Takwimu: Kikwete amejitahidi katika kipindi chake jamani

gwamaka aswile

Senior Member
Mar 26, 2015
186
106
BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA-KIKWETE AMEJITAHIDI KATIKA KIPINDI CHAKE JAMANI-TAKWIMU HIZI

Na mpombe mtalika.

Wakati tukikaribia kumaliza mwaka 2014 na kuingia mwaka 2015 pia kama taifa tunagemea kusheherekea miaka 53 kama taifa huru tangu tulipopata uhuru mwaka tarehe 9 ya mwezi 12 mwaka 1961 chini ya uongozi wa Mw. Juliasi Kambarage Nyerere na chama chake cha TANU baadae CCM.

Kumekuwepo na utaratibu au utamaduni wa kubeza mafanikio na kutokukubali kwa dhati kabisa na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali rais Jakaya Kikwetena chama chake cha CCM.

Kuna wachache walisema hawauoni ubunifu wala utendaji kazi, uchapakazi wa Rais na uadilifu na uawaminifu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Mimi ninaomba nitumie fursa hii kupingana nao na kuwaomba waende wakafanye utafiti kwanza kabla ya kuongea, kubeza na kudharau mafanikio ya Serikali ya CCM ya awamu ya Nne.

Lakini tuondokane na utamaduni wa kubeza mafanikio na kudharau kila kitu ili mradi tu sisi ni Wapinzani, na kuwa mpinzani si kupinga kila kitu ikiwa pamoja na maendeleo, Kumekuwepo na mafanikio mengine ya kujivunia tangu tupate uhuru ingawa kuna baadhi ya watu hawaridhishwi na kasi ya maendeleo iliyopo, ni ukweli usiopingika kuwa bado tunachangamoto za hapo na pale lakini yatupasa kuubali ukweli tumetoka mbali na mafanikio yamepatikana na yanaendelea kupatikana katika awamu zote tatu na ya a sasa anayomalizia Rais Jakaya Kikwete.

Katika awamu hii ya nne kumekuwa na mafanikio ambayo hayakuwahi kutokea ktk nchi hii hata kama baadhi ya watu hawapendi kusikia hivyo, kwa uchache tumefanikiwa katika sekta mbalimbali kama elimu,afya, miundo mbinu na mambo chungu mzima ambayo tukisema tuyataje hapa hatutapa nafasi ya kutosha.

Tukianzia na elimu sote tunakumbuka kuwa serikali yake iliibua mpango wa ujenzi wa sekondari za kata kwa sababu nafasi za wanafunzi kuingia sekondari zilikuwa zimekuwa finyu kiasi cha kwamba ni asilimia kati ya 6 na 10 ya watoto wote waliokuwa wanamaliza shule za msingi mwaka 2005 walikuwa wanaingia sekondari wakati anaingia madarakani.

Pamoja kejeli nyingi zilizoelekezwa kwa shule za sekondari za kata kiasi cha kuitwa Yeboyebo katika miaka ya mwanzoni ya shule hizo, bado zimekuwa na mafanikio makubwa, ambayo ni sehemu ya mafanikio makubwa ya sekta ya elimu katika miaka tisa ya uongozi wa rais KIkwete.

Rais Kikwete alitangaza hivi karibuni kuwa Serikali yake inaangalia uwezekano wa kufuta ada katika shule za sekondari zilizo chini ya serikali, ili kuboresha sera ya elimu na kuhakikisha kila mwanafunzi anayeanza darasa kwanza anamaliza kidato cha nne.

Hii ya kufuta ada itasaidia kila mtoto anayeanzadarasa la kwanza anakuwa na nafasi ya kumaliza sekondari kwa maana ya kidato cha nne bila kulazimika kuacha shule kwa sababu ya ada.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, zilikuwepo jumla ya shule za sekondari 1,745 mwaka 2005 zikiwemo shule 1,202 za Serikali na sasa ziko jumla ya shule za sekondari 4,576 zikiwemo shule 3,528 za Serikali.

