LoyalTzCitizen
JF-Expert Member
- Sep 15, 2010
- 2,234
- 883
Mkuu El Toro,
Jesca Ongalla si mtoto wa kuzaa wa Remmy Onglalla (RIP). Wakati wanakutana, mama alishakuwa na mtoto wa kwanza. Baadaye ndiyo akazaliwa Kalimanguza (KALI) Ongalla. Kali ni mtoto wa pili kwa mama na mtoto wa kwanza wa Marehemu (inawezekana). Ila ninavyofahamu ni kuwa Remmy alikuwa kamchukua na kumlea kama mtoto wake wa kuzaa na Jesca akawa anatumia jina lake.
Wiki jana nimepoteza Rafiki na Ex-room Mate shuleni Mazengo, Herman Emanuel Nzowa na mwanamuziki kipenzi Dr. Remmy Ongalla. Nzowa tulikuwa wote wapenzi wakubwa sana wa muziki. Nakumbuka furaha aliyokuwa nayo baada ya kuona Live Concert ya Sikinde pale Dodoma. Wimbo ambao ulimfurahisha sana ulikuwa ule Hassan Bichuka anaimba "kama hajasikia, ehh x2 Ajali niliyoipata nimekuwa kilema. Na kilema isiwe ni kisingizio cha kuacha kuja kuniona.......". Hii imekuja baada ya kusoma humu kama utani vile kuwa Remmy Ongalla amefariki.
Nakumbuka ile story ambayo Remmy alienda Mwanza na kukataa kurudi Dar. Akawa anaongeza concert moja baada ya nyingine. Mamaa akaona huyu jamaa hataki kurudi? Ngoja aone kasheshe. Mamaa akaenda kwenye kipindi maarufu sana enzi hizo kiitwacho MAMBO MPWITA MPWITA na akaweka tangazo. Tangazo likaja kusomwa "Ramadhani Mtoro Ongalla unatakiwa urudi haraka sana nyumbani, watoto wanaumwa surua..." Akawa kila akikanyaga sehemu, watu wanamkimbilia kwa maneno "...Dr Remmy, rudi nyumbani haraka maana wamesema kuwa watoto wanaumwa surua..." Kumbuka enzi hizo hakuna Mobile phone na simu za Posta ni za shida sana.
Naona hatimaye umerudi NYUMBANI for goor.
Rip NZOWA, RIP Ongalla.
Rip your mate, Rip Dokta!, kumbe na wewe ni mzee wa Camp sio! tupo pamoja mana! Big up Mazengo!