Tamasha la Alex Msama pale Leaders Club si Tamasha la Pasaka , ni Tamasha la kisiasa

Lkn si Kuna tamasha lingine ambalo lilikuwa limeandaliwa kbl ya Tamasha la akina Msama? Tamasha la Christina Shusho ,Rose Mhando na wengine litakuwepo Mlimani City na litaonyweshwa na Wasafi Tv, hivyo wale ambao hawatapenda kwenda la Msama nendeni Hilo.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
Tutapinga uzandiki hadi mwisho
 
Alex Msama anatangaza kila mahali nchini Tanzania kwamba anaanda Tamasha la Pasaka , ambapo inadaiwa Wasanii mbalimbali wa nyimbo za injili watatumbuiza , Hakuishia hapo ameendelea kudai kwamba Mtume na Nabii Boniface Mwamposa atatoa neno .

Kilichonishangaza ni Maelezo kwamba , pamoja na kwamba ni Tamasha la Pasaka lakini pia ni sherehe ya miaka miwili ya Urais wa Samia Suluhu Hassan , na kwamba Mgeni Rasmi wa Tamasha hilo ni Nape Nnauye , ambaye ni Waziri wa Habari

Labda kwa kumbukumbu hasa kwa wale ambao hawamfahamu Alex Msama , ni hivi , huyu Alex Msama ni Kada mtiifu wa ccm anayejificha kwenye matamasha ya Injili , ambapo amekuwa akitumia Taasisi inayoitwa Msama Promotion , aliwahi kuendesha vipindi vya kwaya za Jumapili Clouds FM , huku lengo lake kuu likiwa kujitangaza yeye binafsi , Msama ni mwanaccm aliyejaribu kugombea karibu kila kitu kwenye chama hicho na mara zote ameangukia pua , alifanya hivyo akidhani matamasha ya Kwaya yatambeba .

Kitendo cha kuchanganya Tamasha la Pasaka na sherehe za miaka miwili ya Urais wa Samia Suluhu Hassan , hakieleweki , na ni ishara kwamba huyu ametumia Pasaka kutapeli watu huku lengo lake kuu likiwa ni kusherehekea Miaka miwili ya Samia Madarakani , ili labda huko mbele akumbukwe kwenye teuzi , Lakini kwanini Msama atumie Pasaka kwa ajili ya sherehe za urais wa Samia , mbona angeweza tu kuandaa tamasha la sherehe za miaka miwili ya Samia na angekubaliwa tu ? kingine ni hiki , Nape Nnauye hatujui hata kama aliwahi kupata Kipaimara , sasa mtu kama huyu anawezaje kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la kidini tena la shughuli nyeti kama ya Pasaka ?

Nachukua nafasi hii kumkumbusha Nabii Mwamposa kuwa Makini na kutumika kwenye matamasha haya ya kisiasa yaliyovikwa majina ya kidini , yeye angebaki Tanganyika Parkers kuendelea kufungua watu , hawa akina Msama watampoteza .

Naomba kuwasilisha .
Ulitakiwa useme CCM shikamoo kwa kuwa na intelejensi ya kugundua kuwa jamaa ni Tp mazembe!
 
Back
Top Bottom