Tamko la CUF kuhusu vurugu za Zanzibar

waongo hau Uhamsho ndo CUF na CUf ndo uhamsho wamechange jina tu nmesikitika jana naingia msikitini Eti watu wanafurahi kuuwa kwa Polisi.....ndo utajua hakuna Udini ni siasa.....na hao wanaofurah nawajua ni wanachama wa CUF damu kabisa mbuzi hao
 
KWA NINI KISONGE WAWEWESEKA NA
CUF? Maskani ya KISONGE ndio kinara wa
kucheza ngoma ya baadhi ya
viongozi wa serikali/CCM ya
kupinga maridhiano ya wazanzibari,
serikali ya Umoja wa kitaifa na na
kujenga farka, fitna, chuki, ukabila, ugozi, chokochoko na uvunjifu wa
umoja na mshikamano miongoni
mwa wazanzibari imechomwa moto
kufuatiwa vurugu za hivi juzi
baada ya kutekwa nyara kwa
Sheikh Farid. Katia kuifanikisha azma hyo KISONGE na
wanamtandao wenzao wameapa
kutofautisha baina ya CUF na
harakati za UAMSHO. Kwa kuwa
usalama wa taifa wako dhidi ya
jumuiya ya UAMSHO hazikwepeki tuhumakua wao ndio
wanaotuhumiwa kuandaa kiufundi
mpango wa kumteka Sheikh Farid.
Pia hawawezi kukwepa tuhuma kua
ndio walioandaa kuchomwa kwa
maskani hiyo na nyengine ghafla bila ya kuchelewamara tu
ziliporipuka ghasia hapo juzi. Lengo kuu la mtandao ambao
maskani ya KISONGE linaufanyia kazi
ni kuizima nuru njema ya umoja wa
wazanzibari ambayo ndio silaha
pekee ya kuirejesha Jamhuri ya
watu wa Zanzibar yenye mamlaka kamili. Lengo ni lile lile linaliondaliwa
na system chini ya Jamhuri ya
Muungano na vibaraka wao wa
Zazibar kuwa wazanzibari
wasambaratike, wagombane,
wasiwe wamoja, wasiaminiane na wasisikilizane. Wanajua wazanzibari wakiwa wamoja
wanapata jukwaa na sauti ya
pamoja ya kujadili na kudai nchi
yao huku wakisahau mawazo ya
tofauti zao za kisiasa na badala
yake kuuhisi machungu ya kudhalilika kwa nchi yao.
Ukiwaondoa wazanzibari katika
maelewano na umoja huu kwa
kujenga mazingira ya kila upande
uone bado sisi ni maadui kumbe
baina yetu bila shaka unafanikisha mpango wa kuwagawa wazanzibari
katika agenda tunayoipigania. Naendelea kuwafahamisha vijana
wenzangu vita vya KISONGE ni dhidi
ya CUF na si vinginevyo. Hawana
vita dhidi ya UAMSHO. Sasa tu ni
kwamba wanaumia vyema mtaji
mpya wa UAMSHO. Wanajua inayoudhibiti umoja wa kitaifa na
mwenye engine ya mabadiliko
wanayoyapinga ni CUF. Hivyo
wanafanya kila wawezalo ili CUF
ionekane ndio chanzo cha vurugu
zote hizi, ndio mpangaji, msimamiaji na mtekelezaji. Lengo alo kuu ni
kujenga picha ya uongo kwa CCM
wenzao kuwa CUF si wenzeao na
hawako pamoja na CCM na
wameunda UAMSHO ili waihujumu
CCM/ serikali nje ya maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa. Hili
ndilo linalojengwa na mtandao wa
KISONGE. Kufikia hapo ni
kuwarudisha nyuma wale wote
wenye imani na maridhiano na
umoja wa kiaifa kutoka CCM waone kumbe CUF hawako katika mstari
wa maridhiano. Ndio maana CCM wa
KISONGE wanapindisha ukweli na
kuweka hoja "kwa nini vurugu hizi
zichome maskani za CCM pekee
kama kweli hazikufanywa na CUF?" Mimi sina imani kama maskani za
CCM zimechomwa na wafuasi wa
UAMSHO kwani tumezoea mara
zote kila kunapoashiria kuwepo
kwa harakati za UAMSHO kama vile
mihadhara askari polisi hujipanga kuzilinda maskani mbili za CCM,
KACHORORA na KISONGE. Siku
ambayo KISONGE iliyochomwa moto
askari walikuwepo wapi? Huu bila
shaka ni mpango uliopikwa vyema
yaani polisi wasije na badala yake kundi la vijana lipelekwe kutia
moto ili ionekana wametia moto
UAMSHO. UAMSHO ni taasisi ya kidini
na ilijitangaza wazi haina
mahusiano na chama chochote na
wafuasi wao ni kutoka vyama vyote. Katika kuifuta picha hii ya
kwamba UAMSHO hawana chama,
KISONGE walianza na uchokozi wa
kuandika machapisho ya kila aina
katika mabango yao ambayo
yanatoa ujumbe kuwa UAMSHO ni CUF. Sisi CUF kwa kufahamu
wanachokifanya huwa
hatuchokozeki. Tunaielewa vyema
dawa yao ni kuwadharau na kweli
tumewadharau wamedharaulika.
Lakini wako vijana wa UAMSHO ambao wanachokozeka kila ambapo
kisonge wanapoongeza kejeli na
mausi dhidi ya UAMSHO. Tuanazidi kuambia vijana hao kuwa
huo ni mtego wa KISONGE
Unaodhaminiwa na mtandao
ulioshtushwa na umoja wetu
wanataka muingie kichwa kichwa
katika mtego huo (kama hamjaingia) ili azma yao itimie.
Vipuuzeni vitimbi hivi na badala
yake busara na akili itumike
kupambana navyo. Viongozi wa CUF
mara ngapi wamekamatwa? Mara
ngapi wamefunguliwa kesi? Na mara ngapi wamefungwa
magerezani? Mbona
hawakuhamasisha mapigano? Na mbona wafuasi hawakuingia
barabarani kupigana? Kwa sababu
viongozi wanawalea wana CUF kwa
misingi ya busara na taratibu
sahihi za kupambana na mfumo huu
kandamizi. Ukikurupuka mfumo ndio unakutaka ili ukusambaratishe
kabisa. Mara baada ya KISONGE kuungua,
walitoa taarifa kupitia facebook
kuwa "jiandaeni MTENDENI (Makao
makuu ya CUF) wakati wowote
kuanzia sasa itawaka". Hii
inaonyesha wazi kuwa wao wako dhidi ya CUF kwani wanajua ndiko
ziliko fungua za kasha la
maridhiano na umoja wa kitaifa
wanazozitafuta. Kama hiyo haitoshi wamechapisha katika
kipande cha ubao wao wa uchezi
kilichobakishwa na moto "CUF OYEE, MAPINDUZI DAIMA"
wakimaanisha "hongereni CUF kwa
kutuchomea maskani yetu lakini
tunawambia MAPINDUZI DAIMA" Vijana tutulie tutumie busara,
makundi kadhaa wa kadhaa
yameshaandaliwa na system kamavile ubaya ubaya, mbwa
mwitu na kadhalika ili wafanye
hujuma nyingi kupitia jina la
UAMSHO na huku mtandao
wanahusisha UAMSHO na CUF.
Wazanzibari tunaotaka jamhuri yetu tutulie tufuate kamaba ya
pamoja, akitokea mtu akaikata hii
kamba ya pamoja tutapambana
nae kwa nguvu ya pamoja wakati
ukifika.
 