Baadhi ya mafanikio hayo kama vile upanuzi mkubwa wa elimu ya msingi na uandikishaji wa watoto kuingia shule, upanuzi wa elimu ya sekondari, ongezeko kubwa la wanafunzi wa shule za sekondari, upanuzi wa elimu ya juu ambako sasa kuna vyuo vikuu 51, vikiwemo 15 vya umma, ongezeko la fedha za mikopo ya elimu kutoka sh bilioni 16 mwaka 2005 na kufikia bilioni 345 kwa sasa, kuongezeka kwa wakopaji kutoka wanafunzi 16,000 mwaka 2005 hadi kufikia 95,000 kwa sasa.

Sote tu mashahidi ya kuwa Rais Kikwete alivyoingia alikutana na changamoto mbalimbali ikiwamo ukame ambapo tathimini inaonyesha kuwa mwaka 2006 jumla ya ngombe 250,000, mbuzi 130,000, kondoo 122,000 pamoja na punda zaidi 700 walikufa kutokana na ukame wa ukosefu wa maji, jumla ya mifugo yote hiyo ilikuwa na thamani ya zaidi ya billion 45.3 Baada ya ukame kupungua serikali ya rais Kikwete ikakutana na mtihani mwingine wa kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kusababisha ongezeko la bei katika sekta ya usafiri.

Mtihani mwingine kwa serikali ya Rais Kikwete ilikuwa ilikuwa ni mtikisiko wa wa uchumi duniani ambayo uliathiri kwa kiasi kikubwa kwa mataifa yanayoendelea na yaliyokuwa yameandelea na kuathiri bajeti za chi kadhaa duniani, lakinin kwa uimara wa serikali yake hatukuyumbishwa na mtikisiko huu wa uchumi wa dunia mwaka 2009.

Rais kikwete pia amefanikiwa kuondoa uhasama wa visiwani unguja na pemba uliodumu kwa miaka 10 ambapo aliyemstaafu Benjamini Mkapa aliwahi kukiri baada ya kutoka madarakani kuwa mgogoro wa visiwa hivyo vya Karafuu ulikuwa unamnyima usingizi wakati wa utawala.

Mgogoro huo wa kisiasa ulifikia hatua mbaya kiasi ambacho hata ndugu wa baba mdogo na mkubwa walishindwa kuzikana pamoja na kuombana maji kutokana na misimamo na itikadi ya vyama vyao, lakini leo twaona wazanzibar wote wamekuwa wamoja na wakimbizi waliokwenda Mombasa walirejea nchini.

Pia tuumeshuhudia mabadiliko makubwa katika sekta ya afya pamoja na kuboresha huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili. Serikali ya rais Kikwete imeongeza huduma za ubingwa kwa kiasi kikubwa sana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hususani huduma Dental.

Sasa hivi Kituo cha Dental cha Muhimbili ndicho kituo kikubwa kuliko vituo vingi katika Afrika Mashariki na nchi zote zilizopo Sub-Sahara Africa.

Lakini pia Rais wetu kwa jitihada zake binafsi amejitahidi kujenga Kituo cha kufanya Operesheni za Moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo mpaka sasa operesheni za moyo zaidi ya 400 zimefanyika kwa mafanikio ndani kipindi cha miaka 3.

Hospital hiyo ya rufaa kwa sasa inatoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa figo huduma nyingine nyingi za rufaa za rufaa amabazo hapo awali hazikuwepo.

Bila shaka katika miaka michache ijayo Watanzania wanaohitaji huduma za rufaa watakuwa hawapelekwi nje ya nchi kwa ajili ya kupata huduma hizo, watazipata hapa hapa kwetu.

Haya ni mambo machache ambayo rais wetu ameyafanya katika Sekta ya Afya na ni mambo ambayo yatakuwa Legendre pindi atakapokuwa amemaliza uongozi wake kwa Taifa letu.

HospitaliOcean roard imetangazwa na na tume ya nyuklia duniani kuwa ni mfano hospitali bora ya tiba ya kansa barani Afrika.

Mafanikio ya nchi yanapimwa kimataifa na hivi sasa kigezo kikubwa cha kupima maendeleo ya nchi ni malengo ya millennia.

