Takwimu hizi zinatisha..!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takwimu hizi zinatisha..!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwenda_Pole, Sep 21, 2009.

 1. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  WANAFUNZI wanne wa shule za sekondari wilayani Karagwe, wamehukumiwa kwenda jela miezi sita kila mmoja kwa kosa la kushindwa kuwataja waliowapa ujauzito na kusababisha washindwe kuendelea na masomo.

  Wanafunzi hao kutoka shule za sekondari za Nyabiyonza, Nkwenda na Bugene ambao majina yao yamehifadhiwa, walihukumiwa kifungo hicho hivi karibuni na Mahakama ya Wilaya ya Karagwe.

  Akizungumzia adhabu za wanafunzi hao, Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Kanali mstaafu Fabian Masawe, alisema wazazi wanapaswa kushirikiana na serikali kupiga vita watu wanaowakatisha masomo watoto walio chini ya umri, kwani hao ndio rasilimali ya taifa.

  Masawe alisema mahakama ya wilaya imewahukumu watoto hao wa kike kwenda jela miezi sita kila mmoja, kutokana na kushindwa kuwataja waliowapa ujauzito na kushindwa kutoa ushirikiano kwa mahakama ili kuwatia hatiani wahalifu hao.

  Alisema wanafunzi hao wamepelekwa katika mahakama za watoto watukutu ili iwe fundisho kwa watoto wengine wenye tabia kama hiyo.

  Kwa mujibu wa Kanali Masawe, takwimu zilizopo ofisini kwake zinaonyesha kuwa wanafunzi tisa wa shule za sekondari wamepata ujauzito katika kipindi cha Januari hadi sasa.


  Pia alisema asilimia 85 ya wanafunzi waliopimwa, wamekutwa na virusi vya ugonjwa wa ukimwi.

  Kutokana na hali hiyo, amewaomba wananchi kuwafichua wazazi wanaowaozesha watoto wao walio chini ya umri, wanaowakatisha masomo wanafunzi kwa kuwapa ujauzito ili waweze kufikishwa mbele ya mikono ya sheria.


  Source: Tanzania Daima, 21st September 2009

  Hapo kwenye bold, huyu mwandishi atakuwa amekosea nini...???? au angetuambia tu ni wangapi jumla walipimwa kisha ikapatikana hiyo 85% otherwise hali inatisha...
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kazi kweli kweli. Hivyo hakuna Mahakama za watoto?? unawezaje kumsaidia mtoto mdogo kama akifungwa, au ndio Elimu ya uzazi hawana, inawezekana kabisa kuwa hawa wanafunzi hawajui hata wakina nani waliwapa mimba
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Walipimwa wanafunzi wangapi? itasaidia kupata confidence interval. Kama kweli hizo takwimu ni sahihi basi hili ni janga la taifa....ina maana karibia wananchi wote huko wameathirika!
   
 4. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  inatisha kidogo sio sana - inawezekana kabisa waliwapima wanafunzi ambao wako kwenye high risk ya maambukizi, mfano hao wenye mimba tayari, ambao inamaanisha wao kinga hawajali vile vile.
  Pia ingekuwa bora kutupa sample size, yaani walipimwa wanafunzi wangapi, kwa mfano inatisha kuambiwa wanafunzi 200 wamepimwa, 85% wakawa na virusi (sawa na wanafunzi 170) lakini kama wamepima wanafunzi 10 (9 wakawa na virusi) n stori mbili ama takwimu mbili tofauti kabisa.
   
 5. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  hata kama 10 wamepimwa na 9 wamekutwa nao, bado ni idadi kubwa sana. ndio maana wanatumia %
  85% ni wanafunzi nane kati ya kumi
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Sheria za nchi ndizo zinazopelekea watoto kujazana mimba ,halafu angalia huko jela wanamueka mtu mwenye mimba kwa muda wa miezi sita , hivi watampatia lishe bora ,napo hapa pana ujinga fulani.

  Kwanini wasiruhusu anaetaka kuolewa awache shule, kwisha, ukipata mimba unaachishwa shule na kama ni kuendelea kusoma uendelee kwenye shule za private na sio za serikali japo nazo siku hizi ni za kulipia.

  Kuna makabila wanaozesha watoto wao wakiwa wadogo tu na watu wanaishi miaka mingi mpaka wanafikwa na mauti ,nimefuatilia habari za vikongwe na stori zao wanakwambia waliolewa wakiwa ni wadogo.

  Mambo ya kusema kunaharibiwa Taifa la kesho hayana mshiko kwa hapa Tanzania.
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  wakati mwingine mahakama hazitendi haki
   
 8. M

  Mkubwa Dawa Member

  #8
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mahakama inabidi wawaachie huru au wanafunzi wenye ujauzito kwani huko sio kuwatendea haki bali la msingi ni kuwatafuta hao waliowapa ujauzito na labda kuwapa mimba.
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hebu fikiria watoto watazaliwa jela kwa kosa la wazazi! mhhhh sijui tunataka jenga taifa lipi.
   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hipocrisy at its best, Masawe mwenyewe kashatafuna sana kina Felista pale Mgulani.

  Halafu kuwafunga hawa victim kunaonyesha system yetu ilivyo inhumanly quixotic.
   
 11. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Kwkweli busara inahitajika kwenye mambo sensitive kama haya. Huko jela wamewapeleka watawapa matunzo gani. Sasa inamaana hao watoto watakaozaliwa siyo Taifa la kesho? kwamba linahukumiwa kuzaliwa jela?? Hawa mahakimu sasa naona ni wajinga. Mmoja anaagiza wauaji waachiwe na uchunguzi ufanyike kuwatafuta wauaji, huyu ameshindwa nini kuagiza Polisi wawatufute waliowatia mimba?? Busara hata hairuhusu hata waliowatia mimba kufungwa maana haitawasaidia wenye mimba, ila wangepewa jukumu la kulea mtoto na baadaye watoto na baadaye kuhakikisha aliyekatishwa masomo anarudishwa masomoni na kuhakikishiwa elimu ya kiwango, basi lingekuwa kweli Taifa limelindwa. Lakini kama kuna mjinga anayedhani kuwafunga hao watoto ni sahihi! Basi ni masikitiko matupu. Kuna Vacuum ya Busara kwenye mahakama zetu.
   
 12. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Afu inawezekana wamepata mimba kwa miujiza kama kwenye vitabu vya dini.
   
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kama hii asilimia 85 haikukosewa, hii ndiyo ilitakiwa kuwa habari kubwa kwenye headline.
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Na kama hawamjui aliyewapa uja uzito? Walitaka wasingizie mtu? Na wakimtaja mkubwa mwenzetu ( Mahita et.al) mbona tunakataa kuwaamini?Kuwafunga hawa kutasaidia nini? Je wangepata mimba nje ya shule? Kosa ni wao kusoma au nini? Kama alivyosema Bluray, Hypocrisy of the highest level! Sisi watoto wetu wakipata uja uzito, tunawatoa mimba, tunawahamisha shule n.k. Wanyonge tunawafunga. Kama tulivyomhukumu kifo mbwa immigration!

  Amandla.......
   
  Last edited: Sep 22, 2009
 15. O

  Ogah JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu vipi hapo aisee
   
 16. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Thats the word.
   
 17. O

  Ogah JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo asifanye kazi kwa sababu "alitafuna Felista"..........nilifikiri jambo la msingi hapo la kuuliziwa ni uhalali wa hiyo adhabu......au?

  ...........otherwise 85% inatisha sana
   
 18. b

  bnhai JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Huu ndo uandishi wetu. I went through the newspaper in the morning. Nimeona ni kichekesho. Hakuna ukweli hata kidogo, u will soon hear them denying the stats. Sijui editor hakuona??? Hata Lesotho hawajafikia hapo
   
 19. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2009
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kweli. Hata kama statistics ni za uongo lakini kumfunga mtoto kwa vile hakumtaja aliyempa mimba! Na akimtaja, kumfunga jamaa miaka 30! Tunataka kujenga au kukomoa?

  Amandla.........
   
 20. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Huyo mzee hana jipya. Anatafuta pa kupitia ili Mkuu wa Kaya amwone kuwa anachapa kazi.
   
Loading...