Tamko la ACT-Wazalendo juu ya kusitishwa misaada ya MCC

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
620
1,543
TAARIFA KWA UMMA

TAMKO LA CHAMA CHA WAZALENDO JUU YA UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI WA MCC WA KUSITISHA MAHUSIANO NA TANZANIA YATAWAUMIZA WANANCHI WA VIJIJINI

. CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeupokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa wa MCC wa kusisitisha mahusiano na Tanzania.

.MCC ni Shirika la misaada la Marekani lilianzishwa na Bunge la Nchi hiyo mwaka 2004 kwa lengo la kusaidia miradi ya maendeleo katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa haraka wa uchumi.

Tangu kuanzishwa kwake, shirika hili limesaidia miradi mingi ya maendeleo nchini ikiwemo ujenzi wa barabarani na usambazaji wa umeme vijijini kwa sasa miradi ya aina hiyo inaendelea sehemu mbali mbali hapa nchini na miongoni mwao ni pamoja na mradi wa REA,miradi ya barabara kama ile ya Tunduma Sumbawanga pamoja na Tanga katika barabara ya Horohoro.

Pamoja na vigezo vingine, kigezo mama kwa nchi kufuzu kupata misaada ya MCC ni kwa nchi husika kuzingatia misingi kidemokrasia ikiwemo kufanya uchaguzi ulio huru na haki.

. Jana tarehe 28 Machi 2016 Shirika la MCC lilitangaza kusitisha mahusiano na Tanzania kutokana na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM),kubariki kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 Oktoba 205 na kubariki kurudiwa kwa uchaguzi huo tarehe 20 Machi 2016 katika mazingira ambayo hayakuzingatia misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuvunja matunda ya mwafaka wa kisiasa na kikatiba uliojengwa kwa gharama kubwa visiwani humo.

. Chama cha ACT-Wazalendo kinapigania nchi yetu kujitegemea kiuchumi kama msingi wa kujenga utu na uhuru endelevu wa kisiasa na kijamii. Hata hivyo tunatambua kwamba katika kipindi hiki nchi yetu inahitaji mahusiano mema na Jumuiya ya Kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani, likiwemo shirika la MCC, katika kuendeleza miradi ya maendeleo. Shirika la MCC limekuwa mdau mkubwa katika miradi ya barabara na kusambaza umeme vijini.

Uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCC utawaumiza na kukwaza juhudi za wananchi wa vijijini katika kujikwamua na umaskini.

Tunasikitika kwamba ubabe wa Serikali ya CCM na woga wake wa kushindana kidemokrasia umesababisha nchi yetu ikose pesa za MCC ambazo zingesukuma mbele juhudi za kupambana na umaskini.

Tunatoa wito tena kwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi kuacha ubabe na kufifisha juhudi za miaka ishirini za ujenzi wa demokrasia hapa nchini. Tunatoa wito maalumu kwa wadau wote wa siasa visiwani Zanzibar kurudi mezani na kutatua mgogoro wa kisiasa kwa njia za kistaraabu na katika hali ambayo itarudisha heshima ya nchi yetu katika kukuza demokrasia nchini.

Imetolewa na

Theopister Kumwenda
Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje
29/03/2016
 
Wewe unafanya kazi gani mkuu?

Kwani inakuhusu? Mimi kazi yangu unataka ya nini? Wewe fanya kazi kwa bidii huko unakofanya kazi, na mimi nitafanya kazi kwa bidii huku kazini kwangu. Kwa hiyo kila mtu afanye kazi kwa bidii,. Kama ni mwanajeshi afanye kazi kwa bidii, mwalimu naye afanye kazi kwa bidii, mkulima naye afanye kazi kwa bidii, mtu wa TISS afanye kazi kwa bidii, house girl naye afanye kazi kwa bidii, mkusanya kodi naye afanye kazi kwa bidii, na kadhalika na kadhalika. Lakini majambazi na mafisadi, hapana, za kwao siyo kazi halali.
 
mimi nadhani kuna jambo zito Marekani ameliona kuliko hata huo uchaguzi wa zanzibar,,,,kuna fursa ameona anazikosa...JPM endelea kukaza baba ikibidi tutakula hata nyasi....hakunaga msaada wa bure hata iyo barabara ya Namtumbo Songea waliiba sana madini yetu pande ile
 
TAARIFA KWA UMMA

TAMKO LA CHAMA CHA WAZALENDO JUU YA UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI WA MCC WA KUSITISHA MAHUSIANO NA TANZANIA YATAWAUMIZA WANANCHI WA VIJIJINI

. CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeupokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa wa MCC wa kusisitisha mahusiano na Tanzania.

.MCC ni Shirika la misaada la Marekani lilianzishwa na Bunge la Nchi hiyo mwaka 2004 kwa lengo la kusaidia miradi ya maendeleo katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa haraka wa uchumi.

Tangu kuanzishwa kwake, shirika hili limesaidia miradi mingi ya maendeleo nchini ikiwemo ujenzi wa barabarani na usambazaji wa umeme vijijini kwa sasa miradi ya aina hiyo inaendelea sehemu mbali mbali hapa nchini na miongoni mwao ni pamoja na mradi wa REA,miradi ya barabara kama ile ya Tunduma Sumbawanga pamoja na Tanga katika barabara ya Horohoro.

Pamoja na vigezo vingine, kigezo mama kwa nchi kufuzu kupata misaada ya MCC ni kwa nchi husika kuzingatia misingi kidemokrasia ikiwemo kufanya uchaguzi ulio huru na haki.

. Jana tarehe 28 Machi 2016 Shirika la MCC lilitangaza kusitisha mahusiano na Tanzania kutokana na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM),kubariki kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 Oktoba 205 na kubariki kurudiwa kwa uchaguzi huo tarehe 20 Machi 2016 katika mazingira ambayo hayakuzingatia misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuvunja matunda ya mwafaka wa kisiasa na kikatiba uliojengwa kwa gharama kubwa visiwani humo.

. Chama cha ACT-Wazalendo kinapigania nchi yetu kujitegemea kiuchumi kama msingi wa kujenga utu na uhuru endelevu wa kisiasa na kijamii. Hata hivyo tunatambua kwamba katika kipindi hiki nchi yetu inahitaji mahusiano mema na Jumuiya ya Kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani, likiwemo shirika la MCC, katika kuendeleza miradi ya maendeleo. Shirika la MCC limekuwa mdau mkubwa katika miradi ya barabara na kusambaza umeme vijini.

Uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCC utawaumiza na kukwaza juhudi za wananchi wa vijijini katika kujikwamua na umaskini.

Tunasikitika kwamba ubabe wa Serikali ya CCM na woga wake wa kushindana kidemokrasia umesababisha nchi yetu ikose pesa za MCC ambazo zingesukuma mbele juhudi za kupambana na umaskini.

Tunatoa wito tena kwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi kuacha ubabe na kufifisha juhudi za miaka ishirini za ujenzi wa demokrasia hapa nchini. Tunatoa wito maalumu kwa wadau wote wa siasa visiwani Zanzibar kurudi mezani na kutatua mgogoro wa kisiasa kwa njia za kistaraabu na katika hali ambayo itarudisha heshima ya nchi yetu katika kukuza demokrasia nchini.

Imetolewa na

Theopister Kumwenda
Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje
29/03/2016

uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 October 205 .....

unakimbilia wapi? take your time to proof read before you post
 
Kuna mgombea wao anaitwa Donald Trump. Simuelewagi sana na siasa zake za kibabe. Sijui hiyo ni demokrasia gani
 
Wasitake tukumbuke ubabe waliofanya kwa nchi za Iraq, Afghanistan, Libya, Syria, Iran nk. Sijui hiyo ni demokrasia gani wanayonadi duniani
 
Kwani inakuhusu? Mimi kazi yangu unataka ya nini? Wewe fanya kazi kwa bidii huko unakofanya kazi, na mimi nitafanya kazi kwa bidii huku kazini kwangu. Kwa hiyo kila mtu afanye kazi kwa bidii,. Kama ni mwanajeshi afanye kazi kwa bidii, mwalimu naye afanye kazi kwa bidii, mkulima naye afanye kazi kwa bidii, mtu wa TISS afanye kazi kwa bidii, house girl naye afanye kazi kwa bidii, mkusanya kodi naye afanye kazi kwa bidii, na kadhalika na kadhalika. Lakini majambazi na mafisadi, hapana, za kwao siyo kazi halali.
Umenena vema mkuu, upumbavu wa kuabudu wazungu ni lazima tufike mahali tuupuuze kabisa.
 