Tanzania ni mojawapo ya nchi duniani ambayo ilitekeleza huduma za afya ya msingi kwa mafanikio makubwa sana baada ya uhuru, hii ni kauli ya Rais wa baraza kuu la 65 la UN mwaka 2011 Bw. Joseph Deiss alisema Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano barani Afrika.

Miongoni mwa mafanikio kwenye sekta ya afya pamoja na huduma za afya zimesogezwa karibu wananchi,Utoaji wa chanjo za kuzuia magonjwa mbalimbali bure na chanjo kuhusu mama na mtoto, Kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5.

Huduma ya kinga ya maambukizi ya ukimwi toka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto. Kupungua magonjwa yanayosababishwa na maji, magonjwa hayo ni pamoja na kipindupindu na homa ya matumbo.

%86 miongoni mwa kaya maskini wanatumia huduma za vituo vya afya vya serikali ,Utoaji wa dawa za kupunguza makali ya Ukimwi bure, Utoaji wa tiba ya kifua kikuu na ukoma bure.

Kutokomeza magonjwa mbalimbali ambayo hapo awali yalikuwa ni kero, Kuongeza ajira kwenye sekta ya afya pamoja na kujenga Kujenga miondombinu ya afya.

Katika upambanaji dhidi ya adui " maradhi" kupitia katika sekta muhimu ya afya nchini kuna mengi yamefanyika na yanaonekana waziwazi.

Mathalani kulikuwa na ujenzi wa Zahanati mpya ambapo mwaka 2006 kulikuwa na zahanati 4,679 hadi kufika 2009 zilifika 5,422, huku vituo vya afya vikitoka 526 na kuwa 663, pia makazi ya waganga hayakuasahaulika kwani jumla ya nyumba 394 za waganga zilijengwa mpkaka mwaka 2012 july.

Ongezeko hilo la zahanati na vituo vya afya limekwenda sanjari na ongezeko la madaktari wauguzi na wakunga.

Wakati Kikwete akiingia madarakani 2005 kulikuwa na madaktari 3,528 na mpaka leo hii kuna jumla ya 4,502, pia madaktari wasaidizi nao wakiongezekakutoka 9,028 hadi kufikia 14,017 kwa sasa Akina mama nao hawajasahaulika kwani napo kuna ongezeko la idadi ya wauguzi na wakunga kutoka 18,123 hadi kufikia 23,886.

Ongezeko hilo na uwepo wa jitihada za dhati toka kwa serikali imeabibisha vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano vimepungua ambapo mwaka 2005 kulikuwa na vifo 158 kwa kila watoto, 1000 na kushuka hadi kufikia 75 tathimini hii ni mpaka july 2012.

Kuna mafanikio ya kujivunia katika sector ya ajira pamoja malalamiko ya ukosefu wa ajira lakini kuna hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa na hasa ukizingatia kuwa hakuna sehemu yoyote duniani usiyosikia kelele hizi hata kwa hao mataifa makubwa kelele hizi nipo, lakini pia majirani zetu wanakimbila Tanzania kufatuta ajira kwa kuamini kuna nafuu ya kupata ajira jambo ambalo ni kweli.

Kwa miaka miwili ya 2011/2012 jumla ya ajira 250,678 zilipatikana ambapo vijana waliajiriwa ni 9,056,217 sawa na %80.6 ya vijana nguvu kazi yote ya vijana waliostahili kuajiriwa kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi katika miaka hiyo 2011/2012 Yatupasa kukumbuka mwaka 2011 /2012 kwa mujibu wa takwimu za shirika la kazi duniani ILO na shirika la UNDP matatizo ya ajira yalikuwa kama ifuatavyo kwa baadhi ya nchi ,Ugiriki matatizo ya ajira ni 92% ,Spain matatizo ya ajira ni 55%, Italia matatizo ya ajira ni 38%,.

Africa ya Kusini matatizo ya ajira ni 40% na jirani zetu Kenya matatizo ya- Vijana waoajiriwa ni 9,056,217 sawa na %80.6 ya vijana nguvu kazi yote ya vijana katika miaka hiyo miwili waliostahili kuajiriwa kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi.

