TAKUKURU wamtokea Lukuvi..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAKUKURU wamtokea Lukuvi.....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Sajenti, Jun 17, 2010.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kuna habari kuwa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU inafanya uchunguzi juu ya tuhuma za Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni mbunge wa jimbo wa Isimani mkoani Iringa William Lukuvi kuhusiana na tuhuma za kutoa msaada wa pikipiki 68 na baiskeli 68 katika jimbo hilo. Kitendo cha Lukuvi kutoa pikipiki na baiskeli hizo kimeonekana kama ni utoaji wa rushwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na raisi.....

  My take: I doubt kama kweli Takukuru watakuja na kitu kipya katika suala hilo maana inapokuja wana-CCM kutuhumiwa zinapigwa chenga tu. Lakini mimi naona ni rushwa ya wazi tu hiyo kwa nini pikipiki na baiskeli leo na isiwe miaka ya nyuma??...Lukuvi huyo huyo anawataka Takukuru na polisi eti kumkamata afisa ardhi wa manispaa ya kinondoni kwa kuuza maeneo ya wazi.....:ballchain::ballchain:
   
 2. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #2
  Jun 17, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Sajenti usishangae sana bali jua safari yetu tunakaribia kufika huko tunakokutaka bila kutaka
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Jun 17, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Jana Lukuvi ameagiza baadhi ya maofisa wa Wilaya ya Kinondoni wasirudi ofisini mwao ili kupisha Takukuru wachunguze juu ya sakata la kuuza maeneo ya wazi.
  Nadhani ni busara zaidi na yeye akazuiwa kukanyaga ofisini kwake ili kuwapa nafasi Takukuru wamchunguze juu ya sakata lake.
  Otherwise itakuwa ni usanii kama ule wa Tkukuru kuchunguza mkataba wa Richmond.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jun 17, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,753
  Trophy Points: 280
  TAKUKURU kuchunguza misaada ya Lukuvi


  [​IMG]Thursday, 17 June 2010 04:28
  Na John Daniel
  Majira


  SIKU mbili baada ya Mbunge wa Isimani mkoani Iringa, Bw. William Lukuvi kutoa pikipiki 68 na baiskeli 68 katika jimbo lake, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUURU) imesema itachunguza misaada ya kiongozi huyo.

  Wakati TAKUKURU wakitoa msimamo huo Bw. Lukuvi kwa upande wake ameitetea misaada yake kuwa haina hata chembe ya rushwa kwa kuwa inalenga kukisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na ni mfululizo wa misaada yake ya zaidi ya sh. milioni 500 aliyotoa jimboni humo tangu mwaka 1997.

  Akizungumza Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya Bw. Lukuvi kufungua mafunzo ya siku mbili ya wakurugenzi wa majiji, manispaa na halmashauri zote nchini, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dkt. Edward Hoseah alisema tayari uchunguzi juu ya suala hilo umeanza.

  "Hakuna aliye juu ya sheria, tayari nimemwagiza ofisa wangu wa kanda kushughulikia suala hilo, tulishazungumza kuhusu misaada kama hiyo kwa kipindi hiki, "alisema Dkt. Hoseah.

  Alisema Wabunge wanapaswa kuheshimu sheria kwa kuwa wao ndio wadau wakuu katika kuzitunga na kwamba ni muhimu kuelimsiha wananchi umuhimu wa kutii sheria.
  Kwa upande wake, Bw. Lukuvi ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi huo kwa kofia ya ukuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alisema msaada wake aliyotoa juzi inalenga kusaidia kuwaunganisha wana-CCM na kujianda vyema kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu.

  "TAKUKURU hawana sababu wala haja ya kunichunguza, msaada wangu wa juzi wa pikipiki na baiskeli nilitoa kwa chama changu cha mapinduzi na si kwa mtu, nenda ukaulize ukikuta kuna kitu kimeandikwa jina la mtu utaniambia.

  "Mimi ni kiongozi wa chama, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, nina wajibu kukisaidia chama changu, nimeanza kutoa msaada tangu mwaka 1997 na mwaka 2000 pia nilitoa, nimesaidia chama kununua magari mawili ya Wilaya ya Iringa Vijijini, msaada wa jana ni mdogo sana ukilinganishwa na yale niliyokwishatoa," alisema Bw. Lukuvi.

  Alisema kwa mujibu wa taratibu za CCM, kiongozi yeyote wa chama hicho anao wajibu wa kukisaidia bila kikwazo na kwamba TAKUKURU hawawezi kuingilia kati suala hilo.
  "lakini siwezi kuwakatalia TAKUKURU kufanya kazi zao kama wakiamua kufuatilia wanayo haki, japo naamini misaada yangu haina kitu wala dalili za rushwa," alisisitiza Bw. Lukuvi

  "Jumla ya misaada yangu kwa jimbo langu na chama changu ni sh. 541,350,000, sijatoa peke yangu, wapo marafiki zangu walionisaidia na nimewataja hapa, hii siyo siri na nimeamua kutoa kitabu hiki ili kila anayelalamika au anayefkiri kwamba nimeanza kufanya hivyo juzi au jana ajue ukweli uko wapi," alisema Bw. Lukuvi huku akinukuu 'taarifa ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2005-2010, Jimbo la Ismani Iringa.
  Alisema wanaodadisi misada yake kwa sasa ni maadui wake kisiasa na wasiolitakia mema jimbo lake na wananchi wake na kuhoji sababu ya watu hao kutoona misaada ya mamilioni aliyoanza kutoa kwa miaka mingi sasa.

