TAKUKURU Tabora yamsaka Paul Christian kuhusiana na tuhuma za cheti feki

Nchi hii bana.... Kwanini hao TAKOKURU wasimwambie MAKONDA atoe vyeti vyake original na then waende NECTA kujiridhisha?
 
Ningemshauri atakapokwenda tena aende na wakili wake,wasije wakampoteza.
 
Mmmmnnhhh....mbona huko mawizarani wakikuta cheti kinatumiwa na mtu zaidi ya mmoja hawawaiti takukuru...???!!! na kuna case nyingi tu ...wanawaambia wahusika walete original...ambaye si chake anaingia mtini...wala hakuna anayemtafuta awape story alikipataje...na mmiliki halali kuulizwa kilifikaje kwa x....


Kwa ufupi ni ngumu kumkamata owner hata kama kakiuza...atasema sijui...
Kuna njia nyingi za mtu kupata copy ya cheti cha mtu...anaweza hata waomba masijala wampe copy ya cheti chochote...kukana ni very easy...

Au unaenda mahali kutoa photo copy wao wanatoa extra...ngumu kumkamata true owner...
Mkuu vikisemwa vyeti ni originals, siyo vivuli.
 
Ajibu maswali uongo wake na pia alipokea kiasi gani kudanganya kuwa aliuza cheti chake au kutoa jina lake kutumika.

Makonda angekuwa na kosa basi huyo angeshamalizana nao, ana kitu anaficha alipokea bahasha kumchafua RC mpendwa wa taifa letu na mchapa kazi.
 
Hii zuga tu wala hakuna jipya hapo wenyew wanajuana hawa.
 
Hapana mkuu, huyo Paul Christian anaingia katika sakata hilo kwa kushirikiana na mtuhumiwa kupeana vyeti au cheti. Mtu akipatikana anatumia cheti au vyeti vyako, yeye ataingia kwenye hatia na wewe pia mwenye vyeti utaingia kwenye hatia. Jinsi ilivyo inaonekana inakua treated kama RUSHWA.
hamjaelewa nyiee... ishu hapo ni kwamba.. mwenye cheti halisi.. alichomolewa cheti chake na dadayake ambae alikuwa kimada wa daudi bashite wakati huo. na kilichomolewa bila muhusika kujua. haya yalikuwa ni makubaliano kati ya BASHITTE na kimada wake. kwa makubaliano akifanikisha atamuWOWWA!! huyu paul christian hakujua kama cheti chake kilichomolewa bila yeye kujua. hivi ndivyo ilivyokuwa. SASA!! wakuunganishwa hapo ni yuleee KIMADA wa bashitte ndie ataeleza zaidi ilikuwaje akakafikia hatua hiyo ya uchomozi/udakuzi/ukwapuaji ili amfurahishe bwana wake BASHITTE.
 
kumbe ndio maana watu tunashindwa kesi mahakamami shahidi anakuwa mtuhumiwa na mtuhumiwa snakuwa shahidi au yeye ndio amegushi ?isije ikawa tunaona mapicha picha tu
Hii ni kwa mujibu wa gazeti Mtanzania la leo May 18.

Nakumbuka huyu ndiye jina na vyeti vyake vinahusishwa na Mkuu wa mkoa mmoja hapa nchini.

Ngoja tuone maendeleo yake!

-----------
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora, inamsaka mwandishi na mtangazaji wa Redio Sauti ya Tabora (Voice of Tabora), Paul Pele Christian kwa siku kadhaa sasa bila mafanikio.

Habari za uhakika ambazo MTANZANIA imezipata mjini hapa, zinasema amekuwa akisakwa na maofisa wa taasisi hiyo kwa mahojiano kuhusu kashfa inayomuhusisha na sakata la vyeti vya elimu anavyodaiwa kuvitumia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kujiendeleza kielimu.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tabora, Fidelis Kalungula, aliliambia MTANZANIA kuwa wanamtafua Christian kwa siku kadhaa sasa, lakini hawajafanikiwa kumpata.

“Kweli tunamtafuta kwa mahojiano, hatujafanikiwa kuonana naye,” alisema Kalungula bila kufafanua zaidi.

