Tamko la CHADEMA kuhusu uteuzi wa Biswalo Mganga kuwa Jaji wa Mahakama Kuu

BAVICHA Taifa

Senior Member
Jul 25, 2013
107
1,000
Itakumbukwa kwamba tarehe 11.05.2021 Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu alitangaza uteuzi wa nafasi za Majaji wa Mahakama ya Rufani pamoja na Mahakama Kuu ya Tanzania uliofanywa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan.

Kutokana na unyeti wa nafasi hizo katika kusimamia haki nchini tumeona ni muhimu kusema baadhi ya mambo ambayo tunaamini yalipaswa kufanyiwa kazi zaidi ili kuweza kupata Majaji wenye sifa zisizotiliwa shaka na umma.

Uteuzi wa Biswalo Mganga ambaye alikuwa DPP na ukizingatia aliyoyafanya na kusababisha kuongeza mahabusu katika Magereza kwa kuongeza wigo wa makosa yasiyokuwa na dhamana, hali iliyopelekea Raid Magufuli kuanza ziara ya kutembelea magereza na kuagiza utafutwe utaratibu wa kuondoa msongamano katika magereza nchini.

Kuna uwezekano wa yeye kuwa na mgongano wa kimaslahi kwa sababu mashauri yanaweza kwenda mbele yake kwa rufaa au kuanza kusikilizwa wakati yeye alishiriki moja kwa moja katika kuyaandaa.

Aidha , kuna tuhuma dhidi ya aliyekuwa DPP Biswalo Mganga katika kufuatilia na kushughulikia mchakato wa kampuni ya MR.KUKU FARMERS LIMITED iliyokuwa imesajiliwa na wakala wa usajili wa biashara na leseni (Brela)na kupewa cheti cha usajili Namba 141097253 tarehe 21 February, 2020.

Kampuni tajwa hapo juu ilikuwa inatambuliwa na Mamlaka zote za kodi nchini na ilikuwa na TIN namba pamoja na cheti cha kulipia kodi ya ongezeko la thamani (VAT), na ilipewa cheti cha kuthibitisha kuwa walilipa Kodi (tax clearance) kilichotolewa na TRA.

Kampuni hii ilichukua fedha za wananchi kwa njia ya kuwapatia hisa ili wawe sehemu ya wamiliki wa Kampuni.

Jeshi la Polisi lilimkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Kampuni hiyo na kumfungulia mashtaka ya kuendesha biashara kinyume na sheria na hivyo akafunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi.

Shtaka hilo liliendeshwa kwa utaratibu wa plea bargain uliosimamiwa na DPP , na hatimaye fedha zote zilizokuwa kwenye akaunti ya Kampuni zaidi ya shilingi Bilioni 10 Zilichukuliwa na DPP, na kuwaacha waliokuwa wamenunua hisa bila kujua wafanye nini .Jambo hili linahitaji kuchunguzwa ili kuona kama Biswalo alitekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.

Aidha , DPP Biswalo anatuhumiwa kuwa alikuwa akiwataka wale wote waliokuwa wamekubalina kwa utaratibu wa plea bargaining kumlipa yeye fedha kinyume na kanuni kifungu cha 21 ambacho kinawataka watuhumiwa kumlipa msajili wa hazina ambaye atapokea malipo hayo kwa niaba ya serikali.

Vilevile, aliyekuwa DPP Biswalo anatuhumiwa kuendesha kesi mbalimbali za viongozi wa Chadema kisiasa badala ya kufuata misingi ya sheria. Ana tuhuma za kuzuia Mahakama kutoa dhamana kwa kesi za viongozi wa Chadema kwa misukumo ya kisiasa kama alivyofanya kwenye kesi ya Mhe. Godbless Lema, Mhe.Freeman Mbowe na wengine wengi.