  "Hivi wanaohoji misaada yangu ya juzi walikuwa wapi wakati natoa ile ya mamilioni kwa mtindo huo huo wa wazi kama niliyofanya juzi? Kila nikitoa misaada nahitisha waandishi wa habari, wananchi wote na wana-CCM wot,e mbona hawajawai kuhoji hadi juzi?" alihoji Bw. Lukuvi.

  Kwa mujibu wa kitabu hicho cha Bw. Lukuvi washirika wake waliomsaidia kutoa misaada hiyo ni pamoja na Kanisa Anglikana Tanzania, Kanisa Katoliki, WCS, Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Benki ya Posta, NSSF, PPF, PSPF, TANAPA, Ubalozi wa Marekani, Ubalozi wa Japan na Ubalozi wa Korea Kusini.

  Mashirika mengine ni pamoja na Mfuko wa Wanyamapori, ASSAS, F.M Abri, MBOMIPA, Mbeya Cement, Twiga Cement, Idara ya Wanyamapori, DAHACO, ZAIN, Mzee Flikos na wengine ambao hawakutajwa.

  "Nimetaja kila kijiji, kila kata na aina ya misaada iliyotolewa, naomba kila mwenye shaka apitie hiki kitabu au aendele akawaulize, tuzungumzie maendeleo wananchi wetu bado wanahitaji sana misaada tushikimane nao kuondoa umaskini," alisema Bw. Lukuvi.`  MAONI YANGU:
  Alikuwa wapi huyu Lukuvi miaka yote hii asitoe misaada katika jimbo lake hadi asubiri mwaka 2010? Hii ni rushwa haina kificho kabisa na huyu na wengine wote walioanza kumwaga rushwa katika majimbo yao washughulikiwe ipasavyo ili kukomesha chaguzi zilizojaa rushwa ndani ya Tanzania yetu ambazo zinatupa Viongozi wabovu kuanzia ngazi za juu kabisa za uongozi ndani ya Tanzania ambao wameweka mbele maslahi yao badala ya yale ya Watanzania.
   
 5. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2010
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mi hata sijui wanachunguza nini wakati kila kitu kiko wazi........... usikute hao takukuru wanajiosha tu kwa umma ili tujuwe wanafanya kazi lakini hakuna kitu chochote kitakacho amuriwa juu yake. Ni kulinda maslahi ya chama.

  Hivi huyu ni mkuu wa mkoa wa dar na pia ni mmbunge wa isamilo..........hivi haya majukumu yake anayafanye jamani? Kwa nini watu wanavyeo zaidi ya kimoja tena vyote very demanding kwa wakati mmoja........... halafu tunashangaa tuko masikini.......ahhhhhgrrrruuuuuuuueeeeeppppppppp
   
 6. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hii ni rushwa tena ametumia cheo chake cha ukuu wa Mkoa kujikusanyia mapesa ya kutoa rushwa jimboni. Nani asiyeweza kuelewa jinsi ambavyo cheo chake na Ubunge vimekaa namna ambayo hawezi kabisa kuepuka kujikita katika hali tata kama hiyo. Kwa vyovyote ni lazima kutakuwepo na "conflict of interests" katika utendaji kazi za Mkuu wa Mkoa ambao ni mji Mkuu wa nchi na hapo hapo Mbunge wa Mkoa mwingine. Ukifanyika uchunguzi wa kutosha hata hao waliomchangia watakuwa walipewa au kuidhinishiwa kitu na yeye mwenyewe kama viwanja kontrakt nk. Hao anaowalaumu kuwa wameuza maeneo ya wazi watamkumbusha aliyoyafanya yeye kwa hao hao waliomchangia. Swala litakuwa tu kusubiri usanii wa TAKUKURU.
   
 7. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  wizi mtupu!!!!!!!!!!!!!!
   
 8. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kumbe unalijua hilo Mkuu?
   
 9. T

  Tall JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  mbona nilikutana na mpiga kura wake mmoja akasema lukuvi hagombei tena?
   
 10. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #10
  Jun 24, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Hata kuwavaa watu wa Idara ya Ardhi ilikuwa ni cover up ya tuhuma zake lukuki. ndio maana Mwenyekiti wa Tume aliyounda ni mtu ambaye ana tuhuma nyingi za kugushi nyaraka, double allcation ya viwanja na na kupanda mawe juu ya ardhi zenye hati miliki. Hamna kitu!!!!!!!!
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  muosha huosha haha
   
Loading...