Takwimu za Magufuli zinatia shaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takwimu za Magufuli zinatia shaka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by tatanyengo, May 10, 2011.

 1. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Waziri Magufuli anasifika kwa kutaja takwimu mbalimbali zinazohusu wizara yoyote anayoiongoza. Katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, Magufuli alikuwa anajikanganya katika kutoa takwimu kama vile za makandarasi. Mfano, mara anasema makandarasi wako mia saba mara mia tisa. Hilo likanifanya nihisi kwamba pengine data zake haziko sahihi.

  Pia katika kipindi hicho, Maufuli hakumpa mtangazaji nafasi ya kumuuliza maswali ili aweze kueleza issues za wizara yake isipokuwa alichokifanya ni kutaja data mpaka mwisho wa kipindi!
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,923
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  duh inaitwa counter-attack style...kinyume chake kuna mtangazi sstar-tv alishawahi kutumia style hii kwa Dk Slaa,mtangazaji hakumpa nafasi Dk kumwaga data...uzuri wa Dk alimstukia,akamchana live kwamba kama hunipi nafasi uliniitia nini..!!
   
 3. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,856
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  Kwa kweli Magufuli alijitahidi Kuongea ila Ukweli wa Mambo mengi aliyoongea Yana ukweli kidogo, ila vitu Kama Kusema Dar es salaam ina watu milioni nne na Nusu Hadi tano kwa makisio Hilo nakubaliana nalo!! Ila kati ya yote Crap kubwa aliyotoa ni kusema inasadikika dar es salaam ina magari yanayokaribia 800,000 hadi 1,000,000 huu ni uwongo Mkubwa na kuonyesha kama waziri hana data za Uhakika!! Fikiria kwa wastani wa Takwimu zake tuseme dar kuna gari 900,000 ok!! Watu 4,500,000 ok!! Hivyo basi 4,500,000/900,000 = 5 Je wajameni tuseme kwa dar Kila familia ya watu watano kuna gari moja? Hii ni Uzembe wa kufikiri na kama serekali inaonekana Hawana Data sahihi!! Ni aibu!!
  Simpingi Magufuli ila amejaribu lakini awambie wataalamu wake wampe data Kamili! na sio hizi ambazo anapata kwa akina LUKUVI!!!!
  Hivyo basi kwa makisio Yangu ya Haraka Dar es salaam Hakuna magari zaidi ya Laki moja unusu 150,000. ila tatizo ni poor management ya barabara!! Yote haya aliyaongea nashukuru sana!!
  Hivyo basi nashauri aliyoyaongea ayafanyie Kazi kama sio jana basi leo kwani hali inatisha Mzee Magufuli!!
   
 4. m

  mukwano Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni bora tuwe wakweli Bwn Mghufuli kaulizwa maswali mengi na katoa majibu, mara zote alipoulizwa!! Data alizokosea ni zipi, zielezee?????? Nyonge nyongeni lakini haki yake mpeni!!
   
 5. Zamaulid

  Zamaulid JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 16,358
  Likes Received: 6,700
  Trophy Points: 280
  atakuwa mwalimu Mabuga huyo,ndo maana tulimchapa lalago sec!!!
   
 6. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2011
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  si kweli Magufuli alisema

  MAKANDARASI WALIOSAJILIWA WAKO 7000
  NA MAENGINEER WAKO 9000

  HUKUSIKILIZA VIZURI.HATA MIMI SIKUELEWA MWANZO ILA ALIRUDIA TAKWIMU HIZO BAADAE.
  TKUBALI TUU JAMAA NI MMEZAJI MZURI NA HII WIZARA AMEIMEZA PIA
   
 7. I

  Isae Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 79
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kusema ukweli zaidialiulizwa maswali na alijibu vizuri. Ndugu yangu unayebisha takwimuza magari tafadhali go back and work out kwani Dar kuna Institution nyingi, wizara nyingi zenye magari mengi so he might be true
   
 8. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,628
  Trophy Points: 280
  hivi unafikiri bakhresa,sdv(ami),madina,koru,cargo star,mcc,msc,mohamed,manji,simba trailer,trh,tpa,ticts,voda,tigo,twiga...nk.wana magari mangapi ukiachilia mbali wizara,manispaa,watu wenye magali ya abilia na usafiri binafsi?
   
 9. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kwangu Magufuli ni sehemu ya tatizo si sehemu ya ufumbuzi.
  Kesi ya samaki aliisababishia serikari gharama kwa utunzaji wa samaki.
  Nyumba ziliuzwa wizara yake.
  Sasa amefanya baadhi wabomoe nyunba zao, na zoezi limekwamishwa na hachukui hatua. Kila siku anaanzisha nyimbo mpya.
   