TAARIFA KWA UMMA

TAMKO LA CHAMA CHA WAZALENDO JUU YA UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI WA MCC WA KUSITISHA MAHUSIANO NA TANZANIA YATAWAUMIZA WANANCHI WA VIJIJINI

. CHAMA cha ACT-Wazalendo kimeupokea kwa masikitiko makubwa uamuzi wa Bodi ya Wakurugenzi wa wa MCC wa kusisitisha mahusiano na Tanzania.

.MCC ni Shirika la misaada la Marekani lilianzishwa na Bunge la Nchi hiyo mwaka 2004 kwa lengo la kusaidia miradi ya maendeleo katika nchi mbalimbali duniani kwa ajili ya kuchochea ukuaji wa haraka wa uchumi.

Tangu kuanzishwa kwake, shirika hili limesaidia miradi mingi ya maendeleo nchini ikiwemo ujenzi wa barabarani na usambazaji wa umeme vijijini kwa sasa miradi ya aina hiyo inaendelea sehemu mbali mbali hapa nchini na miongoni mwao ni pamoja na mradi wa REA,miradi ya barabara kama ile ya Tunduma Sumbawanga pamoja na Tanga katika barabara ya Horohoro.

Pamoja na vigezo vingine, kigezo mama kwa nchi kufuzu kupata misaada ya MCC ni kwa nchi husika kuzingatia misingi kidemokrasia ikiwemo kufanya uchaguzi ulio huru na haki.

. Jana tarehe 28 Machi 2016 Shirika la MCC lilitangaza kusitisha mahusiano na Tanzania kutokana na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM),kubariki kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika tarehe 25 Oktoba 205 na kubariki kurudiwa kwa uchaguzi huo tarehe 20 Machi 2016 katika mazingira ambayo hayakuzingatia misingi ya demokrasia ya vyama vingi na kuvunja matunda ya mwafaka wa kisiasa na kikatiba uliojengwa kwa gharama kubwa visiwani humo.

. Chama cha ACT-Wazalendo kinapigania nchi yetu kujitegemea kiuchumi kama msingi wa kujenga utu na uhuru endelevu wa kisiasa na kijamii. Hata hivyo tunatambua kwamba katika kipindi hiki nchi yetu inahitaji mahusiano mema na Jumuiya ya Kimataifa na wadau mbalimbali wa maendeleo duniani, likiwemo shirika la MCC, katika kuendeleza miradi ya maendeleo. Shirika la MCC limekuwa mdau mkubwa katika miradi ya barabara na kusambaza umeme vijini.

Uamuzi huu wa Bodi ya Wakurugenzi wa MCC utawaumiza na kukwaza juhudi za wananchi wa vijijini katika kujikwamua na umaskini.

Tunasikitika kwamba ubabe wa Serikali ya CCM na woga wake wa kushindana kidemokrasia umesababisha nchi yetu ikose pesa za MCC ambazo zingesukuma mbele juhudi za kupambana na umaskini.

Tunatoa wito tena kwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi kuacha ubabe na kufifisha juhudi za miaka ishirini za ujenzi wa demokrasia hapa nchini. Tunatoa wito maalumu kwa wadau wote wa siasa visiwani Zanzibar kurudi mezani na kutatua mgogoro wa kisiasa kwa njia za kistaraabu na katika hali ambayo itarudisha heshima ya nchi yetu katika kukuza demokrasia nchini.

Imetolewa na

Theopister Kumwenda
Makamu Mwenyekiti, Kamati ya Katiba, Sheria na Mambo ya Nje
29/03/2016
KAMA WAO WANACHAPA FEZA ZAO NA SISI TUCHAPE ZETU.
 
Back
Top Bottom