TAKUKURU Tabora yamsaka Paul Christian kuhusiana na tuhuma za cheti feki

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
Hii ni kwa mujibu wa gazeti Mtanzania la leo May 18.

Nakumbuka huyu ndiye jina na vyeti vyake vinahusishwa na Mkuu wa mkoa mmoja hapa nchini.

Ngoja tuone maendeleo yake!

-----------
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora, inamsaka mwandishi na mtangazaji wa Redio Sauti ya Tabora (Voice of Tabora), Paul Pele Christian kwa siku kadhaa sasa bila mafanikio.

Habari za uhakika ambazo MTANZANIA imezipata mjini hapa, zinasema amekuwa akisakwa na maofisa wa taasisi hiyo kwa mahojiano kuhusu kashfa inayomuhusisha na sakata la vyeti vya elimu anavyodaiwa kuvitumia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kujiendeleza kielimu.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tabora, Fidelis Kalungula, aliliambia MTANZANIA kuwa wanamtafua Christian kwa siku kadhaa sasa, lakini hawajafanikiwa kumpata.

“Kweli tunamtafuta kwa mahojiano, hatujafanikiwa kuonana naye,” alisema Kalungula bila kufafanua zaidi.

Akizungumza kwa simu na MTANZANIA, Christian alikiri kupigiwa simu na maofisa wa taasiisi hiyo wakimtaka afike ofisini kwao kwa mahojiano.

“Nimepigiwa simu na maofisa wa Takukuru nifike ofisini kwao, leo (jana) ni siku ya nne sijatokea,” alisema.

Christian alisema kila anapohitajika amekuwa akibanwa na majukumu mengi ya kazi zake, hivyo kushindwa kuwajibu lolote akihofia kuwapotezea muda wao.

Alisema hii si mara ya kwanza kuhojiwa na maofisa wa taasisi hiyo, kwani walishafanya hivyo mara mbili.

Christian alisema mara ya kwanza ilikuwa Aprili 15, mwaka huu alipopigiwa simu na Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Tabora, akidai ana mazungumzo naye.
Alisema baada ya wito huo, alifika ofisi za Takukuru saa 8:20 mchana.

“Katika mazungumzo yetu, walitaka kujua historia niliposemea kuanzia elimu ya msingi, sekondari, chuo na namfahamu vipi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,” alisema.

Alisema mara ya pili alihojiwa tena Mei 10, mwaka huu saa 5 asubuhi kwa muda wa saa tatu.

“Mbali ya mahojiano na maofisa hao, niliwakabidhi nakala za vyeti vyangu vya elimu ya sekondari,” alisema.

Pia alisema Mei 15, mwaka huu, alipata taarifa ya kutafutwa tena na taasisi hiyo kwa mahojiano kupitia kwa mkurugenzi wake wa Voice of Tabora, Ismail Aden Rage.

Christian alisema kuwa anashangazwa na hatua ya kutafutwa mara kwa mara, japo mhusika wa suala hilo yuko Dar es Salaam.

Chanzo: Mtanzania
 
naona Director General wa hiyo taasisi anataka kugusa kabuli lililommeza Mh wa jimbo la Mtama!huyo bwana ndiye mwana kipenz cha baba hivo poga ua huyo atapeta tuu hadi baba yake asepe madalakani, just imagine ishu ya clouds jinsi mwigulu na wazir wa ulinzi walivokaa kimya mwishowe tukaambiwa wizaran kwao sio kila tukio ni habar kaul ambayo sikuilewa na simlaumu yy coz maybe alitumia lugha ya kisomi sana so ni kosa langu mm kukimbia shule na kwenda kugema ulanzi...ajifunze pia kwa yule boss wa FBI yan katika kazi sometimes katika kazi sio tuu ufate misingi ya kaz ila kuna mda lazma ujue nn boss anataka ufanye na nn hataki ufanye