 10. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,856
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  Mimi nadhan suala la Kuhusisha pamoja na Big Trucks, Kitu ninachotaka kusema big trucks sums nothing on Numbers, Niambie Mwenyewe Bakhresaa anaweaza kuwa na big Trucks 1,000? 50 tons? That is not true!! Ila data zangu za kusema dar Hakuna gari zaidi ya 150,000 sikurupuki kwani ndio ukweli halisi!! Labda pamoja na pikipiki zinaweza kufikia laki Tatu!! Naomba magufuli atafute data kama hizo za social economic study na sio kutoa data ambazo zinatia walakini, pia ajue any planning inategemea realistic data na sio hizi za kisiasa!! Katika hali ya kawaida kama Tanzania ingekuwa na hiyo ration ya watu watano gari moja nadhan hakuna mtu angepanda daladala!! Wote wangekuwa kwenye private cars kwenye foleni!! Namwomba magufuli afanye traffic Counts kwa major roads hapa dar, na kulinganisha na performance design ya hizo barabara na asipogundua barabara karibu zote zinafanya kazi for a capacity of below 40%.
  Aliongelea kuhusu Mvurugano uliopo kwenye hizo barabara!! Hii inatia aibu kwani inadhihirisha kama hii nchi haina utawala wa sheria!!
  Nenda Mchikichini, Manzese, Ubungo, Mwenge junction, Tegeta na sehemu nyinginezo hali ni Hovyo!! Je hii aionyeshi kama Wakurugenzi wa manisipaa hawajui wajibu wao?? Wafanye planning na kutenga maeneo ya masoko na kuwatoa watu katikati ya barabara!! Hii ni aibu, Sasa nadhan kwa watanzania hatutofautiani sana na wanyama wanavyoishi kwani hata bidhaa zote huwa zinauziwa chini aridhini!! Angalia Kona ya Utumishi magogoni na kariakoo, Ubungo etc,
   
 11. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,856
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  Pia ndugu Zangu wa TRA waweka vifaa maalumu kutambua kodi inayopotea kutokana na uuzwaji wa Ice creams katikati ya barabara na watu wa Tanroads kwa barabara kubwa na Manispaa waweze kuchukua kodi ya pango mamepa kwani maeneo ya barabara yamegeuka ofice za kuuza Azam Icecream bila ulipaji wa pango wala Kodi!! Shame on This!! Promotion za watu wa Simu zimekuwa ni ofice kando kando ya barabara, bila hata kujali maisha ya wateja wao, Hakuna anayesemea kila kitu Mpango wa Mungu ajali ikitokea!!
   
 12. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Ni wasiwasi kama ulisikiliza kile kipindi. Mheshimiwa bwana Magufuli hakutaka kuulizwa maswali. Aligeuza kipindi kile kuwa ni kipindi cha kutolea takwimu za Wizara yake kuhusu barabara, mabango na kadhalika. Kwa bahati mbaya sana kwa sababu Tanzania bado hatujakuwa na waandishi wa kweli wa habari, muandishi aliyekuwa akikiongoza akakubali mheshimiwa awe ndio kiongozi wa kipindi!
  Kulikuwa na maswali muhimu sana ambayo kama kipindi kile kingekuwa cha "Maswali na Majibu' kweli, muendesha kipindi angeweza kuyauliza:

  1. Mheshimiwa anajisikiaje baada ya zoezi lake la bomoa bomoa kuwasitishwa na wakubwa zake wawili, tena kwa namna 'inayomkebehisha' yeye?
  2. Je baada ya kusitishwa huko, anajisikiaje wakubwa hao hao tena wanapomtaka aendelee na zoezi hilo lakini akiwa na hurua?
  3. Vipi ushiriki wake katika sakata la kituo cha petrol cha jijini Mwanza uliosababisha mmiliki wake kwenda mahakamani na kushinda na hivyo kuilazimu Serikali kutoboka mfuko kwa mamilioni kadhaa?
  4...
  5...
  Kipindi cha '45' pengine kilikuwa na concept nzuri lakini naona sasa kimegeuka na kuwa kipindi cha waheshimiwa kuuza sura na kujipigia debe.
   
 13. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,856
  Likes Received: 498
  Trophy Points: 180
  Kweli Magufuli anaweza asiwe bora sana ila ni nani tena anaweza kusimama na kuelezea kuwa anaweza kusimamia utawala wa sheria? Barabara kugeuka office za mobile operators, Vibanda vya Ice cream, Super market za mboga mboga, na kila uozo wa mambo ya kiolela, Hakuna wa kuyasemea sasa wadanganyika tunaona magufuli anaweza kuwa angalau ila pia sioni? Je ndio mambo yametushinda kihivyo? Duh bora tusingedai UHURU MAPEMA. Viongozi wanafikiri kwa kutumia matumbo yao, Wakati wakolono walikuwa wanatumia Ubongo!!

  MAGUFULI TUPO PAMOJA NAWE TUKELEZA ULIYOONGEA JANA ANGALAU KUTAKUWA NA NAFUU
   
 14. s

  smz JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli mwandaaji wa kipindi hiki Semunyu, jana aligeuka msikilizaji. Nadhani Magufuli alitumia njia hiyo kumnyima mtangazaji muda wa kumuuliza maswali ambayo Magufuli hakuwa na majibu.

  Na kama mnavyojua Magufuli ni mzee wa jazba, angeulizwa maswali kama yaliyotajwa hapo juu, basi studio pasingetosha., eidha angemtukana mwandishi au ageidhalilisha serikali. Kwa hiyo naona Magufuli alikuwa anajihami zaidi.

  Nadhani Semunyu kapata somo, atakapokutana na mtu wa aina ya Magufuli ameshajua jinsi ya ku-approach.
   
 15. M

  Marcossy A.M Verified User

  #15
  May 10, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Naamini kuwa Magufuli alikuwa akijitahidi kuuonesha Umma ni namna gani anayajua mambo lakini amekosa nafasi ya kuyafanyia kazi ipasavyo: Kwangu mimi naye amekuwa akilalamika na ni haki kwake. Pamoja na kuainisha matatizo yote yale: tumsaidiaje???? Je, nafasi aliyoipata leo haitoshi kwake kutekeleza wajibu wake na kutatua matatizo aliyoainisha?? na hili lingine lazima tukiri kuwa anahitaji msaada: kuuelewa vema mfumo wa uendeshaji serikali KATIKA INJI yenye serikali huru za Mitaa. KAKA bado kuna mambo yanakuchanganya hapa, OMBA MSAADA WA NDANI.
   
Loading...