU YA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI NCHINI TAREHE 18.09.2012

Kamati ya Jumuiya ya Madaktari Nchini , kwanza inapenda kutoa pole kwa Wanahabari wote nchini kwa kitendo cha kinyama ambacho Mwanaharakati na Mwandishi wa habari, Marehemu David Mwangosi alifanyiwa, hii ni ishara kuwa Jeshi la Polisi wameamua kutumia njia ya kuua raia ili kujenga hofu na woga miongoni mwa wapenda demokrasia na maendeleo nchini.
Pia tunapenda kulaani kitendo cha Serikali kupitia Wizara ya Michezo, Habari na Utamaduni kulifungia gezeti makini la Mwanahalisi kwa sababu ya kutoa taarifa za ukweli juu ya waliotaka kukatiza uhai wa Dr.Ulimboka Stephen, Jamii ya Madaktari na watanzania wengi bado wanaamini kuwa waliotajwa na gazeti la Mwanahalisi ni miongoni mwa waliohusika na kutekwa, kuteswa na kutelekezwa kwake na si yule anayesemekana kuwa na matatizo ya akili aliyedaiwa kukamatwa na Suleimani Kova. Hivyo tunalitaka Jeshi la Polisi litoe ripoti yake ya Uchunguzi ili kubaini ukweli wa taarifa hii.

Pia, tunachukua nafasi hii kupongeza mshikamano ambao Madaktari wameendelea kuuonyesha licha ya changamoto nyingi tunazopitia, ni vema ikafaamika kuwa ni katika kipindi hiki ambacho Mwenyekiti wa MAT na MAT imefunguliwa kesi 2 mahakamani, Ni katika kipindi hiki ambacho zaidi ya interns 300 wanasubiri kuitwa kuhojiwa na MCT bila kujua ni lini hilo litafanyika, Ni katika kipindi hiki ambacho Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari anapata mapumziko baada ya kutoka katika Matibabu nchini Afrika Kusini, lakini ni katika kipindi hiki ambacho mpaka sasa hakuna hata hoja moja ya Madaktari imefanyiwa kazi na Serikali.

Tunapenda ieleweke kuwa suala la madai ya Madaktari si tukio, ni mchakato ambao utaendelea kwa vizazi vya sasa na vijavyo, ndio maana tumeshuhudia migomo hii katika nyakati tofauti pamoja na kujitokeza kikundi au mtu kutumiwa kuomba msamaha kwa lengo la kudhalilisha taaluma na kurudisha nyuma jitihada za kuboresha hali ya afya nchini na maslai ya watumishi kwa ujumla.
Kuhusu suala la interns, Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 10, Julai 2012, Baraza la Madaktari Nchini lilitoa taarifa kwa umma kuwa imesitisha leseni za muda kwa Madaktari waliochini ya mafunzo kwa vitendo, pia waliahidi kuwaita kwa nia ya kuwahoji mmoja mmoja pindi wakatapokamilisha uchunguzi wao, cha kushangaza ni kwamba miezi 2 sasa imepita bila hilo kufanyika.
Katika vikao mbalimbali ambavyo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Naibu wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, na Kaimu Katibu Mkuu wameshiriki, wamekuwa wakisisitiza kuwa hili lipo kisheria na interns wasuburi kuitwa kwa ajili ya kuhojiwa. Hivyo tunapenda kutumia nafasi hii kuitaka MCT itekeleze kwa haraka majukumu yake kwa lengo la kuharakisha upatikanaji wa haki.

Hivyo basi Kamati ya Jumuiya ya Madaktari imejiandaa vya kutosha na taratibu za kisheria na itahakikisha inaweka wakili pale interns watakapoanza kuhojiwa kwa kuwa sheria inayounda MCT inatoa hiyo nafasi.
Mwisho kabisa tunapenda kutoa wito kwa interns kutumia hekima na busara katika kipindi hiki kigumu, waepuke kutumiwa na kikundi cha watu ambao wanatumika au wanajitumia kwa maslai ya kustarehesha watawala.


IMETOLEWA NA; KAMATI YA JUMUIYA YA MADAKTARI TANZANIA.
 
Haya matamko sasa ni balaa
Kila mmoja anakuja na lake
Tusubiri tuone wala wa jana nao watasema nini juu ya tamko hili
 
naona 'fushi'limeanza upya kabisa.niliwahi kusema migogoro haiishi kwa propaganda za kisisasa.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
wakuu hii ni ile jumuiya ya madaktari iliyokuwa ikitoa matamko ya migomo hapo awali.

Mimi nilikuwa nasubiri kusikia kauli ya MAT ama jumuiya ya madaktari iliyokuwa chini ya Dr. Ulimboka.
Usaliti umekuwa ni sehemu ya maisha ya kawaida ya mtanzania. Madaktari wameasalitiana kama waandishi wa habari wanavyosalitiana juu ya kifo cha mwenzao marehemu Daudi Mwangosi. Walikubaliana kwamba wasiripoti habari za polisi walau kwa siku hizi arobaini lakini wapi kesho yake tu wengine wakaanza kutiririka na kauli za marpc.
 
Full confusion...wengine wanageuza fani kama hizi ni vile vyeo vya siasa wanavyogombania na kupita bila kupingwa.
 
ngoja tuone kama tbc wataishadidia habari hii kama walivyofanya kwa ile ya jana.i guess dsmage is already done.
 
tunajua mwenyekiti wa jumuiya ya madaktari ni dr ulimboka, je na yeye ameshiriki kuandika taarifa hii??

hii taarifa imetolewa na makamu mwenyekiti DR Godbless charles.obvious Dr Ulimboka atakuwa kashirikishwa.
 
Wale wa jana,nilisha waona Wanafiki..,! Utaombaje msamaa kwenye kudai aki.? G'ment shld be the1 to appologize..
 
Sasa ninyi doctors kwanini mnasalitiana? Tuuangane tuikomboe nchi yetu, tatizo uchaguzi ukifika mnasahau matatizo yetu, dhaifu yetu mtakuwa kama mateachers
 
Back
Top Bottom