TAMKO: CUF wamjibu Spika wa Bunge, baada ya kusema hamtambui Maalim Seif

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,697
8,843
CUF wamjibu Spika wa Bunge, baada ya kusema hamtambui Seif




MAELEZO YA UFAFANUZI WA MASUALA MBALIMBALI YANAYOENDELEA NDANI YA CUF KWA WAANDISHI WA HABARI YALIYOTOLEWA LEO TAREHE 5 AGOSTI, 2017 KATIKA UKUMBI WA OFISI YA WABUNGE WA CUF-MAGOMENI, DAR ES SALAAM:

1. UTANGULIZI:

Ndugu Waandishi wa Habari, Awali hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia uhai na afya njema kuweza kukutana. Tuwashukuru kwa kazi kubwa mnayoendelea nayo ya kuuhabarisha umma wa watanzania ndani na nje ya mipaka ya Tanzania juu ya masuala mbalimbali yanayoendelea nchini hususani ndani ya Chama chetu cha CUF.

Kama tunavyofahamu kuwa Jana yamefanyika mazishi ya aliyekuwa Rais (Mwenyekiti wa Taifa) wa Chama TADEA ndugu John Lifa CHIPAKA. Kwa niaba ya Chama Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Taifa Mheshimiwa Julius MTATIRO ambaye yupo nchini Marekani kwa masomo ya Utawala katika Chuo kikuu nchini humo ametuma salaamu za Rambirambi kwa Chama cha TADEA, ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huu kwa namna moja au nyingine. “CUF imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha John Chipaka ambaye amekuwa ni mpambanaji wa kudai demokrasia na ni muasisi wa mageuzi nchini kabla na baada ya Uhuru wa Tanganyika.

Aliamini ktk utawala wa kidemokrasia kwa mfumo wa uwepo wa vyama vingi nchini, jambo lilompelekea kuonekana ni mtu mbaya kwa watawala na kuwekwa kizuizini kwa kosa la uhaini kwa miaka zaidi ya kumi na mbili chini ya utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere. Pamoja na misukosuko aliyopitia kipindi chote hicho hakuwahi kurudi nyuma na kubadilisha msimamo wake wa kudai uhuru wa fikra na hoja mbadala kwa maslahi ya Taifa. Mwaka 1992 John Chipaka pamoja na umri wake kuwa mkubwa naye alishiriki kuasisi tena mageuzi nchini kwa kuanzisha moja ya chama cha siasa kinachojulikana kwa jina la TADEA na yeye kuwa Rais wa chama hicho mpaka alipofariki.

Hakika marehemu Chipaka katika msimamo huo ameacha funzo kubwa kwa vijana na wazee wenzake kuwa na moyo wa mageuzi, na ujasiri wa kupambana kudai haki na uhuru”. Ameeleza Mheshimiwa Mtatiro. Mwenyezi Mungu amsamehe mapungufu yake na amuweke mahala pema peponi. Amiin!! 2.

KUHUSU KESI/MASHAURI YA CUF YALIYOPO MAHAKAMANI:

Kama tunavyofahamu mwaka jana mwezi wa Septemba 24, 2016 baada ya Lipumba kufanya uvamizi wa ofisi za chama pale Buguruni kinyume na sheria na taratibu baada ya Kujiuzulu kwa hiari yake na kuiacha ofisi hiyo takribani kwa kipindi cha mwaka mzima. Chama cha CUF kupitia maamuzi ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa iliagiza Kamati ya Utendaji ya Taifa kusimamia suala hilo kwa kulifikisha mbele ya vyombo vya sheria-Mahakama ili kulipatia ufumbuzi.

Ni kwa msingi huo kuliendelea kujitokeza kwa ukiukwaji wa mambo mbalimbali na athari za uvamizi huo na mpaka sasa kuna Mashauri 6 ya Msingi yaliyopo Mahakamani Pamoja na mashauri madogo mengine ambayo sijayataja katika orodha hii kama ifuatavyo;

a) Kuna shauri la msingi (Civil Application/Cause) namba 23/2016 hili linahusu kuhoji uhalali wa maamuzi ya Msajiri wa Vyama vya siasa nchini Jaji Franscis Mutungi kumrejesha Lipumba katika Uenyekiti kinyume na Katiba ya CUF na maamuzi ya Mkutano Mkuu wa Taifa. Lipo mbele ya Jaji Kihiyo na limepangwa kutajwa Tarehe 7/9/2017.

b) Kuna shauri la msingi la madai (Civil Application no. 21/2017) kuhusu wizi wa Ruzuku na shauri dogo (Miscellaneous Civil Application No.28/2017) hili linahusu kuhusu kuweka Zuio [Injuction] kutolewa Ruzuku ya Chama kutokana na wizi wa shilingi 369 zilizoibwa na Lipumba na kundi lake wakishirikiana na Msajili Jaji FRANCIS Mutungi. Limepangwa kutolewa maamuzi ya Pingamizi Tarehe 11 Agosti, 2017 Lipo Mbele ya Mheshimiwa Jaji Wilfred Ndyansobera.

c) Kuna Shauri La Madai Namba 13/2017 Lililofunguliwa Na Ally Salehe dhidi ya RITA, Lipumba na wenzake kuhusu uhalali wa Bodi FEKI ya Wadhamini ya CUF iliyosajiliwa na RITA. Na shauri dogo namba 51/2017 linaloomba kuwepo kwa zuio (Injuction) ya kuizuia bodi hiyo kufanya kazi mpaka shauri la msingi litakaposikilizwa na kufanyiwa maamuzi. Limepangwa kutajwa na au kusikilizwa tarehe 11 Agosti, 2017. Nalo lipo mbele ya Mheshimiwa Jaji Ndyansobera.

d) Kuna shauri la Jinai namba 50/2017 kuhusu Lipumba na wenzake, Emmy Hudson -RITA, Jaji FRANCIS Mutungi kughushi nyaraka na kutaka kuingilia mwenendo wa mashauri yaliyopo Mahakama (CONTEMPT OF COURT PROCEEDINGS)

e) Kuna shauri la msingi (Election Petition) namba 1/2017 linalohusiana na uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la Afrika Mashariki katika Mahakama kuu ya Dodoma kati ya Twaha Taslima, Abdallah Mtolea, Katani Ahmed katani dhidi ya Bunge kwa kukiuka utaratibu na kanuni za uchaguzi huo uliompa Mohamed Habibu Mnyaa uwakilishi wa CUF hali si mwanachama.

f) SHAURI LA MSINGI (CIVIL CASE NO.143/2017) Juu ya Wabunge 8 wa CUF na Madiwani 2 kupinga kuvuliwa uanachama na Lipumba lakini pia kuna maombi madogo (Miscelleneous Civil Application No. 447/2017) ambayo inahusiana na kuomba Zuio la muda (Temporary Injuction Order and To maintain Status Quo)

UFAFANUZI WA KILICHOTOKEA NA MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU:

Shauri la msingi (CIVIL CASE NO. 143/2017) Limepangwa kusikilizwa/kutajwa Tarehe 31/8/2017 shauri hili lililofunguliwa na wabunge wetu 8 na Maadiwani wawili wa manispaa za ubungo na Temeke ambao ni

1. MIZA BAKARI HAJI

2. SAVERINA SILVANUS MWIJAGE [MBUNGE]

3. SALMA MOHAMED MWASA [MBUNGE]

4. RAISA ABDALLAH MUSSA [MBUNGE]

5. RIZIKI SHAHRI NG’WARI [MBUNGE]

6. HADIJA SALUM ALLY AL QASSIM [MBUNGE]

7. HALIMA ALI MOHAMED [MBUNGE]

8. SAUMU HERI SAKALA [MBUNGE]

9. ELIZABETH ALATANGA MAGWAJA- DIWANI VITI MAALUMU MANISPAA YA TEMEKE.

10. LAYLA HUSSEIN MADIBI- DIWANI VITI MAALUM-MANISPAA YA UBUNGO.

DHIDI YA;

1) BODI YA WADHAMINI -CUF,

2) MWENYEKITI WA CHAMA TAIFA,

3) KAIMU KATIBU MKUU-CUF,

4) MKURUGENZI TUME-NEC,

5) KATIBU WA BUNGE,

6) MKURUGENZI MANISPAA- TEMEKE

7) MKURUGENZI MANISPAA -UBUNGO

8) RUKIA AHMED KASSIM,

9) SHAMALA AZIZ MTAMBA,

10) KIZA HUSSEIN MAYEYE,

11) ZAINAB MNDOLWA AMIR,

12) HINDU HAMIS MWENDA,

13) SONIA JUMAA MAGOGO,

14) ALFREDINA APOLINARY KAHIGI,

15) NURU AWADH BAFADHILI

Wabunge na Madiwani Wetu wanadai haki ya uanachama wao kwa kuhoji mchakato uliotumika kufikia maamuzi hayo ambao haukufuata katiba ya CUF na huku kukiwa na mashauri ya msingi yanayoendelea mahakamani yanayohoji uhalali wa Uongozi juu ya ‘Mgogoro uliopandikizwa na Vyombo vya dola kwa kumtumia Msajili wa Vyama vya siasa unaoendelea.

Wanahoji juu ya uhalali wa vyombo vilivyochukua hatua hizo za nidhamu dhidi yao kama zimefuata taratibu ikiwa ni pamoja na kuwapatia taarifa za tuhuma zao kwa maandishi ili waweze kujiandaa kwa utetezi, siku na tarehe ya kikao hicho ukizingatia kuwa si wote wanaoishi hapa Dar es Salaam, uharaka wa Bunge na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuchukua hatua bila kujiridhisha na alau kiubinaadamu Bunge ikiwa ni wajumbe wake kuwauliza na kujua kutoka kwako hicho kilichojitokeza, kwa ujumla hawakupewa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea, maamuzi hayakuzingatia haki za kikatiba ikiwemo kukata Rufaa ndani ya siku 14 Ibara ya 108(5) ya katiba ya CUF, Wabunge wamekatia Rufaa maamuzi hayo na kumuandikia barua na kukiomba Chama kupitia Katibu Mkuu kiweze kuitisha Mkutano Mkuu wa Taifa ili kufikisha rufaa yao.

Mkutano Mkuu ndio wenye mamlaka na maamuzi ya mwisho juu ya masuala yote ndani ya Chama. Hilo lilifanywa na Lipumba na wenzake pale Baraza Kuu la uongozi taifa lilipowachukulia hatua za kinidhamu kwa kuwasimamisha uanachama Tarehe 28 Agosti, 2017. Hayana mengine ndiyo yanayohojiwa Mahakamani katika shauri hili la msingi.

3. KUHUSU SHAURI DOGO LA MADAI [MISCELLENEOUS CIVIL CASE NO. 447/2017] WABUNGE [8] NA MADIWANI [2] WA CUF DHIDI YA walalamikiwa walewale 15 tajwa hapo juu.

Maombi hayo yanahusu kuiomba Mahakama Kuu itoe zuio la muda [Temporary Injuction Order and to maintain Status Quo- HII MAANA YAKE NI KUSIMAMISHA MAAMUZI YA BUNGE NA TUME NA KUWAREJESHA WABUNGE WALIODAIWA KUVULIWA UANACHAMA WAENDELEE NA SHUGHULI ZA BUNGE NA KUWAWAKILISHI HALALI] katika kipindi hiki mpaka hapo shauri la msingi litakapoamuriwa. Kabla maombi hayo hayajasikilizwa Walalamikiwa (Respondent's No.1,2,3,4,5,8-15) waliweka Pingamizi la Awali ( Preliminary Objections) juu ya shauri hilo kwa madai ya kukosa sifa za kisheria (incompetence enacted provisions of law) na hoja hizo 4 za pingamizi zilizosikilizwa takribani kwa masaa 4 Tarehe hiyo 2/8/2017 pale shauri hilo lilipoitwa kwa kusikilizwa na baadae kupangwa kutolewa maamuzi ya Pingamizi hilo jana Tarehe 4/8/2017.

4. MAAMUZI JUU YA PINAMIZI LA AWALI YALIYOTOLEWA NA MAHAKAMA KUU;

Katika kupitia hoja zilizowasiilishwa Mahakamani hapo katika pingamizi hilo la awali (Preliminary Objection) lililowekwa na walalamikiwa Mahakama Kuu imekubaliana na hoja za waweka pingamizi kuwa kifungu cha sheria kilichotumika kufungulia shauri hilo mahakamani sio sahihi na hivyo kuliondoa shauri hilo kwa maana ya ‘STRUCK OUT” Unapozungumzia pingamizi unazungumzia hoja za kisheria pekee (pure points of law) kati ya hoja 4 zilizowasilishwa hoja 3 zimekataliwa na moja kukubaliwa iliyohusiana na matumizi ya sheria za uingereza (Common Law) section 2(3) ya JALA kifungu ambacho kwa mtazamo/maoni ya Jaji hakiipi mamlaka ya kisheria Mahakama kusikiliza maombi hayo. Nini maana ya maamuzi hayo na tafsiri ya kisheria juu ya neno “Struck out na Dismissal”

LEGAL DEFINITION :

"Difference between DISMISSAL and STRIKE OUT. When a case is dismissed, there is no right to reinstate it in the future. This is the legal way to say the case is closed and it cannot be re-opened. When a case is struck out, it may be re-opened.

TAFSIRI YA KISHERIA:

“Tofauti kati ya kufuta na kuondoa (shauri) ni kwamba kesi ikifutwa, hakutakuwa na haki ya kuirejesha tena (kurudisha/kuifungua upya) hapo baadae. Hii ni njia ya kisheria kusema kuwa kesi imefikia mwisho na huwezi kuifungua upya. Pale kesi inapoondoshwa, inaweza kufunguliwa upya.” Pingamizi juu ya maombi ya Shauri namba 447/2017 yameondolewa mbele ya Mahakama na wala hakuna hiko kitu kinachoitwa ‘kesi imefutwa, au kutupiliwa mbali au mahakama imeruhusu Wabunge wapya kuapishwa, KWA HAKIKA HAKUNA USHINDI WA MAAMUZI YALIYOTOLEWA’ kama inavyoripotiwa.

Shauri limeondolewa kwa kumaanisha kama vile hakukuwa na kitu kilichopaswa kujadiliwa na Mahakama juu ya maombi hayo. Pingamizi la awali [Preliminary Objection] na Maombi ya Zuio [injuction/Stop Order] ni vitu viwili tofauti kisheria. Wabunge wa CUF wameomba Zuio. Lipumba na wenzake wameweka Pingamizi. Huo ndio usahihi wa maelezo ya nini kilichojitokeza katika maamuzi ya Mahakama Kuu jana.

5. MATOKEO YA MAAMUZI YA MAHAKAMA KUU;

Maamuzi hayo yametupa fursa ya kuandaa vizuri zaidi nyaraka hizo na tayari tumepata faida ya kujua hoja wanazosimamia walalamikiwa (Respondents). Wabunge wetu wameweza ndani ya masaa 2 baada ya maamuzi tayari nyaraka zilitayarishwa, kusainiwa pamoja na marekebisho yote ya msingi na ya lazima yaliyopaswa kuingizwa ikiwemo kuwajumuisha katika shauri hilo Wakurugenzi wa Manispaa za Ubungo na Temeke ambao wanahusika kutokana na Madiwani waliopo katika halmashauri zao kuathiriwa na maamuzi ya Lipumba na genge lake. Ni matarajio yetu kuwa Jumatatu ya tarehe 7/8/2017 tutapata mrejesho wa kujua Mahakama Kuu imelipanga lini kulisikiza shauri hilo kutokana na kuingizwa kwa hati ya dharura/haraka (Under Certificate of Urgency).

6. WITO KWA WAAANDISHI WA HABARI, WANACHAMA NA WATANZANIA KWA UJUMLA: KESI ni MCHAKATO siyo TUKIO.

Utaratibu wa kisheria una njia na namna kadhaa za kupitia ili kuifikia haki inayopiganiwa. Tunawaomba waandishi wa habari kuripoti habari za kimahakama kwa uashihi na kutumia weledi ili kuepusha taharuki na kuwachanganya wananchi na wadau mbalimbali wa habari. Tusitoe taarifa kwa kutumia ‘mizuka’ mkanganyiko uliojitokeza jana na leo katika vyombo vya habari haukujenga weledi na afya njema kwa kuwahabarisha wananchi ndivyo sivyo.

Tunatoa wito kwa wanachama wa CUF, Wapenzi na Watanzania kwa ujumla kupuuza habari za upotoshaji na propaganda zinazoendelea kufanyika kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari. Si shauri la msingi wala maombi ya zuio lililosikilizwa na Mahakama Kuu na kuyatolea maamuzi. Kilichotolewa maamuzi ni Pingamizi juu ya hoja za za kisheria pekee ambazo zimesharekebishwa na kurejesha upya shauri hilo mahakamani.

Tuendelee kuwa watulivu na kwamba viongozi wenu ngazi ya Taifa wapo makini kulisimamia suala hili na kuhakikisha kuwa haki inapatikana. Tuna imani kubwa na Mahakama kuwa ni chombo cha kusimamia haki si Chombo cha kuchezewa.

Maamuzi ya Mahakama Kuu juu ya pingamizi tumeyapokea, ni sahihi kwa mujibu maoni ya Jaji kwa mujibu wa sheria na wala SI HUJUMA DHIDI YA HAKI kama inavyotaka kuaminishwa na baadhi ya wasiojua taratibu na misingi ya kisheria. Hakuna maamuzi yoyote mpaka sasa yaliyotolewa na Mahakama Kuu katika kadhia hii inayoendelea zaidi ya Kuzuia Ruzuku isitolewe kwa Lipumba na genge lake na hili la kuondoa maombi madogo yaliyowasilishwa.

Tutaendelea kukilinda na kukitetea Chama chetu cha CUF kwa nguvu zetu zote na kukiimarisha zaidi ilii kiendelee kutekeleza wajibu wake katika uendeshaji wa siasa za kistaarabu, na kwa njia za amani na zinazofuata Katiba ya CUF, Katiba ya JAMHURI ya Muungano wa Tanzania na Sheria nyingine za nchi yetu.

CUF NI TAASISI IMARA, YENYE VIONGOZI MAKINI.

HAKI SAWA KWA WOTE
 
Ila kafu walikosea kuchelewa kuchagua mwenyekiti wao ,,wangeiga wenzao chadema walivyowahi kuziba nafasi ya slaha haya yasingetokea
 
Hivi zile sayansi za asili za Zanzibar zimeisha? Kama zingalikuwepo kama tulivyokuwa tunasimuliwa, mpaka sasa kuna watu wangeshapewa vibusha! Yaani wooote wanaowasema au kuifanya vibaya kafu wangekuwa na miondoko ya kutanua miguu na kutochomekea visuruali vyao.
Watu wa Zanzibar hususan Pemba waliwaogopesha sana watu, lakini mwee wamekuwa weupeeeee kama karatasi ya fotokopi. Yaani chogo bado wanawasumbua! Haiwezekani, au wamekosea mizimu?
 
TISS ya Bongo ni aibu tupu !!

Sent using Jamii Forums mobile app

Kama kweli TISS inahusika, kama mkurugenzi wa sasa wa TISS alikuwa naibu mkurugenzi wa NIDA, kwa nini hao wakuu wa taasisi kama NEC, RITA, Bunge na Polisi wasiwe watu wa TISS? Halafu kwa nini mpaka leo hakuna Jaji Mkuu, yupo anaye kaimu tu? Je, yawezekana wanasubiri muda kidogo ili kupata Jaji Mkuu ambaye atakuwa mtu wa TISS? Kuna uwezekano kuwa kuna majaji ambao ni watu wa TISS ambao waliteuliwa muda wa hivi karibuni lakini kuwapatia hiyo nafasi sio rahisi kwa sasa.

Halafu kama kweli ni TISS, mbona wanacheza chess kama vile wamelewa?
 
Ila kafu walikosea kuchelewa kuchagua mwenyekiti wao ,,wangeiga wenzao chadema walivyowahi kuziba nafasi ya slaha haya yasingetokea
Maalim seif anaujua mchezo wooote ila anawageuza wenzie wapumbavu sina imani na maalim seif kabisaaa nadha naye ni mwanachama mtiifu wa chama cha makinikia ila ni kwa umakini mkubwa sana tena sana na ndio maana hata vikao vya usuluhishi alikuwa anataka aende peke yake, huyi maalim ana wauza CUF hakika,
 
Ila kafu walikosea kuchelewa kuchagua mwenyekiti wao ,,wangeiga wenzao chadema walivyowahi kuziba nafasi ya slaha haya yasingetokea

Huna kumbukumbu Wewe!

Chadema waliitisha Kikao cha kuziba nafasi ya Dkt Slaa baada ya kuona kwa jirani kuna fuka moshi!, mpaka tetesi zikaanza kuwa na Dkt Slaa nae anarudi kutengua Barua yake ya kujiuzulu
 
Kama kweli TISS inahusika, kama mkurugenzi wa sasa wa TISS alikuwa naibu mkurugenzi wa NIDA, kwa nini hao wakuu wa taasisi kama NEC, RITA, Bunge na Polisi wasiwe watu wa TISS? Halafu kwa nini mpaka leo hakuna Jaji Mkuu, yupo anaye kaimu tu? Je, yawezekana wanasubiri muda kidogo ili kupata Jaji Mkuu ambaye atakuwa mtu wa TISS? Kuna uwezekano kuwa kuna majaji ambao ni watu wa TISS ambao waliteuliwa muda wa hivi karibuni lakini kuwapatia hiyo nafasi sio rahisi kwa sasa.

Halafu kama kweli ni TISS, mbona wanacheza chess kama vile wamelewa?

Hivi TISS ndio waliwapumbaza CUF Wakawa bize kuzurura Ulaya baada ya Uchaguzi Mkuu badala ya kuziba nafasi ya Lipumba? Sio kila ujinga na uzembe wa Wanasiasa wa Upinzani ibebeshwe TISS
 
Ila kafu walikosea kuchelewa kuchagua mwenyekiti wao ,,wangeiga wenzao chadema walivyowahi kuziba nafasi ya slaha haya yasingetokea
maamuzi tayari waliishafanya walimkaimisha ndg Twaha twasilima na alitambuliwa na huyo msajiri
 
Back
Top Bottom