Takwimu ya bodi ya mikopo mwaka huu hii hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takwimu ya bodi ya mikopo mwaka huu hii hapa

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Apollo, Sep 2, 2011.

1. Apollo

Apollo JF-Expert Member

#1
Sep 2, 2011
Joined: May 26, 2011
Messages: 4,889
Likes Received: 1,378
Trophy Points: 280
Hii ndio takwimu iliyopo. Wanafunzi 23,340 sawa na
asilimia 70 ya watakaojiunga na
vyuo vikuu nchini kwa mwaka
wa masomo wa 2011/12
watapata mikopo kutoka Bodi ya
Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu
ya Juu (HESLB).
Hatua hiyo ilitangazwa jana jijini
Dar es Salaam na Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB,
Lubambula Machunda,
alipozungumza na waandishi wa
habari.
Machunda alisema kuwa
wanafunzi walioomba kujiunga
na vyuo vikuu kwa mwaka huu
wa masomo kupitia Tume ya
Vyuo Vikuu (TCU) ni 48,477, lakini
baada ya kupitiwa majina hayo,
waliopata udahili ni wanafunzi
37,924 sawa na asilimia 78.
Alisema kuwa wanafunzi 33,692
walifikiriwa na HESLB kwa ajili ya
kupewa mikopo. Hata hivyo,
alisema kati ya hao wanafunzi
23,340 ndio waliokidhi vigezo
vya kupewa mikopo hiyo.
Machunda alisema kuwa HESLB
imetoa mikopo hiyo kwa
kutumia vigezo kadhaa na kutaja
baadhi yake kuwa ni uwezo wa
bajeti, uhitaji wa mwombaji,
programu za vipaumbele,
uwasilishaji wa nyaraka sahihi
na waliowasilisha mikataba kati
ya HESLB na madhamini wa
mwombaji.
Alisema wanafunzi 1,995
wamekosa mikopo kutokana na
sababu mbalimbali. Wanafunzi
138 majina yao ya kuomba
mikopo yalitofautiana na majina
ya waliodahiriwa; 823
walibainika kuwa wanaendelea
kunufaika kwa mikopo; 213
maombi yao
hayakushughulikiwa kutokana
na kubainika kuwa na matatizo
wakati 821 hawakusaini na
kukubaliana na masharti ya
mikopo.
Mwaka huu
wanafunzi waliopewa mikopo ni
wachache kulinganisha na
mwaka jana ambao walikuwa
25,000.
Alisema kuwa sababu
zilizochangia ni kuwepo kwa
waombaji wengi zaidi kuliko
vipaumbele na kwamba mwaka
huu kulikuwepo na kigezo cha
uwazi na usawa.
Kuhusu malalamiko
yanayotolewa na wanafunzi
kuwa utaratibu mpya wa kutoa
mikopo ya wanafunzi wapya
kwa kupelekewa fedha zao
katika vyuo vyao badala ya benki
katika akaunti binafsi, Machunda
alisema kuwa hawapaswi
kulalamika kwa sababu
utawasaidia.
Alisema kuwa utaratibu wa
kupelekewa fedha vyuoni ni
kuisogeza bodi mahali walipo
badala ya kulazimika kila wakati
kwenda kufuatilia fedha zao
HESLB.
Alisema chini ya utaratibu huo
mpya menejimenti za vyuo
zitawajibika kwenda kufuatilia
fedha za wanafunzi badala ya
kazi hiyo kufanya na wanafunzi.
Aidha, Machunda alisema kuwa
kupelekwa kwa fedha hizo
vyuoni kutasaidia kuepusha
uwezekano wa kuwekea fedha
kwenye akaunti ya mwanafunzi
ambaye ameacha masomo ama
kufariki dunia.
Vile vile, alisema kupelekwa kwa
fedha hizo vyuoni
kutaviharakishia vyuo kukata
fedha zao kwa huduma
zilizotolewa kwa wanafunzi.
Alifafanua kuwa kuna wanafunzi
wanaopata huduma za vyuo na
kuahidi kuzilipia baada ya
kupelekewa fedha zao na HESLB,
lakini hawatekelezi ahadi hizo
baada ya kupelekewa fedha na
bodi.
Alisema kuwa hali hiyo imekuwa
ikivilazimisha vyuo kuchukua
hatua mbalimbali, ikiwemo ya
kuzuia matokeo yao.
Katika Bajeti ya mwaka huu wa
fedha 2011/12 HESLB
imetengewa Sh. bilioni 317.8
kwa ajili ya mikopo kwa
wanafunzi wa elimu ya juu
ikilinganisha na mwaka 2010/11
ambao zilitengwa Sh. bilioni
237.8. Source ipp! Nimewakilisha..

2. Perry

Perry JF-Expert Member

#2
Sep 2, 2011
Joined: Feb 24, 2011
Messages: 10,029
Likes Received: 868
Trophy Points: 280
Hao 823 wanao endelea kunufaika na mkopo,wananufaika kivip,au ndo sound?

3. Apollo

Apollo JF-Expert Member

#3
Sep 2, 2011
Joined: May 26, 2011
Messages: 4,889
Likes Received: 1,378
Trophy Points: 280
Nilijua tu member mwenye akili ya kufikiria angeuliza hili swali. Yaani hata mimi sielewi ni changa la macho au?