Akizungumza kwa simu na MTANZANIA, Christian alikiri kupigiwa simu na maofisa wa taasiisi hiyo wakimtaka afike ofisini kwao kwa mahojiano.

“Nimepigiwa simu na maofisa wa Takukuru nifike ofisini kwao, leo (jana) ni siku ya nne sijatokea,” alisema.

Christian alisema kila anapohitajika amekuwa akibanwa na majukumu mengi ya kazi zake, hivyo kushindwa kuwajibu lolote akihofia kuwapotezea muda wao.

Alisema hii si mara ya kwanza kuhojiwa na maofisa wa taasisi hiyo, kwani walishafanya hivyo mara mbili.

Christian alisema mara ya kwanza ilikuwa Aprili 15, mwaka huu alipopigiwa simu na Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tabora, akidai ana mazungumzo naye.
Alisema baada ya wito huo, alifika ofisi za Takukuru saa 8:20 mchana.


“Katika mazungumzo yetu, walitaka kujua historia niliposemea kuanzia elimu ya msingi, sekondari, chuo na namfahamu vipi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,” alisema.

Alisema mara ya pili alihojiwa tena Mei 10, mwaka huu saa 5 asubuhi kwa muda wa saa tatu.

“Mbali ya mahojiano na maofisa hao, niliwakabidhi nakala za vyeti vyangu vya elimu ya sekondari,” alisema.

Pia alisema Mei 15, mwaka huu, alipata taarifa ya kutafutwa tena na taasisi hiyo kwa mahojiano kupitia kwa mkurugenzi wake wa Voice of Tabora, Ismail Aden Rage.

Christian alisema kuwa anashangazwa na hatua ya kutafutwa mara kwa mara, japo mhusika wa suala hilo yuko Dar es Salaam.


Chanzo: Mtanzania
 
11cdfa3508f7f4560884e895d832dc93.jpg

Unganisheni dot hapo, kwanini tukio la kutafutwa huyo Paul Christian linaenda sambamba na hilo la bashite kuongelea mambo yake yanayosemwa kupitia Star TV?
 
Ni sahihi kabisa. TAKUKURU majukumu yao ni mapana sana mkuu. Hapo huyo Paul Christian anatafutwa kwa kuingia kwenye vitendo vya rushwa, kumuuzia mtu mwingine vyeti vyake vitumike kinyume na ilivyokusudiwa kuwa ni mali yake tu na si vinginevyo.

Mtu akipatikana anatumia vyeti au cheti kisicho chake, wewe uliyempa ni lazima uingie kwenye tuhuma za kuhusika na suala hilo, na linakua katika sura ya RUSHWA.
Tuhuma hizo sio mpya, kwanini hawakumtafuta baada ya tuhuma kutolewa? kuna jambo gani jipya wamegundua ambalo hawakuweza kuliona tangu tuhuma za udanganyifu wa taaluma kwaa bashite?
 
Mmmmnnhhh....mbona huko mawizarani wakikuta cheti kinatumiwa na mtu zaidi ya mmoja hawawaiti takukuru...???!!! na kuna case nyingi tu ...wanawaambia wahusika walete original...ambaye si chake anaingia mtini...wala hakuna anayemtafuta awape story alikipataje...na mmiliki halali kuulizwa kilifikaje kwa x....


Kwa ufupi ni ngumu kumkamata owner hata kama kakiuza...atasema sijui...
Kuna njia nyingi za mtu kupata copy ya cheti cha mtu...anaweza hata waomba masijala wampe copy ya cheti chochote...kukana ni very easy...

Au unaenda mahali kutoa photo copy wao wanatoa extra...ngumu kumkamata true owner...
Hao watakuwa wamepewa maagizo tu ili wajaribu kumsafisha bashite. Kama wangekuwa na nia ya dhati kushughulikia sakata hilo wangeanza na bashite, atoe vyeti vyake na kisha Paul Christian atoe vyake halafu utata ukamalizwe NECTA na baada ya hapo ndio wachunguze rushwa.
 
Back
Top Bottom