Takukuru nini tatizo kila siku mnashindwa?

babalao 2

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
5,398
3,243
vipi jamani hivi vitengo vyetu vya takukuru na usalama wataifa kushindwa kunusa harufu ya uhalifu ktk wizara zetu? kazi zao mbona ni kama hawapo na umuhimu wao haupo tena. mbona mkaguzi wa mahesabu amedhubutu na ameweza hawa wanashindwa nini au wajiuzulu pamoja na mawaziri? wanatuboa hawa
 
TAKUKURU wanafanya mambo yao kimyakimya. hata kesi ya mramba liyumba na nyingine za BOT watu walidhani takukuru imelala kumbe wanakamilisha uchunguzi.
 
Hakuna lolote!
Baada ya kutajwa Bungeni kama moja ya taasisi dhaifu zinazotakiwa kubadilisha uongozi, ndo sasa wanajifanya kufufua kesi walizoziacha siku nyingi.

Kwani Hosea wao siku hizi ameacha tabia ya kuwalazimisha wenye kesi kukodisha ofisi yake ya uanasheria? Ukiwa na kesi ya ya mabilioni wewe kodisha kampuni yake tu, na kesi itakwisha kwa usalama.
 
hao takukuru nao ni binadamu kama wengine na wana mahitaji yao...wanaweza wakawa wanapigwa hela na wao vile vile...mjini hapa:dizzy:
 
TAKUKURU wanafanya mambo yao kimyakimya. hata kesi ya mramba liyumba na nyingine za BOT watu walidhani takukuru imelala kumbe wanakamilisha uchunguzi.
I see!!.....kwahiyo tuvute subira hata kwa waliokula pesa za rada ya ulanguzi akiwamo Andrew Chenge kama Mwanasheria mkuu!!
 
TAKUKURU kweli hamna kitu bado mpaka leo hii sijaelewa shida ni nini mpaka idara hii imezorota kiasi hiki!!!!
 
Takukuru is an organazation of looters. Kazi ya Wapumbavu Tukukuru ni kuwasafisha Mafisadi na kuwarudisha tena kwenye jamii ili wakubalike tena, kitu ambacho hakiwezekani. Kuwalinda Mafisadi kwa gharama yoyote ile, kuhakikisha Mafisadi hawapelekwi jela. Tukukuru kwangu mimi ni sawa na Kitengo cha Majambazi kinacholindwa na Mafisadi kwa Maslai yao.

Cooooooome 2015 niwaadabishe mafisadi
 
vipi jamani hivi vitengo vyetu vya takukuru na usalama wataifa kushindwa kunusa harufu ya uhalifu ktk wizara zetu? kazi zao mbona ni kama hawapo na umuhimu wao haupo tena. mbona mkaguzi wa mahesabu amedhubutu na ameweza hawa wanashindwa nini au wajiuzulu pamoja na mawaziri? wanatuboa hawa

As long as Hosea Edward atendelea kuwa kiongozi wa Taasisi hiyo just forget. Alitakiwa aondoke na akina Msabaha na EL lakini amebaki hata akina Mwanyika walistaafu yeye anwalinda walaji wa Rushwa yeye na Mpwawe DPP ? Usalama aw Taifa chini ya Othman mponda raja aw Uingereza aliyeteuliwa na Rostam Aziz is another time bomb. Huwezi ukata na walaji Rushwa Kama Manumba na boss wake Said Mwema mambo yakenda. Hivi waulizeni hao wameshaacha kulipwa pesa za kujikimu na Yusuf Manji au bado wanendelea. Bila mapinduzi kubadilisha Mawaziri is just cosmetics ni Mkorogo. JK na CCM wamenasa hata ukija na Bulldozer huwakwamui wataozea walipo.
 
Takukuru is an organazation of looters. Kazi ya Wapumbavu Tukukuru ni kuwasafisha Mafisadi na kuwarudisha tena kwenye jamii ili wakubalike tena, kitu ambacho hakiwezekani. Kuwalinda Mafisadi kwa gharama yoyote ile, kuhakikisha Mafisadi hawapelekwi jela. Tukukuru kwangu mimi ni sawa na Kitengo cha Majambazi kinacholindwa na Mafisadi kwa Maslai yao.

