TAKUKURU yamshikilia Mhasibu Wizara ya Afya kwa ubadhilifu wa fedha

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019



Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), mkoani Kilimanjaro inamshikilia Mhasibu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa tuhuma za kufanya ubadhirifu wa zaidi ya Sh. milioni 34 katika fedha za chanjo ya Rubella.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mjini Moshi, Kamanda wa TAKUKURU, mkoani hapo, Holle Makungu, amesema taasisi hiyo inamshikilia Mhasibu huyo kutokana na kufanya makosa hayo kinyume na kifungu cha 22 na 28 vya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Amesema mhasibu huyo ambaye anajulikana kwa jina la Yahya Athuman, alimdanganya mwajiri wake na kufanya ubadhirifu wa fedha za umma zaidi ya Sh. milioni 34.2.

Aidha amesema Uchunguzi wa TAKUKURU unaonyesha kuwa mwaka 2014 wizara iliendesha zoezi la chanjo ya Rubella katika halmashauri mbalimbali ikiwemo halmashauri ya Moshi Vijijini na kwamba wahasibu kutoka wizara hiyo walipewa jukumu la kusimamia fedha hizo na kufanya ubadhirifu huo.

“Sh. milioni 491.8 ziliwekwa kwenye akaunti na zilikuwa na maelekezo na Yahya alikabidhiwa ili asimamie matumizi katika Halmashauri za Manispaa ya Moshi, Moshi vijijini, Siha, Hai, Rombo, Mwanga na Same “amesema.
 
Kumbe TAKUKURU ina vijitawi vingi eh...AKUKURU😑..

yote kwa yote hayamfanyi mtanzania maskini akapata mlo akisoma madude yenu haya...tupishe sie
 
“Sh. milioni 491.8 ziliwekwa kwenye akaunti na zilikuwa na maelekezo na Yahya alikabidhiwa ili asimamie matumizi katika Halmashauri za Manispaa ya Moshi, Moshi vijijini, Siha, Hai, Rombo, Mwanga na Same “amesema.
Mbowe ana kesi ya kujibu!
 
Takukuru iongeze kasi,wezi hasa wenye madaraka makubwa wasafishwe kila kona. Wazame vizuri kwenye halmashauri zetu huko nikama wanakwepakwrpa...
 
Takukuru iongeze kasi,wezi hasa wenye madaraka makubwa wasafishwe kila kona. Wazame vizuri kwenye halmashauri zetu huko nikama wanakwepakwrpa...
Hapa sasa tumeelewana naisi,hii nchi ni yetu sote tunapaswa kukemea pale mambo yanapokuwa ovyo,na tunaitaji kusifia pale tunapoona hatua inachukuliwa,nchi imeoza sanaaaaaaa mbele ya viongoz wa ccm ,sasa tunapoona rais anachukua hatua wote tusapot kuijenga nchi ili hata watoto wetu na wajukuu wakute kitu
 
Adabu inahijika sana kwenye fedha za Umma.Na Tume ya Maadili ya viongozi wa Umma imecharuka sasa hivi imekunjua makucha yake.Ushindi 2020 ni asubuhi na mapemaaaa
 
Since 2014 ? leo ndio uchunguzi umekamilika au ndio wamegundua leo? kdg naona kama hatupo serious
Uchunguzi wa Takukuru huchukua muda sana maana unakuta Mhasibu huyo alikuwa anaendelea na kazi zake kama kawaida pia lazima wachunguze hata wafanyakazi wengine bila ya kuwasitisha kuendelea kutoa huduma.
Pia nyaraka za serikali kwa kawaida mpaka miaka mitano ipite...
 
Back
Top Bottom