NB:Jamaa wanaweza kuwa wanataka kucheza na akil za wabongo,inawezakuwa washatengeneza mpango wa kumsafisha yule dogo wa kujiita mbabe wa vita/BASHITE
 
naona Director General wa hiyo taasisi anataka kugusa kabuli lililommeza Mh wa jimbo la Mtama!huyo bwana ndiye mwana kipenz cha baba hivo poga ua huyo atapeta tuu hadi baba yake asepe madalakani, just imagine ishu ya clouds jinsi mwigulu na wazir wa ulinzi walivokaa kimya mwishowe tukaambiwa wizaran kwao sio kila tukio ni habar kaul ambayo sikuilewa na simlaumu yy coz maybe alitumia lugha ya kisomi sana so ni kosa langu mm kukimbia shule na kwenda kugema ulanzi...
Usikute anamsaka yule Paul ambaye ni mtangazaji
 
TAKUKURU tena na vyeti? au me ndio mjinga sielewi
Ni sahihi kabisa. TAKUKURU majukumu yao ni mapana sana mkuu. Hapo huyo Paul Christian anatafutwa kwa kuingia kwenye vitendo vya rushwa, kumuuzia mtu mwingine vyeti vyake vitumike kinyume na ilivyokusudiwa kuwa ni mali yake tu na si vinginevyo.

Mtu akipatikana anatumia vyeti au cheti kisicho chake, wewe uliyempa ni lazima uingie kwenye tuhuma za kuhusika na suala hilo, na linakua katika sura ya RUSHWA.
 
Kwa hiyo mwenye cheti halali ndiye kafoji na aliyefoji ndiye halali ?! Ngoja tuone
Hapana mkuu, huyo Paul Christian anaingia katika sakata hilo kwa kushirikiana na mtuhumiwa kupeana vyeti au cheti. Mtu akipatikana anatumia cheti au vyeti vyako, yeye ataingia kwenye hatia na wewe pia mwenye vyeti utaingia kwenye hatia. Jinsi ilivyo inaonekana inakua treated kama RUSHWA.
 
Ni sahihi kabisa. TAKUKURU majukumu yao ni mapana sana mkuu. Hapo huyo Paul Christian anatafutwa kwa kuingia kwenye vitendo vya rushwa, kumuuzia mtu mwingine vyeti vyake vitumike kinyume na ilivyokusudiwa kuwa ni mali yake tu na si vinginevyo.

Mtu akipatikana anatumia vyeti au cheti kisicho chake, wewe uliyempa ni lazima uingie kwenye tuhuma za kuhusika na suala hilo, na linakua katika sura ya RUSHWA.
Sasa kwa sheria ninachojua, mtoa na mpojea rushwa wote wana hatia. Sasa kuna juhudi zozote zilizofanywa ili mtoa rushwa (aliyenunua) nae atiwe hatiani?
 
Kumbe huwa tunaanza na aliyepokea rushwa kwanza halafu mwishoni tunarudi kwa aliyetoa?
Aiseee haya maajabu hapo
 
Sasa kwa sheria ninachojua, mtoa na mpojea rushwa wote wana hatia. Sasa kuna juhudi zozote zilizofanywa ili mtoa rushwa (aliyenunua) nae atiwe hatiani?
Mkuu kila kazi zina taratibu zake. Watakapompata mwenye vyeti mhusika halisi wa vyeti, yeye ndiye atawasaidia kumhoji huyo mtuhumiwa, ikiwa kuna u serious katika hili. Let's wait and see, but the move is ok.
 
Ni sahihi kabisa. TAKUKURU majukumu yao ni mapana sana mkuu. Hapo huyo Paul Christian anatafutwa kwa kuingia kwenye vitendo vya rushwa, kumuuzia mtu mwingine vyeti vyake vitumike kinyume na ilivyokusudiwa kuwa ni mali yake tu na si vinginevyo.

Mtu akipatikana anatumia vyeti au cheti kisicho chake, wewe uliyempa ni lazima uingie kwenye tuhuma za kuhusika na suala hilo, na linakua katika sura ya RUSHWA.
So aliyepokea rushwa si Mhalifu?
 
Back
Top Bottom