Takwimu za bwawa la Nyerere zinastaajabisha sana

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,231
12,733
Nafikiri toka uhuru hatujawahi kufanya mradi mkubwa namna hii. Kukamilika kwake kutatujengea roho ya uthubutu kwenye miradi mikubwa.

Eneo la ziwa litakuwa na ukubwa wa karibu km za eneo 1,350. Hii ni kama mara mbili ya ukubwa wa Mtera. Na kwa eneo litakuwa la tano nyuma ya ziwa Rukwa.

Japo ziwa Rukwa ni kubwa kwa eneo, likiwa na km za mraba 5700+. Ziwa la Nyerere litakuwa na maji mengi zaidi. Km za ujazo 33 dhidi ya 20 za ziwa Rukwa.

Litakuwa ni moja ya maziwa makubwa ya kutengenezwa na binadamu kwa ujazo. Ziwa kubwa kuliko yote la kutengenezwa duniani ni ziwa Kariba, likiwa na ujazo wa km za ujazo 180.

Umeme MW 2100 utatufaa sana. Hope tutaanza kupikia na umeme. Aliyethubutu kuanza mradi huu aliona mbali sana.
 
Back
Top Bottom