Kwa upande wa kimataifa na utawala bora Tanzania imepiga hatua kubwa sihitaji kulizungumzia hilo kwa sanatunajua ugeni wa rais wa china na rais Obama pamoja na kuingia mikataba ya maendeleo kwa nchi yetu.

Ikumbukwe kuwa Apri mwaka huu rais Kikwete alipata tuzo ya heshima ya kuwa rais mwenye mchango mkubwa kwa nchi yake barani Africa kwa mwaka 2013.

Tuzo hiyo ya heshima ilitolewa na jarida maarufu la African Leadership Magazine Group, MjiniWashington DC ilipokelewa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Mhe Bernard Membe. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka kwa viongozi wa Africa wenye mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii.

Kwa watanzania tuliowengi rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha kuwa mstahamilivu, shupavu mwenye msimamao na mpenda haki na asiyechukua maamuzi ya kukurupuka kwa maneno ya vijiweni ambayo mengi ni uzushi na uongo yenye kuleta ochonganishi baina wananchi na serikali yao walioichagua.

Pia rais kikwete ni mtu wa watu anayesikiliza kilio cha cha watu, mwisho namenda kumpongeza mheshimiwa rais kwa kuturudishia JKT kwa vijana wanaomaliza kidato cha sita kwa muda mchache tangu JKTilirudi imerudisha nidhamu na uzalendo na umoja na kuipenda nchi yetu.

Kurejeshwa kwa JTK kutatuondolewa mavazi maarufu ya kata k, ambayo yaliongezeka baada ya kufutwa kwa mafunzo hayo Jeshi la kujenga Taifa.
 
Kwa hiyo unatwambia kuwa amejitahidi na sio kwambe ameweza!?
Nazidi kumwombea usiku na mchana chama hiki kikongwe kisifie mikononi mwake pia maana dalili si nzuri!
 
Umesahau kumwambia kasaidia dola imepanda
na vile vile tutamkumbuka kwa kusaidia kupanda kwa deni la taifa
hajawahi kutokea rais kama huyu
 
1 usd= 2000 tsh..nlipokumbuka hii wala sijaangaika na kusoma hizo siasa zote!!
 
Duuuh, kiongozi pole sana. Takwimu zina namna yake ya kuzidadavua.Hivyo ulivyofanya wanatakiwa wafanye wanasiasa sio mtu wa jukwaa hili. Mfano wakati Mh. Kikwete anaingia madarakani kakuta katika kila wanafunzi 100 wanaoanza s/msingi ni wanafunzi chini ya 5% ndio wanaofika chuo kikuu hali hii anaiacha hivi hivi. Kuna viwango vya kimataifa mfano daktari 1 anatakiwa atibu wagonjwa 10,000 kwa Tanzania daktari 1 hutibu wagonjwa 30,000 (Raia Mwema no. 307). Uchambuzi wako wa kitakwimu una matatizo makubwa. Serikali yenyewe katika ripoti ya uchumi 2012/2013 imekiri pamoja na uchumi kukua kwa wastani wa 7% umaskini umekuwa ikipungua kwa wastani wa 2%.
 
BANIANI MBAYA KIATU CHAKE DAWA-KIKWETE AMEJITAHIDI KATIKA KIPINDI CHAKE JAMANI-TAKWIMU HIZI

Na mpombe mtalika.

Wakati tukikaribia kumaliza mwaka 2014 na kuingia mwaka 2015 pia kama taifa tunagemea kusheherekea miaka 53 kama taifa huru tangu tulipopata uhuru mwaka tarehe 9 ya mwezi 12 mwaka 1961 chini ya uongozi wa Mw. Juliasi Kambarage Nyerere na chama chake cha TANU baadae CCM.

Kumekuwepo na utaratibu au utamaduni wa kubeza mafanikio na kutokukubali kwa dhati kabisa na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali rais Jakaya Kikwetena chama chake cha CCM.

Kuna wachache walisema hawauoni ubunifu wala utendaji kazi, uchapakazi wa Rais na uadilifu na uawaminifu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Mimi ninaomba nitumie fursa hii kupingana nao na kuwaomba waende wakafanye utafiti kwanza kabla ya kuongea, kubeza na kudharau mafanikio ya Serikali ya CCM ya awamu ya Nne.

