Tamko la Ikulu juu ya tishio la kuuawa viongozi wa CHADEMA

Malaria Sugu

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
2,653
264
Tamko toka ikulu

Katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili ya kuwaua viongozi wa chadema.

Huku akihoji sababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wa taifa haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana Nini hasa idara ya usalama wa taifa ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.


source;vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo wavuti
 
Atuambie vifo vya Kolimba,Kombe nk wahusika kina nani?Anajidanganya akidhani yeye anaishi peponi kumbe bure kabisa,ukweli jamii inaufahamu.
 
pengine hajui kuwa kuna ambao hawapendi yanayofanywa na TISS katika kipindi cha miaka saba sasa!
 
Poleni sana, msipochunguza haya madai kwa makini, mjue ukimwi hauchagui chama, wala rangi, wala kabila, wala cheo. Ikitokea kuna kikundi ndani chenye huo mchezo, hata mkanushaji yuko hatarini.
 
tamko toka ikulu

katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili

ya kuwaua viongozi wa chadema.

Huku akihoji sababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wa taifa

haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana Nini hasa idara ya usalama wa taifa

ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.



source;vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo wavuti

Nimeipenda, ila hapo penye nyekundu pananipa shida. Tungefunguka zaidi kama Ktb Kioongizi angetueleza watu waliowahi kuuwawa na usalama wa taifa, na waliuwawa kwa sababu zipi. Pia angetueleza, watanzania ambao wamedhuriwa kama Dr Ulimboka, Usalama wa taifa ulifanya/umefanya nini hadi sasa kutuwezesha kubaini yaliyopelekea usalama wa Daktari huyu kuwa mashakani kiasi hiki. Ingependeza pia kujua maslahi ya kwanza ya usalama wa taifa ni yepi, kati ya Rais (ambaye ni mwenyekiti wa chama) na Watanzania bila kujali itikadi zao.
Pia ingekuwa bora akatueleza ni nini mpaka kati ya maslahi binafsi (watawala, viongozi wa UWT, nk) na usimamizi wa taasisi hii nyeti?
 
tamko toka ikulu

katibu mkuu kiongozi balozi ombeni sefue atamka kwamba hakuna mpango wowote unaoratibiwa na idara ya usalama wa taifa kwa ajili

ya kuwaua viongozi wa chadema.

Huku akihoji sababu za serikali kutaka kuwaua viongozi wakati si tishio lolote kwa wananchi huku akisema idara ya usalama wa taifa

haiko kwa ajili ya kuua raia au viongozi bali kulinda maslahi ya taifa sasa kwa nini wawaue wana Nini hasa idara ya usalama wa taifa

ifanye hivo, idara hii haifanyi kazi kisiasa inaangalia maslahi ya watz wote.



source;vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo wavuti

Usalama wa taifa umelinda maslahi gani hapa:-
  • mikataba mibovu ya madini
  • ufisadi na utoroshaji raslimali na fedha za watanzania
  • rushwa kubwa za viongozi
 
kama kazi ya usalama wa taifa ni kuangalia maslahi ya taifa, kwanini ufisadi umekithiri hapa nchini, rushwa ndo usitheme, wanafiki tu hao, kazi kubwa ya usalamawa taifa ni kulinda maslahi ya viongozi tena mafisadi.



" ZA MBAYUWAYU CHANGANYA NA ZA GONGAGONGA"

" ZA BALOZI OMBEN SEFUE CHANGANYA NA ZAKO"
 
Tamko lipo shalow kama limetoka kwa four ya shule ya kata. Tamko linaibua maswali mengi kuliko majibiu!!!!
 
Ikulu ya Tanzania imekuwa kama pango la wacheza kamari. Tuhuma nzito namna ile wanajibu kirahisi bila uchunguzi!
 
ivi slaah! lema mnyika! nikama nani katika nchii hiii! mpaka watishiwe kuuwawa? hawa adhari na wanatishia kitu gani nchi hii! mbona ni watoto wadogo sana katika hii nchi! kuna watu wanaoweza kutishia hii nchi na kuna watu ni hatari wakuweza kuadhiri hii nchi! sio hao watoto wadogo! bali wanapoteza muelekeo tu hawa wanasiasa! mtu wa slaa kwenye usalama wa taifa soon atatoka madarakani sasa izi ni njama za kumchafua kaimu kwa kuwa sio mwana siasa mwenzao! waachwe kuawa wakina edward m ambao sasa ni wako BBc ambao walitishia hii nchi itakuwa ha watoto jamani! unafki tu huu! afu ni woga
 
Back
Top Bottom