Talaka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Talaka!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jpinduzi, Nov 19, 2011.

 1. Jpinduzi

  Jpinduzi Senior Member

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 136
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hati ya talaka ni kweli ilikuweko katika jamii ya kiisraeli mwanamume aliweza kutoa hati ya talaka lakini sio kwa kila jambo hasa ni katika uzinzi ambao tutauongelea zaidi katika agano jipya Yesu anaposema Musa aliwaruhusu kutoa haki ya talaka kwa sababa ya ugumu wa mioyo yenu lakini mambo hayakuwa hivyo tangu mwanzo, Injili ya Mtakatifu Mt. 19:3-12.
  Wangapi leo wanakwenda kwa padree au mchungaji na kusema padre\mchungaji mimi leo nimetereza, nimeshindwa mji au ndoa imevunjika. Ni kweli Padre anaweza kushuhudia ndoa na kuitakatifunza lakini hana madaraka ya kusema sakramenti iliyokuwa halali imeisha nadhani watalaamu washeria za kanisa watatusaidia sana hapa. Je hata tunapoamua kuachana kwa nguvu ni kiasi gani cha madhara tunayashuhudia katika familia na jamii nzima?

  Kwa ujumla katika Agano la Kale watoto ni wenye thamani kubwa (Zab 127:4-5). Ndiyo maana katika utasa ruksa ya kuoa mwingine ilitolewa kwa ridhaa ya wana ndoa wote na ndiyo maana iliruhusiwa kumridhi ndugu yako endapo amekufa na kumzalia ndugu yako watoto Kumb 25:5-10, na kijana aliyeoa karibuni hakuruhusiwa kwenda vitani kabla hajazaa watoto kumb 20;7 watototo ilikuwa ni dawa ya kifo kwamba hata wazazi wakifa wanaishi kwa njia ya watoto.

  Dhamani ya watoto sio katika agano la kale tu ila ni katika kila jamii ulimwenguni, ni bahati mbaya kwamba baadhi ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea zimekuwa na utamaduni wa kukataa uzazi kwa hofu ya hali mbaya ya uchumi lakini dawa ya hali mbaya ya uchumi haina maana tupunguze watu kwani chakula kinapopungua mezani dawa sio kupunguza watu ila kuongeza chakula tujenge mazingira ya kuzisaidia familia kubeba majukumu yake.
  Huyo uliyenaye ndie huyo wa kufa na kuzikana acha tamaa na anasa za maisha!!!!!!
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...umeoa?
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Talaka tatu au talaka rejea?
   
 4. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 421
  Trophy Points: 180
  namrudia mke wangu talaka hiyo siitambui.Nalog off
   
 5. data

  data JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,786
  Likes Received: 6,554
  Trophy Points: 280
  cjasoma
   
 6. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Paulo alisema kama mwanamke asiyeamini akiondoka,mwanamume hafungwi,anaweza kuoa tena.The question is,asiyeamini ni nani?LAKINI PIA KAMA IKIGUNDULIKA KWAMBA MWANA NDOA MMOJA ALIINGIZWA KWENYE NDOA BILA RIDHAA YAKE,KWA HILA NK.NDOA HIYO NI BATILI,KWA HIYO INAWEZA KUVUNJWA.
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Sijajua unataka nini! Unaongelea 3 things:
  1 padri kutaitakatifunza ndoa lakini ashindwe kuruhusu kuvunjika kwa ndoa hii
  2 umuhimu wa watoto ktk ndoa (biblically) na umuhimu wa kuzaa kuijaza dunia (bila kujali chakula hakitoshi)
  3 unaasa tuache tamaa manake tulie nao ni wa kufa na kuzikana
  La kwanza umejijibu mwenyewe kuwa ilikatazwa na Yesu mwenyewe,coz mitume waliruhusu shauri ya ugumu wa mioyo ya watu which is still valid I would say, how do hold on a serial cheater!!
  2 tunalazimika kulimit namba ya watoto kutokana na uwezo wa mazingira (resources). Chakula kina limit kwani kinategemea hali ya hewa, wadudu washambulizi na wanyama, rutuba etc. So kama unaweza kulisha watu 30 wewe waweke nyumbani kwako (nna wasiwasi ww msukuma,lol)
  3 naona unakinzana na mtazamo wako wa #1. Sasa kuna situation zingine inabidi uruhusu tu kuachana,it takes two to tangle dude!
   
 8. ram

  ram JF-Expert Member

  #8
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,213
  Likes Received: 912
  Trophy Points: 280
  Mambo ya agano la kale na agano jipya yanakinzana sana binafsi huwa yananichanganya, kwenye suala la ndoa ni bora tungebase kwenye agano moja, ukitafakari sana hata ndoa ya mke zaid ya mmoja ingeruhusiwa tu. Wapi Mpatanishi nasubiri mawazo yako kwenye hili
   
Loading...