Lakini tuondokane na utamaduni wa kubeza mafanikio na kudharau kila kitu ili mradi tu sisi ni Wapinzani, na kuwa mpinzani si kupinga kila kitu ikiwa pamoja na maendeleo, Kumekuwepo na mafanikio mengine ya kujivunia tangu tupate uhuru ingawa kuna baadhi ya watu hawaridhishwi na kasi ya maendeleo iliyopo, ni ukweli usiopingika kuwa bado tunachangamoto za hapo na pale lakini yatupasa kuubali ukweli tumetoka mbali na mafanikio yamepatikana na yanaendelea kupatikana katika awamu zote tatu na ya a sasa anayomalizia Rais Jakaya Kikwete.

Katika awamu hii ya nne kumekuwa na mafanikio ambayo hayakuwahi kutokea ktk nchi hii hata kama baadhi ya watu hawapendi kusikia hivyo, kwa uchache tumefanikiwa katika sekta mbalimbali kama elimu,afya, miundo mbinu na mambo chungu mzima ambayo tukisema tuyataje hapa hatutapa nafasi ya kutosha.

Tukianzia na elimu sote tunakumbuka kuwa serikali yake iliibua mpango wa ujenzi wa sekondari za kata kwa sababu nafasi za wanafunzi kuingia sekondari zilikuwa zimekuwa finyu kiasi cha kwamba ni asilimia kati ya 6 na 10 ya watoto wote waliokuwa wanamaliza shule za msingi mwaka 2005 walikuwa wanaingia sekondari wakati anaingia madarakani.

Pamoja kejeli nyingi zilizoelekezwa kwa shule za sekondari za kata kiasi cha kuitwa Yeboyebo katika miaka ya mwanzoni ya shule hizo, bado zimekuwa na mafanikio makubwa, ambayo ni sehemu ya mafanikio makubwa ya sekta ya elimu katika miaka tisa ya uongozi wa rais KIkwete.

Rais Kikwete alitangaza hivi karibuni kuwa Serikali yake inaangalia uwezekano wa kufuta ada katika shule za sekondari zilizo chini ya serikali, ili kuboresha sera ya elimu na kuhakikisha kila mwanafunzi anayeanza darasa kwanza anamaliza kidato cha nne.

Hii ya kufuta ada itasaidia kila mtoto anayeanzadarasa la kwanza anakuwa na nafasi ya kumaliza sekondari kwa maana ya kidato cha nne bila kulazimika kuacha shule kwa sababu ya ada.

Kwa mujibu wa takwimu rasmi, zilikuwepo jumla ya shule za sekondari 1,745 mwaka 2005 zikiwemo shule 1,202 za Serikali na sasa ziko jumla ya shule za sekondari 4,576 zikiwemo shule 3,528 za Serikali.

Baadhi ya mafanikio hayo kama vile upanuzi mkubwa wa elimu ya msingi na uandikishaji wa watoto kuingia shule, upanuzi wa elimu ya sekondari, ongezeko kubwa la wanafunzi wa shule za sekondari, upanuzi wa elimu ya juu ambako sasa kuna vyuo vikuu 51, vikiwemo 15 vya umma, ongezeko la fedha za mikopo ya elimu kutoka sh bilioni 16 mwaka 2005 na kufikia bilioni 345 kwa sasa, kuongezeka kwa wakopaji kutoka wanafunzi 16,000 mwaka 2005 hadi kufikia 95,000 kwa sasa.

Sote tu mashahidi ya kuwa Rais Kikwete alivyoingia alikutana na changamoto mbalimbali ikiwamo ukame ambapo tathimini inaonyesha kuwa mwaka 2006 jumla ya ngombe 250,000, mbuzi 130,000, kondoo 122,000 pamoja na punda zaidi 700 walikufa kutokana na ukame wa ukosefu wa maji, jumla ya mifugo yote hiyo ilikuwa na thamani ya zaidi ya billion 45.3 Baada ya ukame kupungua serikali ya rais Kikwete ikakutana na mtihani mwingine wa kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kusababisha ongezeko la bei katika sekta ya usafiri.

Mtihani mwingine kwa serikali ya Rais Kikwete ilikuwa ilikuwa ni mtikisiko wa wa uchumi duniani ambayo uliathiri kwa kiasi kikubwa kwa mataifa yanayoendelea na yaliyokuwa yameandelea na kuathiri bajeti za chi kadhaa duniani, lakinin kwa uimara wa serikali yake hatukuyumbishwa na mtikisiko huu wa uchumi wa dunia mwaka 2009.

Rais kikwete pia amefanikiwa kuondoa uhasama wa visiwani unguja na pemba uliodumu kwa miaka 10 ambapo aliyemstaafu Benjamini Mkapa aliwahi kukiri baada ya kutoka madarakani kuwa mgogoro wa visiwa hivyo vya Karafuu ulikuwa unamnyima usingizi wakati wa utawala.

Mgogoro huo wa kisiasa ulifikia hatua mbaya kiasi ambacho hata ndugu wa baba mdogo na mkubwa walishindwa kuzikana pamoja na kuombana maji kutokana na misimamo na itikadi ya vyama vyao, lakini leo twaona wazanzibar wote wamekuwa wamoja na wakimbizi waliokwenda Mombasa walirejea nchini.

Pia tuumeshuhudia mabadiliko makubwa katika sekta ya afya pamoja na kuboresha huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili. Serikali ya rais Kikwete imeongeza huduma za ubingwa kwa kiasi kikubwa sana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hususani huduma Dental.

Sasa hivi Kituo cha Dental cha Muhimbili ndicho kituo kikubwa kuliko vituo vingi katika Afrika Mashariki na nchi zote zilizopo Sub-Sahara Africa.

Lakini pia Rais wetu kwa jitihada zake binafsi amejitahidi kujenga Kituo cha kufanya Operesheni za Moyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo mpaka sasa operesheni za moyo zaidi ya 400 zimefanyika kwa mafanikio ndani kipindi cha miaka 3.

Hospital hiyo ya rufaa kwa sasa inatoa huduma za matibabu ya ugonjwa wa figo huduma nyingine nyingi za rufaa za rufaa amabazo hapo awali hazikuwepo.

Bila shaka katika miaka michache ijayo Watanzania wanaohitaji huduma za rufaa watakuwa hawapelekwi nje ya nchi kwa ajili ya kupata huduma hizo, watazipata hapa hapa kwetu.

Haya ni mambo machache ambayo rais wetu ameyafanya katika Sekta ya Afya na ni mambo ambayo yatakuwa Legendre pindi atakapokuwa amemaliza uongozi wake kwa Taifa letu.

HospitaliOcean roard imetangazwa na na tume ya nyuklia duniani kuwa ni mfano hospitali bora ya tiba ya kansa barani Afrika.

Mafanikio ya nchi yanapimwa kimataifa na hivi sasa kigezo kikubwa cha kupima maendeleo ya nchi ni malengo ya millennia.

Tanzania ni mojawapo ya nchi duniani ambayo ilitekeleza huduma za afya ya msingi kwa mafanikio makubwa sana baada ya uhuru, hii ni kauli ya Rais wa baraza kuu la 65 la UN mwaka 2011 Bw. Joseph Deiss alisema Tanzania ni nchi ya kupigiwa mfano barani Afrika.

Miongoni mwa mafanikio kwenye sekta ya afya pamoja na huduma za afya zimesogezwa karibu wananchi,Utoaji wa chanjo za kuzuia magonjwa mbalimbali bure na chanjo kuhusu mama na mtoto, Kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5.

Huduma ya kinga ya maambukizi ya ukimwi toka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto. Kupungua magonjwa yanayosababishwa na maji, magonjwa hayo ni pamoja na kipindupindu na homa ya matumbo.

%86 miongoni mwa kaya maskini wanatumia huduma za vituo vya afya vya serikali ,Utoaji wa dawa za kupunguza makali ya Ukimwi bure, Utoaji wa tiba ya kifua kikuu na ukoma bure.

Kutokomeza magonjwa mbalimbali ambayo hapo awali yalikuwa ni kero, Kuongeza ajira kwenye sekta ya afya pamoja na kujenga Kujenga miondombinu ya afya.

Katika upambanaji dhidi ya adui “ maradhi” kupitia katika sekta muhimu ya afya nchini kuna mengi yamefanyika na yanaonekana waziwazi.

Mathalani kulikuwa na ujenzi wa Zahanati mpya ambapo mwaka 2006 kulikuwa na zahanati 4,679 hadi kufika 2009 zilifika 5,422, huku vituo vya afya vikitoka 526 na kuwa 663, pia makazi ya waganga hayakuasahaulika kwani jumla ya nyumba 394 za waganga zilijengwa mpkaka mwaka 2012 july.

Ongezeko hilo la zahanati na vituo vya afya limekwenda sanjari na ongezeko la madaktari wauguzi na wakunga.

Wakati Kikwete akiingia madarakani 2005 kulikuwa na madaktari 3,528 na mpaka leo hii kuna jumla ya 4,502, pia madaktari wasaidizi nao wakiongezekakutoka 9,028 hadi kufikia 14,017 kwa sasa Akina mama nao hawajasahaulika kwani napo kuna ongezeko la idadi ya wauguzi na wakunga kutoka 18,123 hadi kufikia 23,886.

Ongezeko hilo na uwepo wa jitihada za dhati toka kwa serikali imeabibisha vifo vya watoto wenye umri chini ya miaka mitano vimepungua ambapo mwaka 2005 kulikuwa na vifo 158 kwa kila watoto, 1000 na kushuka hadi kufikia 75 tathimini hii ni mpaka july 2012.

Kuna mafanikio ya kujivunia katika sector ya ajira pamoja malalamiko ya ukosefu wa ajira lakini kuna hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa na hasa ukizingatia kuwa hakuna sehemu yoyote duniani usiyosikia kelele hizi hata kwa hao mataifa makubwa kelele hizi nipo, lakini pia majirani zetu wanakimbila Tanzania kufatuta ajira kwa kuamini kuna nafuu ya kupata ajira jambo ambalo ni kweli.

Kwa miaka miwili ya 2011/2012 jumla ya ajira 250,678 zilipatikana ambapo vijana waliajiriwa ni 9,056,217 sawa na %80.6 ya vijana nguvu kazi yote ya vijana waliostahili kuajiriwa kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi katika miaka hiyo 2011/2012 Yatupasa kukumbuka mwaka 2011 /2012 kwa mujibu wa takwimu za shirika la kazi duniani ILO na shirika la UNDP matatizo ya ajira yalikuwa kama ifuatavyo kwa baadhi ya nchi ,Ugiriki matatizo ya ajira ni 92% ,Spain matatizo ya ajira ni 55%, Italia matatizo ya ajira ni 38%,.

Africa ya Kusini matatizo ya ajira ni 40% na jirani zetu Kenya matatizo ya- Vijana waoajiriwa ni 9,056,217 sawa na %80.6 ya vijana nguvu kazi yote ya vijana katika miaka hiyo miwili waliostahili kuajiriwa kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi.

Kwa upande wa kimataifa na utawala bora Tanzania imepiga hatua kubwa sihitaji kulizungumzia hilo kwa sanatunajua ugeni wa rais wa china na rais Obama pamoja na kuingia mikataba ya maendeleo kwa nchi yetu.

Ikumbukwe kuwa Apri mwaka huu rais Kikwete alipata tuzo ya heshima ya kuwa rais mwenye mchango mkubwa kwa nchi yake barani Africa kwa mwaka 2013.

Tuzo hiyo ya heshima ilitolewa na jarida maarufu la African Leadership Magazine Group, MjiniWashington DC ilipokelewa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa,Mhe Bernard Membe. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka kwa viongozi wa Africa wenye mchango mkubwa wa kiuchumi na kijamii.

Kwa watanzania tuliowengi rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha kuwa mstahamilivu, shupavu mwenye msimamao na mpenda haki na asiyechukua maamuzi ya kukurupuka kwa maneno ya vijiweni ambayo mengi ni uzushi na uongo yenye kuleta ochonganishi baina wananchi na serikali yao walioichagua.

