TAKUKURU waanze kufuatilia hii michango holela kupitia kampeni za media

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,950
29,532
Kuna kampeni na uhamasishaji mbalimbali unaofanywa na vyombo vya habari kama vile kuwaombea michango watoto wenye magonjwa mbalimbali na baadae kuwapeleka kwenye matibabu ingawa ni mara chache sana tunapata mrejesho wa kiasi halisi kilichochangwa au hata taarifa kamili ya kilichojiri kwa mgonjwa.

Hoja hii inajikita katika mashaka ya kiasi gani hasa cha fedha huchangwa na kutangazwa kuwa kimechangwa??

Kuna haja kubwa ya TAKUKURU kufuatilia aina hii ya fursa ya upigaji.
 
Kuna kampeni na uhamasishaji mbalimbali unaofanywa na vyombo vya habari kama vile kuwaombea michango watoto wenye magonjwa mbalimbali na baadae kuwapeleka kwenye matibabu ingawa ni mara chache sana tunapata mrejesho wa kiasi halisi kilichochangwa.

Kuna haja kubwa ya takukuru kufuatilia aina hii ya fursa ya upigaji.

unaonaje TAKUKURU ikianza uchunguzi wa rambirambi ya Bukoba na Arusha??
 
Unaungana na Makonda kuwapiga vita clouds!Clouds endeleeni na moyo huo wa kuwasaidia walio katika hali ngumu ambao hawana pa kuomba msaada!
Makonda ametuamsha kuhusu hili jambo...tumewahi kusikia uhamasishaji wa watu kuombewa fedha za kwenda India kufanyiwa upasuaji wa Matende....sijawahi kupata mrejesho wa wagonjwa kama wanepona au la...na je gharama za matibabu zilikuwaje?

Isije ikawa ni njia ya kutakatishia fedha chafu.

HII NI HOJA NZITO SANA
 
Hata mtenda mema mtampiga vita kumtetea Bashite na watu wa aina yake!
 
unaonaje TAKUKURU ikianza uchunguzi wa rambirambi ya Bukoba na Arusha??
Kwa taatifa yako hiyo fedha ya maafa huwa inakaguliwa kama fedha nyingine zote za serikali...

Hoja ya Rambirambi ipo ...tukutane kule kule
 
Kama kuna fununu za ubadhirifu weka wazi mkuu isije kuwa UNATUMIKA kisiasa
 
Hata mtenda mema mtampiga vita kumtetea Bashite na watu wa aina yake!
Takukuru ni taasisi huru na ya haki...hapo haonewi wala kutetewa mtu....ni vizuri utaratibu huu ukaanza....inaelekea hii style ya harambee na kuchangiachangia ndio style ya upigaji wa hela na pengine kutakatishia fedha haramu.
 
Nasema hivi,hayo mnasema sasa kutokana na uhasama uliopo!Mpaka mkosane na mtu ndio muanze kutafuta kumshurutisha!Wakati urafiki umenoga mbona hamkusema hayo?
Mwenye akili anajua
 
Takukuru imchunguze Gambo anyedaiwa kutumia million tisa kupamba uwanja wa mpira,siku ya kuaga miili ya marehemu
 
Ni kweli kabisa Mkuu ila utanikubalia hii ya kwako umeileta kwa unafiki baada ya kutoka kule..
Ukifikiria kwa mtindo huo basi mada za members wote humu zitakuwa za kinafiki....na pengine hara swali lako litakuwa la kinafiki kwani na wewe inaelekea umetoka kule kule.
 
okey basi kwenye maelezo yako omba TAKUKURU wachunguze michango yote ikiwepo Rambirambi ya Bukoba na Arusha.
Naanza na hii michango kupitia media...kama rambirambi zenye kupitia media zipo basi na zenyewe ni sehemu ya mjadala.

Hoja ya msingi ni Takukuru kufanya ukaguzi wa kina na ufuatiliaji...siamini kama watanzania wana roho nzuri ,huruma na uwezo wa kuchangia hivyo ..liko jambo nyuma ya pazia...ni Takukuru wenye nafasi ya kutuambia na pengine law enforcers wanaweza kulichukulia kwa umuhimu wa kipekee.
 
Back
Top Bottom