Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Njombe imetoa wito kwa vyama vya siasa nchini kuhakikisha michakato ya uchaguzi wa ndani inafanyika kwa uhuru na haki, ili kupata viongozi waadilifu na walioko tayari kujitolea kuleta maendeleo bila kushawishiwa na vitendo vya rushwa.
Wito huo umetolewa Mei 28, 2025 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Njombe, Kassim Ephrem, wakati wa kikao na vyombo vya habari kilicholenga kueleza mafanikio ya taasisi hiyo kwa kipindi cha Januari hadi Machi 2025.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
“Ili tuwe na uchaguzi wa haki, ni lazima michakato ya ndani ya vyama iheshimu katiba, kanuni na sheria za nchi. Wanachama wasikubali kudhalilishwa kwa kupewa rushwa. Mtu akichaguliwa kwa njia ya rushwa, anapotwaa nafasi hufikiria namna ya kurudisha fedha alizotumia badala ya kuhudumia wananchi,” amesema Ephrem.