Cooooooome 2015 niwaadabishe mafisadi
Mzalendo hapo umejitoa mhanga sasa hawa wa usalama wa taifa kazi yao ni nini maana nyara za serikali zinaibiwa mchana kweupe wao ishu zao ni zipi ina maana kwetu hatuna vitengo vya kijasusi kama kwa wenzetu? tujuzeni wajamen
 
Bosi wake,Dakta Hoseah alikwishaweka wazi sababu kuu katika mahojiano-yaliyovujishwa katika mtandao wa leakleaks- kati yake na balozi moja wa dunia ya kwanza!!...kuwa mtawala wa juu kabisa hapa nchini ndio kikwazo cha taasisi hiyo kutekeleza majukumu yake.
 
Mnawaonea wivu Tiss na Takukuru c muombe ajira nanyi muajiriwe wivu tu tena wa kike wakijinga!
 
Shida kubwa ya idara nyingi za serikali ya Tz ni kuwa, wafanyakazi wengi wanatekeleza wajibu wao kwa kufuata mazoea yao badala ya kufuata utaratibu. Hili la Takukuru kutowajibika kikamilifu ni kilio cha watz wengi!!!!!!! Na kwa hali tunayokuwa nayo sioni kama wataweza kujirekebisha bila huu mfumo kubadilika kwanza!
 
hii inaitaitwa TAasisi ya KUkuza na KUpamba RUshwa. Wanafanya kazi waliyotumwa,sasa kwanini tunawalaumu?

rushwa ni kama ngono. hufanywa kwa siri. watu wakikubaliana hasa kwenye rushwa kubwakubwa kupata ushahidi wa kusimama mahakamani ni kazi kweli kweli
 
Wana JF hivi TAKUKURU wameshashinda kesi ngazi kubwa na muhimu? Nimeona mara nyingi sana huwa wanashindwa kesi zao.

vipi jamani hivi vitengo vyetu vya takukuru na usalama wataifa kushindwa kunusa harufu ya uhalifu ktk wizara zetu? kazi zao mbona ni kama hawapo na umuhimu wao haupo tena. mbona mkaguzi wa mahesabu amedhubutu na ameweza hawa wanashindwa nini au wajiuzulu pamoja na mawaziri? wanatuboa hawa
 
Hakuna lolote!
Baada ya kutajwa Bungeni kama moja ya taasisi dhaifu zinazotakiwa kubadilisha uongozi, ndo sasa wanajifanya kufufua kesi walizoziacha siku nyingi.

Kwani Hosea wao siku hizi ameacha tabia ya kuwalazimisha wenye kesi kukodisha ofisi yake ya uanasheria? Ukiwa na kesi ya ya mabilioni wewe kodisha kampuni yake tu, na kesi itakwisha kwa usalama.
Eee bana eh kumbe,nina ki EPA changu kiko jikoni kitaiva muda si mrefu,sasa sina wasiwasi ngoja nikipakue,halafu likibumburuka nitaenda kwenye kampuni ya uwakili ya mheshimiwa sana Hosea.
 
Wana JF hivi TAKUKURU wameshashinda kesi ngazi kubwa na muhimu? Nimeona mara nyingi sana huwa wanashindwa kesi zao.

Naomba nikuweke sawa, na nipo tayari kurekebishwa. Kwanza, kazi ya uendeshaji wa mashtaka si kazi ya Takukuru, ni kazi ya Dpp. Na ndo maana ktk kesi zote kubwa, waendesha mashtaka hutoka kwa Dpp. Kazi ya Takukuru ni uchunguzi tu ukiachia mbali utafiti na uelimishaji. Ingawa unaweza kuona PP's wa Takukuru wakiwa mahakamani, pale wanafanya kazi ya dpp. Hivyo, kisheria anayeshinda/kushindwa kesi ni dpp. PILI, kazi ya PP's huwa inaishia ktk Ruling, si ktk judgment(Huu ni msimamo wa Jurists wengi. Iwapo PP's atafanikiwa kuishawishi mahakama imuone mshtakiwa ana kosa la kujibu huo ni ushindi wa PP's. Baada ya ruling, hapo sasa ni kazi ya defence na hatimae hakimu. Wanasheria na hasa wataalam wa jurisprudence, tujadili hapa. Na kama kukosolewa, nipo tayari.
 
Mnawaonea wivu Tiss na Takukuru c muombe ajira nanyi muajiriwe wivu tu tena wa kike wakijinga!

Pole wewe mwenye wivu na maendeleo ya watanzania watu kama nyinyi mnastahili mtubu mpate busara.Hao PCCB/TISS wanakula kodi ya kikwete au ya watanzania?
 
Back
Top Bottom