Mapendekezo

1. Tunapendekeza kuundwa Baraza la nidhamu dhidi yake hasa kwenye masuala ya makubaliano ya kukiri kosa (plea bargaining) ambayo yana malalamiko mengi ya wananchi na kubambikia watu kesi mbalimbali wamchunguze mwenendo wake alipokuwa DPP na kama bado anazo sifa za kuteuliwa kuwa Jaji.

2. Tunapendekeza uanzishwe utaratibu wa wazi wa kuwapata Majaji kama vile kuwashindanisha kwa vigezo ikiwa ni pamoja na kufanya usaili wa wazi na sio kuteua watu moja kwa moja. Mfano mzuri ni namna ya upatikanaji Majaji nchini Kenya na nchi nyingine.

3. Tunashauri kusitishwa kwa mchakato wa kumuapisha kuwa Jaji aliyekuwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Biswalo Mganga hadi hapo malalamiko dhidi yake yatakapokamilika kuchunguzwa na yatakapoamuliwa na Baraza la Nidhamu (Tribunal) litakaloundwa ili kuchunguza malalamiko na tuhuma dhidi yake.

4. Kwa kuwa Katiba iliyopo Ibara ya 112 (1) wajumbe wa tume ya kuajiri ya mahakama, mawakili hawana uwakilishi.
Kwa hiyo tume ya sasa inatekeleza majukumu yake bila uwakilishi wa mawakili wa kujitegemea, uwakilishi wa kijinsia na sifa zinazoainishwa katika Katiba. Hivyo tunapendekeza uwekwe utaratibu wa kuhakikisha kuwa Tume inakuwa na uwakilishi sawia.

5. Tunapendekeza kuwa uwekwe utarataibu wazi wa kuwapata Majaji ikiwa ni pamoja na kuweka wazi uwepo wa nafasi za Ujaji kwa kutangaza ili watu wenye sifa waombe, washindanishwe kwa vigezo na masharti mbalimbali hii ingesaidia kupata Majaji wenye uwezo usiotiliwa shaka, Majaji huru na wasiopendelewa au wasiozua minong’ono ya kubebwa au wenye nasaba za kisiasa.

6.Katika utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Mahakama ,Bunge linajukumu la kutunga sheria itakayoweka masharti ya utekelezaji wa majukumu ya Tume.

Imetolewa Leo Jumapili Mei 16, 2021

John Mrema - Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje. View attachment 1787263

IMG-20210516-WA0001.jpg
 

Elli M

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
43,117
2,000
Wacha kabisa! Mama atatia pamba masikioni au atamla kichwa? Kwakifupi Mama angeanza na timu mpya tu ili kuziba mapengo, mashimo na mahandaki ya "Shujaa wa Africa"
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
24,389
2,000
Ni kama vile kila mteuliwa alikua busy kulazimisha kugewa pesa na raia.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,313
2,000
Principal State Attorney Joseph Pande ambaye sasa ni DDPP Naibu Mkurugezi Mkuu wa Mashtaka anauzoefu mkubwa ktk kesi za kisiasa enzi za mwendazake, hivyo katika awamu ya sita tutegemee atapitia mafaili yote yenye kesi zisizotakiwa kuwepo mahakamani kama alivyotamka Mh. Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rejea mifano ya kesi zilizowahi kushughulikiwa na ofisi ya DPP:
 

Big Eagle

JF-Expert Member
May 3, 2020
476
500
Changamoto kweli mama atashindwa kusimama kwenye kauli yake ya haki kama akifumbia macho mawazo ya wananchi.
 

Biggs

JF-Expert Member
May 3, 2014
685
1,000
To me this was one of the worst pick that should never have happened at all.
 

Bukali

JF-Expert Member
May 7, 2018
837
1,000
Sura yako tu inaonyesha unapambana na dhiki ya kutisha mkuu, dikteta alikunyoosha aswa.
Mkuu kwangu hakuna utawala ambao nishawahi jutia, hata atawale nani nitkulabata kama kawaida, maana malizangu hazitokani makandokando.

Pole kama uliumizwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom