TAMATI...safari ya mwisho ya Dakta ndio hiyoooo

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,303
4,684
Umati ni mkubwa uliohudhuria shughuli za kumpa heshima za mwisho mwanamuziki maarufu hapa nchini Hayati Ramadhani Mtoro maarufu kama Dakta Remmy.

Ni majonzi, vilio na simanzi vilitawala mahali hapa lakini pia faraja toka kwa watu mbalimbali zimekuwa zikiwafikia watu woote walioonekana kuwa na maumivu moyoni...

''kazi yake mola haina makosa''

''bwana ametoa na bwana ametoa so msilie''

''cha msingi ni kumuombea ili akapate kupumzika kwa amani''

Hayo ni baadhi ya maneno yaliyosikika kuwafariji wafiwa.
Hakika ni hudhuni kila kona ya mahali hapa...
 
''aamualo mola wala hawezi kosea
Narudi udongoni nilipotokea
Kwa nguvu za mwenyezi ntapotea usingizini
Nikiwakosa basi yarabi yu kazini
Uhai bado nautamani, ila sipaswi kubaki duniani
Safari ya ahera ishafika
Kwaherini masela ndugu na jamaa
Mja rudi kwa mola wako kama umepote
Kumbuka ahera ndiko unakoelekea
Anza kutenda mema kabla kifo hakijakukuta
Ukipuuza haya we utakuja kujuta...
 
safari yangu sasa imeshawadia
Kurudi kwa Baba yanipasa naaga Dunia
Mwili umenyong'onyea viungo vimelegea
Fahamu nshapoteza nimezingilwa na Giza
Milango ya fahamu ishafungwa, kamanda naokoteza uhai nalamba mchanga....
 
naukumbuka wimbo wake wa muziki nini!!
Muziki kilio, muziko maombolezo, muziki fundisho,
jamani watu wote hufa ila kuna watu jamaniiiii
God bless his soul, wafarijike ndugu zake na jamaa zake, Remmy ameacha legacy.
Apumzike kwa amani Amina.
 
Umati ni mkubwa uliohudhuria shughuli za kumpa heshima za mwisho mwanamuziki maarufu hapa nchini Hayati Ramadhani Mtoro maarufu kama Dakta Remmy.

Ni majonzi, vilio na simanzi vilitawala mahali hapa lakini pia faraja toka kwa watu mbalimbali zimekuwa zikiwafikia watu woote walioonekana kuwa na maumivu moyoni...

''kazi yake mola haina makosa''

''bwana ametoa na bwana ametoa so msilie''

''cha msingi ni kumuombea ili akapate kupumzika kwa amani''

Hayo ni baadhi ya maneno yaliyosikika kuwafariji wafiwa.
Hakika ni hudhuni kila kona ya mahali hapa...

R.I.P Remmy

Btw huu Dr wake ni kama wa Slaa au wa JK?
 
Baadhi ya umati wa waombolezaji waliojitokeza katika ibada ya kuaga mwili wa marehemu Dk.Remmy Ongala katika viwanjavya Biafra leo mchana jijini Dar es Salaam.

Mke wa Marehemu Dk. Remmy akiuaga mwili wa mmewa huku akisaidiwa na watoto wake Kally Ongala na mwenzake.

Watoto na wajukuu wa DK Remmy wakiuaga mwili wa ndugu yao leo/

Mtoto wa kwanza wa marehemu DK.Remmy Ongala Kally Mangonga ambaye ni mchezaji wa timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam akiwa na dada yake Jesca wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa baba yao katika viwanja vya Biafra .
 
Dah
 
its all over now.
Dakta ulitoka kwa udongo umerudi kwa udongo.
Pumzika kwa amani Baba
 
Naam kamanda. Ukumbusho na kuukubali ukweli ni Safari ya sote hiyo.
Rest in Peace Dr.Remmy, Ramadhan Mtoro Ongala!
 
RIP Dr. Remmy. Hakuna maneno yanayoweza kuelezea huzuni yetu. Kwa kuwa hayo ni maamuzi ya Mola, hatuna budi kuyapokea. Kazi yako itakumbukwa daima. Pumzika kwa amani. Amen.
 
Thursday, December 16, 2010
BURIANI DOKTA REMMY ONGALA
Mzee Makassy, Mjomba wa marehemu
Dk Remmy Ongala akiwa msibani

Mjane na watoto wa marehemu Dk Remmy Ongala
ambaye alijaaliwa watoto sita

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi, akitoa rambirambi za Serikali wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Dk Remmy Ongala aliyefariki majuzi na kuzikwa leo kwenye makaburi ya Sinza jijini Dar. Shughuli ya kutoa heshima za mwisho ilifanyika uwanja wa Biafra, Kinondoni
Dk. Emmanuel Nchimbi akiongoza umati wa waombolezaji kutoa heshima za mwisho kwa Dk. Remmy Ongala uwanja wa Biafra Kinondoni leo. Kulia ni mtoto mkubwa wa Dk. Remmy, Kalimangonga Ongala ambaye ni mwanasoka nyota.
Mbunge wa Ubungo, Mh. John Mnyika na Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan wakititoa heshima zao za mwisho kwa Dk. Remmy Ongala
Mshirika wa karibu wa siku nyingi wa Dk. Remmy Ongala, Cosmas Thobias Chidumule, akiwa na uchungu wakati wa heshima za mwisho kwa besti wake waliefanya kazi kwa miaka mingi kabla ya wote kuokoka na kuanza kumwimbia Mungu
Toni, Mjane wa Dk. Remmy Ongala, akiwa ameghubikwa na huzuni
Mzee Jangala na wadau wengine kibao walijitokeza kumuaga Dk. Remmy Ongala
Umati mkubwa ulikuja kumuaga Dk Remmy Ongala kiasi hata ikabidi polisi waitwe kuweka mambo sawa
Jeneza lenye mwili wa marehemu Dk Remmy ambaye jina lake kamili ni Ramazani Mtoro Mungamba Ongala
mdau wa Radio Kilimanjaro ya Sweden
naye yupo kurekodi tukio hili

Wake kwa waume, vijana kwa wazee
walijitokeza kwa Dk REmmy Ongala

Cosmas Thobias Chidumule akiongea
kwa niaba ya wanamuziki wote

Toka shoto ni wakongwe Mzee Makassy, Tchimanga Kalala Assosa (wa tatu waliosimama) akifuatiwa na King Kikii, Kanku Kelly na Abou Semhando
Mmoja wa viongozi wa kamati ya Mazishi
John Kitime akiandaa kitabu cha maombolezi

Familia ya Dk. Remmy Ongala

Malkia wa Mipasho Khadija Omar Kopa
na wadau wengine wakiwa na huzuni

Waombolezaji wakiwa katika majonzi
Umoja wa kwaya ukimlilia Dk Remmy
kwa wimbo maalumu waliomtungiaPicha kutoka kwa Michuzi Blog: MICHUZI
 
Mtoto wa kwanza wa marehemu DK.Remmy Ongala Kally Mangonga ambaye ni mchezaji wa timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam akiwa na dada yake Jesca wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa baba yao katika viwanja vya Biafra .

Mkuu El Toro,
Jesca Ongalla si mtoto wa kuzaa wa Remmy Onglalla (RIP). Wakati wanakutana, mama alishakuwa na mtoto wa kwanza. Baadaye ndiyo akazaliwa Kalimanguza (KALI) Ongalla. Kali ni mtoto wa pili kwa mama na mtoto wa kwanza wa Marehemu (inawezekana). Ila ninavyofahamu ni kuwa Remmy alikuwa kamchukua na kumlea kama mtoto wake wa kuzaa na Jesca akawa anatumia jina lake.

Wiki jana nimepoteza Rafiki na Ex-room Mate shuleni Mazengo, Herman Emanuel Nzowa na mwanamuziki kipenzi Dr. Remmy Ongalla. Nzowa tulikuwa wote wapenzi wakubwa sana wa muziki. Nakumbuka furaha aliyokuwa nayo baada ya kuona Live Concert ya Sikinde pale Dodoma. Wimbo ambao ulimfurahisha sana ulikuwa ule Hassan Bichuka anaimba "kama hajasikia, ehh x2 Ajali niliyoipata nimekuwa kilema. Na kilema isiwe ni kisingizio cha kuacha kuja kuniona.......". Hii imekuja baada ya kusoma humu kama utani vile kuwa Remmy Ongalla amefariki.

Nakumbuka ile story ambayo Remmy alienda Mwanza na kukataa kurudi Dar. Akawa anaongeza concert moja baada ya nyingine. Mamaa akaona huyu jamaa hataki kurudi? Ngoja aone kasheshe. Mamaa akaenda kwenye kipindi maarufu sana enzi hizo kiitwacho MAMBO MPWITA MPWITA na akaweka tangazo. Tangazo likaja kusomwa "Ramadhani Mtoro Ongalla unatakiwa urudi haraka sana nyumbani, watoto wanaumwa surua..." Akawa kila akikanyaga sehemu, watu wanamkimbilia kwa maneno "...Dr Remmy, rudi nyumbani haraka maana wamesema kuwa watoto wanaumwa surua..." Kumbuka enzi hizo hakuna Mobile phone na simu za Posta ni za shida sana.

Naona hatimaye umerudi NYUMBANI for goor.

Rip NZOWA, RIP Ongalla.
 
Back
Top Bottom