PreGE2025 TAKUKURU yataka uchaguzi ndani ya vyama uwe uhuru

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Nyie fanyeni maigizo tu na ma-ushungi wenu. Hamjui damage mnayoifanya kwenye nchi ya Tanzania. Si mmeamua kubadilisha uovu uwe ndiyo halali, na haki ndiyo iwe uovu? Madhara yake yatakuja kuwapata wengi wenu. Najua kuna wengi wanafaidika kwa ufisadi lakini hata hizo mali zitakuja kuwa za moto. Hili ni suala la muda tu.
Ufisadi imekuwa ndiyo mafanikio
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Njombe imetoa wito kwa vyama vya siasa nchini kuhakikisha michakato ya uchaguzi wa ndani inafanyika kwa uhuru na haki, ili kupata viongozi waadilifu na walioko tayari kujitolea kuleta maendeleo bila kushawishiwa na vitendo vya rushwa.

Wito huo umetolewa Mei 28, 2025 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Njombe, Kassim Ephrem, wakati wa kikao na vyombo vya habari kilicholenga kueleza mafanikio ya taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2025.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Ili tuwe na uchaguzi wa haki, ni lazima michakato ya ndani ya vyama iheshimu katiba, kanuni na sheria za nchi. Wanachama wasikubali kudhalilishwa kwa kupewa rushwa. Mtu akichaguliwa kwa njia ya rushwa, anapotwaa nafasi hufikiria namna ya kurudisha fedha alizotumia badala ya kuhudumia wananchi,” amesema Ephrem.

Waende pia kwenye tume ya uchaguzi Tanzania ili isiwe tume ya uchafuzi

Waende na huko kwa msajili wa vyama vya siasa nako kuna tuhuma mbalimbali
 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Njombe imetoa wito kwa vyama vya siasa nchini kuhakikisha michakato ya uchaguzi wa ndani inafanyika kwa uhuru na haki, ili kupata viongozi waadilifu na walioko tayari kujitolea kuleta maendeleo bila kushawishiwa na vitendo vya rushwa.

Wito huo umetolewa Mei 28, 2025 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Njombe, Kassim Ephrem, wakati wa kikao na vyombo vya habari kilicholenga kueleza mafanikio ya taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2025.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

“Ili tuwe na uchaguzi wa haki, ni lazima michakato ya ndani ya vyama iheshimu katiba, kanuni na sheria za nchi. Wanachama wasikubali kudhalilishwa kwa kupewa rushwa. Mtu akichaguliwa kwa njia ya rushwa, anapotwaa nafasi hufikiria namna ya kurudisha fedha alizotumia badala ya kuhudumia wananchi,” amesema Ephrem.

Ila nje ya chama uwe wa magumashi
 
Back
Top Bottom