Tamko la Ikulu juu ya tishio la kuuawa viongozi wa CHADEMA

Atuambie vifo vya Kolimba,Kombe nk wahusika kina nani?Anajidanganya akidhani yeye anaishi peponi kumbe bure kabisa,ukweli jamii inaufahamu.

Na cdm watuambie Chacha wangwe kwa nn walimuua kwa uroho wa madaraka wa Mbowe?????
 
tamko toka ikulu

katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili

ya kuwaua viongozi wa chadema.

Huku akihoji sababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wa taifa

haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana Nini hasa idara ya usalama wa taifa

ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.

source;vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo wavuti

Did u expect wakubali?this time salva amechuna sefue team work
 
nilikuwa siamini kama asili ya watu weusi ni manyani, lakini kwa tamko hili toka ikulu inajitosheleza kuonesha asili ya waliko tokea. time will tell. itafika karibia na uchaguzi wataanza kutafutana wao kwa wao hapo sinema itakuwa imenoga
 
[h=6]Peter Mwininga
[/h][h=6]‎'Tokea dkt slaa atoe Tuhuma dhidi ya Chombo chetu Muhimu na nyeti KUKITUHUMU KINAWAFUATILIA KUWAUWA,NI MWENDAWAZIMU.UNAWEZA FUATILIWA MIENENDO YAKO HASA KWA MTAZAMO WA USALAMA WA TAIFA NA SI WEWE KAMA WEWE,KAULI ZINGINE TUCHUNGE MIDOMO YETU,SLAA SIO MTU MZURI,HATA KANISA LILIAMUA KUJIWEKA PEMBENI NAE,NI HATARI KWA TAIFA.mwenye kuelewa aelewe nawasilisha[/h]
 
tamko toka ikulu

katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili

ya kuwaua viongozi wa chadema.

Huku akihoji sababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wa taifa

haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana Nini hasa idara ya usalama wa taifa

ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.

source;vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo wavuti

Na ambao ni tishio kwa viongozi wa CCM inakuwaje?! Halafu inaonesha huyu ndio mmoja wa viongozi wa idara hii katika ngazi za juu.

Kama hawaui, nani anayeua?
 
Ni dalili kuwa saa ya ukombozi imekaribia,Watafanya kila njia kuzuia mapinduzi lakini haitawezekana.
Aluuuuuta Continueee.
 
[h=2] Dk. Slaa, Mnyika kuhojiwa Polisi [/h] Jumanne, Julai 10, 2012 03:39 Na Maregesi Paul, Dodoma

SIKU moja baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbles Lema kuishutumu Serikali kuwa inataka kuwaua, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, ameliagiza Jeshi la Polisi nchini, liwahoji viongozi hao.
Alisema amelazimika kufanya hivyo, ili kupata ukweli wa kilichosemwa na viongozi hao, wakiongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
 
"Ndugu waandishi wa habari, nimewaita hapa ili tuzungumzie suala moja kubwa ambalo lilizungumzwa jana na viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.

"Katika mazungumzo yake kwa waandishi wa habari, Mbowe alisema Usalama wa Taifa wana mpango wa kuwaangamiza kwa sumu au kwa ujambazi baadhi ya viongozi wa chama hicho.

"Mbowe alisema pamoja na vitisho hivyo, bado hawajatoa taarifa hizo polisi kwa sababu hawaliamini Jeshi la Polisi.

"Kwa hiyo, sisi kama Serikali tumelitafakari hili kwa sababu suala la ulinzi wa wananchi siyo hiari, bali ni suala la wajibu wa kikatiba na kisheria.

"Kwa hiyo, tunapozungumzia usalama wa raia, vyombo vyetu havitamuomba mtu ruhusa kumlinda kwa sababu ni wajibu na kazi yetu kuwalinda Watanzania, tunawataka Watanzania kutosita kutoa taarifa za vitisho katika vyombo vya dola.

"Nichukue fursa hii kuwataka viongozi wote wa kisiasa kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika, hasa polisi, kwa sababu hiyo ni moja ya majukumu yao kikatiba.

"Kwa hiyo, ili kupata uhakika wa taarifa hizi, nimeliagiza Jeshi la Polisi, liwahoji hao wanaosema wanataka kuuawa, waeleze nani anawatisha kisha hatua zichukuliwe," alisema Dk. Nchimbi.

Katika mazungumzo yake, Waziri Nchimbi alikemea tabia ya viongozi wa kisiasa kuishutumu Serikali hadharani badala ya kupeleka malalamiko yao polisi ili yakafanyiwe kazi.

"Tabia inayoanza kujengeka sasa ya viongozi kupiga kelele nje ya utaratibu ni tabia isiyokubalika, kwa sababu inadhamiria kujenga hofu miongoni mwa Watanzania na inawafanya Watanzania wasiamini vyombo vyao vinavyowalinda kwa mujibu wa Katiba na Sheria.

"Lakini vile vile kuimarisha umaarufu wa kisiasa, bila sababu za msingi ni jambo la kweli kwa mwanasiasa kukubalika katika jamii, lakini kukubalika kwa utaratibu huu, hatuwezi kuukubali.

"Kama Serikali nayo ingekuwa inataka kukubalika kwa wananchi kwa njia za ovyo kama wanazotumia Chadema, basi nayo ingefanya hivyo, lakini hatuwezi kufanya hivyo kwa sababu hakuna sababu za msingi," alisema.

Dk. Nchimbi alitolea mfano wa tukio la viongozi wa Chadema kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, ambapo alisema vyombo vya dola havikukurupuka kuwakamata ama kuwapeleka mahakamani viongozi wa Chadema, ingawa walikuwa watuhumiwa namba moja.

"Chadema hawaviamini vyombo vya dola, lakini ieleweke dola inafanya kazi kwa utaratibu na kwa kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio husika.

"Kwa mfano, katika lile tukio la kifo cha Chacha Wangwe, Chadema walikuwa ni kati ya watuhumiwa, lakini hatukuwakamata, polisi walifanya uchunguzi mwishowe dereva wa Chacha Wangwe akakamatwa na kufikishwa mahakamani.
 
Nimeipenda, ila hapo penye nyekundu pananipa shida. Tungefunguka zaidi kama Ktb Kioongizi angetueleza watu waliowahi kuuwawa na usalama wa taifa, na waliuwawa kwa sababu zipi. Pia angetueleza, watanzania ambao wamedhuriwa kama Dr Ulimboka, Usalama wa taifa ulifanya/umefanya nini hadi sasa kutuwezesha kubaini yaliyopelekea usalama wa Daktari huyu kuwa mashakani kiasi hiki. Ingependeza pia kujua maslahi ya kwanza ya usalama wa taifa ni yepi, kati ya Rais (ambaye ni mwenyekiti wa chama) na Watanzania bila kujali itikadi zao.
Pia ingekuwa bora akatueleza ni nini mpaka kati ya maslahi binafsi (watawala, viongozi wa UWT, nk) na usimamizi wa taasisi hii nyeti?

Nono,

Hata Bashar Assad atakuambia kwamba wanampenda , lakini ameshaua watu wa Syria wanaokisiwa kuzidi elfu 15,000 . Kwa hiyo usitarajie Jibu tofauti .

Mimi nazichukulia tuhuma gainst Uslama aw Taifa kuwa ni nzito na kuwa sijui Othman anasema je ? State agents might not come to the line light but Mkuu wao na Cheif Secretary tunawafahamu. Pnatakiwa tamko tena makini.

Tusije leta Scotland Yard au KGB kuchunguza!
 
Kwa ujumla taarifa na matamshi yoyote ya kuuana nayapokea kwa masikitiko sana. Aidha, kinachosikitisha zaidi ni pale tunaposhabikia na kujiaminisha kuwa hili linafanywa na TISS, hii inasikitisha sana na tusipoangalia wapo watakaochukua mwanya huo kuendelea kuwaangamiza wengine na sisi kuendelea kusema ni serikali. Tuseme pale inapoonekana ni muhimu. Kwa kweli tunakoelekea Tanzania siyo kuzuri hasa kwa hili suala la umma kufanya uchunguzu na kuhukumu. Ndiyo kuna mapungufu katika mifumo halali yenye mamlaka kuhusu masuala mabalimbali, lakini ushabiki wetu ndiyo unafanya utendaji huo mdogo wa taasisi zetu kuwa mgumu zaidi.

Hivi tunavyofanya ni kufungua mianya kwa waalifu kufanya unyama na ualifu na kwa kuwa tayari tunajijengea jamii imani potofu itakuwa vigumu kuwadhibiti wahalifu ambao wataanza ku-take advantage ya loophole tunayoitengeneza.
 
huyu mzee nilikuwa namheshimu sana lakini kama ni kwelikaongea hili basi naye ni punguwani kabisa
 
“Ndugu waandishi wa habari, nimewaita hapa ili tuzungumzie suala moja kubwa ambalo lilizungumzwa jana na viongozi wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.

“Katika mazungumzo yake kwa waandishi wa habari, Mbowe alisema Usalama wa Taifa wana mpango wa kuwaangamiza kwa sumu au kwa ujambazi baadhi ya viongozi wa chama hicho.

“Mbowe alisema pamoja na vitisho hivyo, bado hawajatoa taarifa hizo polisi kwa sababu hawaliamini Jeshi la Polisi.

“Kwa hiyo, sisi kama Serikali tumelitafakari hili kwa sababu suala la ulinzi wa wananchi siyo hiari, bali ni suala la wajibu wa kikatiba na kisheria.

“Kwa hiyo, tunapozungumzia usalama wa raia, vyombo vyetu havitamuomba mtu ruhusa kumlinda kwa sababu ni wajibu na kazi yetu kuwalinda Watanzania, tunawataka Watanzania kutosita kutoa taarifa za vitisho katika vyombo vya dola.

“Nichukue fursa hii kuwataka viongozi wote wa kisiasa kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika, hasa polisi, kwa sababu hiyo ni moja ya majukumu yao kikatiba.

“Kwa hiyo, ili kupata uhakika wa taarifa hizi, nimeliagiza Jeshi la Polisi, liwahoji hao wanaosema wanataka kuuawa, waeleze nani anawatisha kisha hatua zichukuliwe,” alisema Dk. Nchimbi.

Katika mazungumzo yake, Waziri Nchimbi alikemea tabia ya viongozi wa kisiasa kuishutumu Serikali hadharani badala ya kupeleka malalamiko yao polisi ili yakafanyiwe kazi.

“Tabia inayoanza kujengeka sasa ya viongozi kupiga kelele nje ya utaratibu ni tabia isiyokubalika, kwa sababu inadhamiria kujenga hofu miongoni mwa Watanzania na inawafanya Watanzania wasiamini vyombo vyao vinavyowalinda kwa mujibu wa Katiba na Sheria.

“Lakini vile vile kuimarisha umaarufu wa kisiasa, bila sababu za msingi ni jambo la kweli kwa mwanasiasa kukubalika katika jamii, lakini kukubalika kwa utaratibu huu, hatuwezi kuukubali.

“Kama Serikali nayo ingekuwa inataka kukubalika kwa wananchi kwa njia za ovyo kama wanazotumia Chadema, basi nayo ingefanya hivyo, lakini hatuwezi kufanya hivyo kwa sababu hakuna sababu za msingi,” alisema.

Dk. Nchimbi alitolea mfano wa tukio la viongozi wa Chadema kuhusishwa na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, ambapo alisema vyombo vya dola havikukurupuka kuwakamata ama kuwapeleka mahakamani viongozi wa Chadema, ingawa walikuwa watuhumiwa namba moja.

“Chadema hawaviamini vyombo vya dola, lakini ieleweke dola inafanya kazi kwa utaratibu na kwa kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio husika.

“Kwa mfano, katika lile tukio la kifo cha Chacha Wangwe, Chadema walikuwa ni kati ya watuhumiwa, lakini hatukuwakamata, polisi walifanya uchunguzi mwishowe dereva wa Chacha Wangwe akakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Mpaka sasa ni matamko matatu,Nzoka,Nchimbi na Sefue sijui la nani litafuata.Both Statements differ in substances,Kwa viongozi walioko makini na hasa ambao wana jukumu la kulinda usalama wa Taifa hili,trusingetemea wanakuwa one sided.Kinachoonekana kwenye matamko yote ni lawama na kujivua lawama.Hii inatishia uhai wa Taifa na watu wake.
 
Katika mazungumzo yake, Waziri Nchimbi alikemea tabia ya viongozi wa kisiasa kuishutumu Serikali hadharani badala ya kupeleka malalamiko yao polisi ili yakafanyiwe kazi.

"Tabia inayoanza kujengeka sasa ya viongozi kupiga kelele nje ya utaratibu ni tabia isiyokubalika, kwa sababu inadhamiria kujenga hofu miongoni mwa Watanzania na inawafanya Watanzania wasiamini vyombo vyao vinavyowalinda kwa mujibu wa Katiba na Sheria.

"Lakini vile vile kuimarisha umaarufu wa kisiasa, bila sababu za msingi ni jambo la kweli kwa mwanasiasa kukubalika katika jamii, lakini kukubalika kwa utaratibu huu, hatuwezi kuukubali.

"Kama Serikali nayo ingekuwa inataka kukubalika kwa wananchi kwa njia za ovyo kama wanazotumia Chadema, basi nayo ingefanya hivyo, lakini hatuwezi kufanya hivyo kwa sababu hakuna sababu za msingi," alisema.

"Chadema hawaviamini vyombo vya dola, lakini ieleweke dola inafanya kazi kwa utaratibu na kwa kufanya uchunguzi wa kina juu ya tukio husika.
.

Naona Nchimbi ameamua kutoa tamko na matishio vyote kwa pamoja. Nchimbi anaposema "hawatakubali CHADEMA kupiga kelele nje ya utaratibu" anamaanisha nini? Hawatakubali (yeye na nani) na watafanya nini kama CHADEMA wataendelea kuiongea 'nje ya utaratibu' anaoutaka yeye Nchimbi?

Lakini Nchimbi amejikita sana kwa CHADEMA na kusahau kadhia iliyomkuta Dr Mwakyembe. Nchimbi na wakubwa wengine wangekuwa na ngozi ngumu wangeagiza 'independent survey' ili kubaini imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi. Nadhani hii ingemsaidia sana Nchimbi kujua ni wapi au nini anatakiwa kufanya badala ya kuendelea kuimba zilipendwa.

NB: Tumekuwa tukisikia kelele za kutaka vijana wapewe nafasi za uongozi, ningetaka kuona ujana au faida za umri wa kiongozi kwenye hii hali inayoendelea sasa hivi nchini. Wananchi wanaanza kuwakimbia polisi, waziri kijana anaweza kuwa na jipya to reverse the trend?
 
Back
Top Bottom