Apollo
JF-Expert Member
- May 26, 2011
- 4,920
- 3,221
Hii ndio takwimu iliyopo. Wanafunzi 23,340 sawa na
asilimia 70 ya watakaojiunga na
vyuo vikuu nchini kwa mwaka
wa masomo wa 2011/12
watapata mikopo kutoka Bodi ya
Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu
ya Juu (HESLB).
Hatua hiyo ilitangazwa jana jijini
Dar es Salaam na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB,
Lubambula Machunda,
alipozungumza na waandishi wa
habari.
Machunda alisema kuwa
wanafunzi walioomba kujiunga
na vyuo vikuu kwa mwaka huu
wa masomo kupitia Tume ya
Vyuo Vikuu (TCU) ni 48,477, lakini
baada ya kupitiwa majina hayo,
waliopata udahili ni wanafunzi
37,924 sawa na asilimia 78.
Alisema kuwa wanafunzi 33,692
walifikiriwa na HESLB kwa ajili ya
kupewa mikopo. Hata hivyo,
alisema kati ya hao wanafunzi
23,340 ndio waliokidhi vigezo
vya kupewa mikopo hiyo.
Machunda alisema kuwa HESLB
imetoa mikopo hiyo kwa
kutumia vigezo kadhaa na kutaja
baadhi yake kuwa ni uwezo wa
bajeti, uhitaji wa mwombaji,
programu za vipaumbele,
uwasilishaji wa nyaraka sahihi
na waliowasilisha mikataba kati
ya HESLB na madhamini wa
mwombaji.
Alisema wanafunzi 1,995
wamekosa mikopo kutokana na
sababu mbalimbali. Wanafunzi
138 majina yao ya kuomba
mikopo yalitofautiana na majina
ya waliodahiriwa; 823
walibainika kuwa wanaendelea
kunufaika kwa mikopo; 213
maombi yao
hayakushughulikiwa kutokana
na kubainika kuwa na matatizo
wakati 821 hawakusaini na
kukubaliana na masharti ya
mikopo.
Mwaka huu
wanafunzi waliopewa mikopo ni
wachache kulinganisha na
mwaka jana ambao walikuwa
25,000.
Alisema kuwa sababu
zilizochangia ni kuwepo kwa
waombaji wengi zaidi kuliko
vipaumbele na kwamba mwaka
huu kulikuwepo na kigezo cha
uwazi na usawa.
Kuhusu malalamiko
yanayotolewa na wanafunzi
kuwa utaratibu mpya wa kutoa
mikopo ya wanafunzi wapya
kwa kupelekewa fedha zao
katika vyuo vyao badala ya benki
katika akaunti binafsi, Machunda
alisema kuwa hawapaswi
kulalamika kwa sababu
utawasaidia.
Alisema kuwa utaratibu wa
kupelekewa fedha vyuoni ni
kuisogeza bodi mahali walipo
badala ya kulazimika kila wakati
kwenda kufuatilia fedha zao
HESLB.
Alisema chini ya utaratibu huo
mpya menejimenti za vyuo
zitawajibika kwenda kufuatilia
fedha za wanafunzi badala ya
kazi hiyo kufanya na wanafunzi.
Aidha, Machunda alisema kuwa
kupelekwa kwa fedha hizo
vyuoni kutasaidia kuepusha
uwezekano wa kuwekea fedha
kwenye akaunti ya mwanafunzi
ambaye ameacha masomo ama
kufariki dunia.
Vile vile, alisema kupelekwa kwa
fedha hizo vyuoni
kutaviharakishia vyuo kukata
fedha zao kwa huduma
zilizotolewa kwa wanafunzi.
Alifafanua kuwa kuna wanafunzi
wanaopata huduma za vyuo na
kuahidi kuzilipia baada ya
kupelekewa fedha zao na HESLB,
lakini hawatekelezi ahadi hizo
baada ya kupelekewa fedha na
bodi.
Alisema kuwa hali hiyo imekuwa
ikivilazimisha vyuo kuchukua
hatua mbalimbali, ikiwemo ya
kuzuia matokeo yao.
Katika Bajeti ya mwaka huu wa
fedha 2011/12 HESLB
imetengewa Sh. bilioni 317.8
kwa ajili ya mikopo kwa
wanafunzi wa elimu ya juu
ikilinganisha na mwaka 2010/11
ambao zilitengwa Sh. bilioni
237.8. Source ipp! Nimewakilisha..
asilimia 70 ya watakaojiunga na
vyuo vikuu nchini kwa mwaka
wa masomo wa 2011/12
watapata mikopo kutoka Bodi ya
Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu
ya Juu (HESLB).
Hatua hiyo ilitangazwa jana jijini
Dar es Salaam na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB,
Lubambula Machunda,
alipozungumza na waandishi wa
habari.
Machunda alisema kuwa
wanafunzi walioomba kujiunga
na vyuo vikuu kwa mwaka huu
wa masomo kupitia Tume ya
Vyuo Vikuu (TCU) ni 48,477, lakini
baada ya kupitiwa majina hayo,
waliopata udahili ni wanafunzi
37,924 sawa na asilimia 78.
Alisema kuwa wanafunzi 33,692
walifikiriwa na HESLB kwa ajili ya
kupewa mikopo. Hata hivyo,
alisema kati ya hao wanafunzi
23,340 ndio waliokidhi vigezo
vya kupewa mikopo hiyo.
Machunda alisema kuwa HESLB
imetoa mikopo hiyo kwa
kutumia vigezo kadhaa na kutaja
baadhi yake kuwa ni uwezo wa
bajeti, uhitaji wa mwombaji,
programu za vipaumbele,
uwasilishaji wa nyaraka sahihi
na waliowasilisha mikataba kati
ya HESLB na madhamini wa
mwombaji.
Alisema wanafunzi 1,995
wamekosa mikopo kutokana na
sababu mbalimbali. Wanafunzi
138 majina yao ya kuomba
mikopo yalitofautiana na majina
ya waliodahiriwa; 823
walibainika kuwa wanaendelea
kunufaika kwa mikopo; 213
maombi yao
hayakushughulikiwa kutokana
na kubainika kuwa na matatizo
wakati 821 hawakusaini na
kukubaliana na masharti ya
mikopo.
Mwaka huu
wanafunzi waliopewa mikopo ni
wachache kulinganisha na
mwaka jana ambao walikuwa
25,000.
Alisema kuwa sababu
zilizochangia ni kuwepo kwa
waombaji wengi zaidi kuliko
vipaumbele na kwamba mwaka
huu kulikuwepo na kigezo cha
uwazi na usawa.
Kuhusu malalamiko
yanayotolewa na wanafunzi
kuwa utaratibu mpya wa kutoa
mikopo ya wanafunzi wapya
kwa kupelekewa fedha zao
katika vyuo vyao badala ya benki
katika akaunti binafsi, Machunda
alisema kuwa hawapaswi
kulalamika kwa sababu
utawasaidia.
Alisema kuwa utaratibu wa
kupelekewa fedha vyuoni ni
kuisogeza bodi mahali walipo
badala ya kulazimika kila wakati
kwenda kufuatilia fedha zao
HESLB.
Alisema chini ya utaratibu huo
mpya menejimenti za vyuo
zitawajibika kwenda kufuatilia
fedha za wanafunzi badala ya
kazi hiyo kufanya na wanafunzi.
Aidha, Machunda alisema kuwa
kupelekwa kwa fedha hizo
vyuoni kutasaidia kuepusha
uwezekano wa kuwekea fedha
kwenye akaunti ya mwanafunzi
ambaye ameacha masomo ama
kufariki dunia.
Vile vile, alisema kupelekwa kwa
fedha hizo vyuoni
kutaviharakishia vyuo kukata
fedha zao kwa huduma
zilizotolewa kwa wanafunzi.
Alifafanua kuwa kuna wanafunzi
wanaopata huduma za vyuo na
kuahidi kuzilipia baada ya
kupelekewa fedha zao na HESLB,
lakini hawatekelezi ahadi hizo
baada ya kupelekewa fedha na
bodi.
Alisema kuwa hali hiyo imekuwa
ikivilazimisha vyuo kuchukua
hatua mbalimbali, ikiwemo ya
kuzuia matokeo yao.
Katika Bajeti ya mwaka huu wa
fedha 2011/12 HESLB
imetengewa Sh. bilioni 317.8
kwa ajili ya mikopo kwa
wanafunzi wa elimu ya juu
ikilinganisha na mwaka 2010/11
ambao zilitengwa Sh. bilioni
237.8. Source ipp! Nimewakilisha..