EMT Nilikuwa napita tu, kumbe hili linahusu "Jamhuri ya Watu wa Zanzibar". Kumbukumbu zilikuwa zimenitoka kidogo
 
Last edited by a moderator:
Taarifa hiyo hata si nzuri kwa Muungano maana iko biased, haiongelei madhara yaliyofanyika Bara!
Iko low contentwise, na kikubwa hapo ni kumsikitikia Farid Basi!
 
Jussa na Seif wapo chama gani???
Alafu hapo kwenye kukata miti hovyo pamenichekesha, hata sijui kwa nini.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wacha uongo mtu mzima ww!!!


Ikumbukwe kuwa vurugu hizi zilianza pale CUF ilipotamka kuwa haimtambui Mbunge aliyechaguliwa hivi karibuni (Jimbo la Bububu). CUF Mnajitoaje kwenye hili? Nionacho mimi mnajikosha ili muonekane na ninyi mnapinga jambo hili lakini ukweli mnaujua
 
Hilo linaloitwa Tamko halina Tamko lolote. Ni maneno tu mtu kama mimi ameandika tu. Haina uzito wowote, labda angesoma Tamko la Maaskofu jana angeweza kuona ni maneno gani yanawekwa kwenye Tamko.
Huu ni usanii tu wa CUF
 
CUF yuko ndani ya ndoa mumewe CCMMFUU kamtuma aelezee nini? hakuna jipya bali tulia kwenye ndoa mpaka....
 
Back
Top Bottom