4. V

Villneth Member

#4
Sep 2, 2011
Joined: Aug 19, 2011
Messages: 16
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Sasa mkuu, inamaana hata tuki appeal kuomba tena mambo hayabadilik! Manake wengne tuna sifa zote bt tumekosa mikopo

5. Apollo

Apollo JF-Expert Member

#5
Sep 2, 2011
Joined: May 26, 2011
Messages: 4,889
Likes Received: 1,378
Trophy Points: 280
kwa kweli sina cha kukujibu kwa kuwa hata mimi nimelishangaa hilo.

6. V

Villneth Member

#6
Sep 2, 2011
Joined: Aug 19, 2011
Messages: 16
Likes Received: 0
Trophy Points: 0

duh 2naumia vbaya mno jaman, waki2fkiria ntashukur mungu

7. Apollo

Apollo JF-Expert Member

#7
Sep 2, 2011
Joined: May 26, 2011
Messages: 4,889
Likes Received: 1,378
Trophy Points: 280
usiwe na shaka ndugu yangu. Naamini watawafikiria vyema. Makesure unakata rufaa, usikubali haki yako ipotee.

8. Perry

Perry JF-Expert Member

#8
Sep 2, 2011
Joined: Feb 24, 2011
Messages: 10,029
Likes Received: 868
Trophy Points: 280

majina waliyoyatoa hayafk hata 18000 so stl kuna mengne watatoa nxt wk nadhan.

9. Mwita Maranya

Mwita Maranya JF-Expert Member

#9
Sep 2, 2011
Joined: Jul 1, 2008
Messages: 10,569
Likes Received: 105
Trophy Points: 145
Huyu Lubambula Machunda kumbe bado yupo? aisee huyu mkulu niligombana nae sana miaka ile bado wizara ya elimu ya juu inashughulika na mikopo moja kwa moja kabla ya kuwepo loan board, alikuwa mnoko na mbabaishaji, sishangai hata huko loan board efficincy yao ni zero kwa kuwa na watu kama huyu.

Ningependa kufahamu utaratibu wa kupata mikopo kwa wale waliochaguliwa kwa "equivalent" entry nao wamepata mikopo na majina yao yametoka ama bado "michakato" inaendelea??

10. Apollo

Apollo JF-Expert Member

#10
Sep 2, 2011
Joined: May 26, 2011
Messages: 4,889
Likes Received: 1,378
Trophy Points: 280
mkuu inaonekana umepitia historia ndefu ya maisha. Mpaka huyu jamaa unamjua! Sorry bado sijajua mchakato huo unaendeleaje.

11. Eshacky

Eshacky JF-Expert Member

#11
Sep 2, 2011
Joined: Apr 26, 2011
Messages: 966
Likes Received: 33
Trophy Points: 45
Asilete porojo! Tuliokosa n weng kuliko waliopata!

12. V

Villneth Member

#12
Sep 2, 2011
Joined: Aug 19, 2011
Messages: 16
Likes Received: 0
Trophy Points: 0

ofcoz ntajtahd nfanye hvo ndg yng, thanx

13. Apollo

Apollo JF-Expert Member

#13
Sep 2, 2011
Joined: May 26, 2011
Messages: 4,889
Likes Received: 1,378
Trophy Points: 280
ure welcome mkuu. Kila la kheri.

14. V

Villneth Member

#14
Sep 2, 2011
Joined: Aug 19, 2011
Messages: 16
Likes Received: 0
Trophy Points: 0

jaman napga magot kwa my God angalau iwe hvo. Maisha magum hme duh

15. Apollo

Apollo JF-Expert Member

#15
Sep 2, 2011
Joined: May 26, 2011
Messages: 4,889
Likes Received: 1,378
Trophy Points: 280
usiwe na shaka. Mungu hamtupi mja wake.

16. Baba Collin

Baba Collin JF-Expert Member

#16
Sep 2, 2011
Joined: Aug 1, 2011
Messages: 458
Likes Received: 0
Trophy Points: 33
Apollo unafanya vzuri kuwapa moyo hawa wandugu.kama ulifatilia vzur tbc1 leo asubuhi jamaa walikuwepo pale na walisema tayari wametoa 79.5bil.kwa mwaka wa kwanza ambazo ndo zilitengwa.hvyo ukichukua idad ya pesa yote iliyotolewa utagundua kua kwel imefika 79.5 bil.
Hvyo kuhusu mikopo game is over.

17. Apollo

Apollo JF-Expert Member

#17
Sep 2, 2011
Joined: May 26, 2011
Messages: 4,889
Likes Received: 1,378
Trophy Points: 280
duh kama game over kuna watu wengi nawaonea huruma sana ndugu yangu.

18. Apollo

Apollo JF-Expert Member

#18
Sep 3, 2011
Joined: May 26, 2011
Messages: 4,889
Likes Received: 1,378
Trophy Points: 280
Hebu tupige mahesabu tuangalie kuna wangapi wamepata ktk matokeo yaliyotoka ktk web yao then tutoe na hiyo idadi tuone kama kuna matokeo mengine yamebanwa au yatatolewa nxt week.

19. d

dy/dx JF-Expert Member

#19
Sep 3, 2011
Joined: Jul 26, 2011
Messages: 622
Likes Received: 17
Trophy Points: 35

Sidhani kama kuna mengine sababu mimi niko kwenye S afu namba yangu iko kwenye elfu ishirini,hivyo hesabu zao zitakuwa sawa.

20. Perry

Perry JF-Expert Member

#20
Sep 3, 2011
Joined: Feb 24, 2011
Messages: 10,029
Likes Received: 868
Trophy Points: 280

acha kuvunja wenzio moyo dogo.

Loading...