Pia rais kikwete ni mtu wa watu anayesikiliza kilio cha cha watu, mwisho namenda kumpongeza mheshimiwa rais kwa kuturudishia JKT kwa vijana wanaomaliza kidato cha sita kwa muda mchache tangu JKTilirudi imerudisha nidhamu na uzalendo na umoja na kuipenda nchi yetu.

Kurejeshwa kwa JTK kutatuondolewa mavazi maarufu ya kata k, ambayo yaliongezeka baada ya kufutwa kwa mafunzo hayo Jeshi la kujenga Taifa.

Mkuu umesahau umeme na Bara bara, amaejenga bara bara ndefu za lami kuliko marais wote waliomtangulia combined, chini ya utawala wake, wananchi wengi zaidi wameunganishiwa umeme katika historia ya Tanzania
 
Kwa uzumbukuku wangu nilidhani kuwa mtu akipewa nafasi hatakiwi kujitahidi, ni kufanya kwa 100%
 
Tatizo la marais wa Tanzania kila akiingia madarakani anaanza kufanya mabo mapya akiacha kabisa aliyoanzisha mtangulizi wake, lakini Kikwete kidogo amejitahidi: Shule za Kata hakuanzisha yeye alianzisha Benjamini William Mkapa ila ametekeleza kwa kiasi fulani ingawaje na wapambe wake wangependa sifa zote zimwendee yeye binafsi. Barabara zote anazodaiwa kuzijenga maandalizi yake, hata upembuzi yakinifu wa miradi hiyo ulifanywa na mtangulizi wake.
Umaskini umeongezeka ingawaje takwimu za kupikwa zinaonyesha uchumi umekuwa na umaskini kupungua hali halisi ya maisha ya watu imedidimia zaidi.
Serkali yake haina fedha shule zinafungwa Hospitali hakuna dawa mifuko ya jamii imefilisiwa na serikali yake. Siamini kama ni kweli unamsifu kwa dhati moyo wako nadhani unamkejeli tu
Mkuu umesahau umeme na Bara bara, amaejenga bara bara ndefu za lami kuliko marais wote waliomtangulia combined, chini ya utawala wake, wananchi wengi zaidi wameunganishiwa umeme katika historia ya Tanzania
 
Mkuu umesahau umeme na Bara bara, amaejenga bara bara ndefu za lami kuliko marais wote waliomtangulia combined, chini ya utawala wake, wananchi wengi zaidi wameunganishiwa umeme katika historia ya Tanzania

Kwa Mikopo aliyoiingizia taifa,hata Mtoto wa darasa laTano angefanya zaidi ya hayo.
 
Naona wanaomtetea Kikwete hawaelewi kitu kimoja kikubwa

Kikwete kafanya 'mengi na makubwa' katika urais wake

tatizo ni kuwa alipata nafasi ya kufanya hayo aliyoyafanya mara 50 au zaidi...
kwa hiyo tukimpima kwa nafasi na mazingira aliyofanyia kazi ndo tunamuona
'ameshindwa' kama urais wake alitengeneza ajira milioni 3 wakati kumbe alikuwa na uwezo
wa kutengeneza ajiramilioni 20...tutamhukumu kuwa 'kashindwa'
hatusemi hajafanya kitu
 
Cyo kajitahidi bali amefanya vzr zaidi kuliko marais wote waliomtangulia, huo ndo ukweli mengine ni wivu tuu,
 
kuwa na kikwete kama raisi ni aibu na fedheha kubwa sana aende zaje hatumhitaji.
 
Kipindi cha Kikwete dadangu alikuwa anafanya kazi halmashauri ya Bagamoyo mishahara ikawa inalipwa na tajiri aitwaye Shubash Patel.

Yaani Ikawa halmashauri inakopa hela ya mishahara kwa mtu i.e mtu alikuwa na hela kuliko serikali.
 
Watu wakurupukaji sana aisee!Hivi unaweza kutuwekea vithibitisho hapa?.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom