Tamba na Jicho πŸ‘ la Ustawi wa Jamii Mtaa kwa Mtaa πŸ‡ΉπŸ‡Ώ

Dkt. Gwajima D

Minister
Joined
Nov 28, 2015
Posts
1,706
Reaction score
8,657
Wasalaam

Leo 24 Julai, 2025 asubuhi, nakiri kupokea taarifa kadhaa kutoka kwa Wananchi wa Kata ya Baraa, Mtaa wa Kibao cha Njano kwa Mrefu, Arusha.

Kwamba, mtu mmoja mzima analea binti wa umri kati ya miaka 8 hadi 10 hivi ambapo yaani ni anampa vipigo tu apendavyo yeye hivyo, mtoto amejaa makovu ya vipigo kila sehemu, ananyimwa chakula, anafungiwa mlango alale nje na mateso mengine aina hiyo hadi shuleni, maendeleo yanasua sua.

KILICHOFUATA: niliwasiliana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo, maafisa ustawi wa jamii mara moja walielekea eneo la tukio na kumfikia mtoto. Hii ni kuonesha kuwa, ustawi wa jamii wako speed... wewe tu toa ushirikiano.

Watuhumiwa wataijibu sheria ya mtoto na vifungu vyake.

UJUMBE GANI KWA JAMII: tuache kutesa watoto, jicho la ustawi wa jamii linatamba alipo mwanajamii yeyote kwa ushirikiano na wananchi wenye mapenzi mema.

Hima, tuendelee kutamba na jicho la ustawi wa jamii πŸ‘πŸ‡Ή kuwadaka watu katili wa watoto popote/kokote πŸ‡ΉπŸ‡ΏβœοΈ

Pia, kumbuka kupiga 116 kituo cha taarifa za watoto. Vilevile, kuna namba za maafisa binafsi na za vituo vya huduma kwa wananchi hapa chiniπŸ‘‡zikumbuke, mpe na mwingine.....
 

Attachments

  • IMG-20250724-WA0058.jpg
    249.3 KB · Views: 19
  • IMG-20250708-WA0027(5).jpg
    186.1 KB · Views: 17
  • IMG-20250708-WA0028(6).jpg
    151.2 KB · Views: 22
  • IMG-20250510-WA0045(23).jpg
    115.6 KB · Views: 19
Muheshimiwa hizi namba za bure zipo active kweli?
 
Sasa mhe. waziri mbona unatoa taarifa za huyo binti wa miaka 8 kabla ya mtuhumiwa kukamatwa. Je akiwa ni mwana JF akabahatika kuiona hii taarifa hapa, na kuamu kutoroka, hapo utakuwa umetengeneza au umeharibu?
 
Wengine tunatafuta hizi nafasi za kukaa na watoto, wengine wanazipata halafu wanazichezea. Hongera sana mheshimiwa kwa hatua za haraka ulizochukua, naamini utatupa mrejesho wa kilichobainika eneo la tukio.
 
Upewe Wizara zote uongoze. Hawa wengine kazi kusifu na kulamba viatu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…