TAKUKURU, kuna kesi moja yenye ushahidi CHADEMA

Tuhuma za rushwa Bavicha zipelekwe TAKUKURU-Zitto



Na Tumaini Makene

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Kabwe Zitto ametoa pongezi kwa Mwenyekiti mpya wa Baraza la Vijana (BAVICHA), huku
akisema kuwa atamwandikia barua katibu mkuu wake, kushauri tuhuma za kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa juzi, zipelekwe mbele kwa hatua zaidi.

Akizungumza na Majira jana, Bw. Zitto alisema kuwa leo atawasilisha barua hiyo kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa, kumwomba tuhuma za rushwa zifikishwe katika Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ili zifanyiwe uchunguzi, kisha hatua za kisheria zichukuliwe kwa watakaobainika.

"Nafikiri nitaiwasilisha kesho hiyo barua, nitamwomba katibu mkuu hizi tuhuma zifikishwe PCCB, nafikiri hiyo itakuwa ni hatua bora zaidi, PCCB wachunguze watakaobainika na makosa wachukuliwe hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa watu wengine wote wanaojihusisha na vitendo vya namna hiyo ndani ya chama.

"Nitatumia nafasi yangu ya Naibu Katibu Mkuu. Kwa sababu tusipofanya hivyo itaweza kujenga hisia za kuwa walioondolewa katika uchaguzi huo kwa tuhuma za rushwa wameonewa. Italeta hisia za upendeleo...kwa sababu mwenye haki ya ku-determine rushwa ni mahakama hivyo ni bora wachukuliwe hatua zaidi," alisema Bw. Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.

Akizungumzia ushindi wa Mwenyekiti wa BAVICHA, Bw. John Heche, alisema kuwa changamoto kubwa aliyonayo ni kuwaunganisha vijana wote na kuwa kiongozi wao, wakiwemo wale waliokuwa washindani wake na watu waliokuwa nyuma yao wakiwasapoti.

"Nampongeza sana Heche, kwa ushindi wake alioupata. Sasa hivi ni wakati wa kukijenga chama, uchaguzi umeisha si wakati wa kulalama tena...vijana wanamtegemea atakuwa mwenyekiti wao, mimi nafikiri moja ya changamoto zake kubwa ni pamoja na kuwaunganisha vijana, wote hata walioenguliwa," alisema Bw. Zitto.

Juzi akizungumza na Majira juu ya uchaguzi wa BAVICHA uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Slaa alisema kuwa vitendo vyote vilivyo kinyume na maadili ya kampeni kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha katiba ya chama hicho, pamoja na waliohusika, vitajadiliwa katika ngazi ya Kamati Kuu kwa maamuzi zaidi.

Alisema kuwa baadhi ya wagombea, hasa walioenguliwa, walibainika kwenda kinyume na maadili ya chama hicho, hasa katika kupiga vita ufisadi wa aina yoyote kama vile kufanya hila katika uchaguzi, kujenga makundi yenye kuhatarisha chama na kutaka kuvuruga uchaguzi.
 
Code:
"Nitatumia nafasi yangu ya Naibu Katibu Mkuu. Kwa sababu tusipofanya hivyo itaweza kujenga hisia za kuwa walioondolewa katika uchaguzi huo kwa tuhuma za rushwa wameonewa. Italeta hisia za upendeleo...kwa sababu mwenye haki ya ku-determine rushwa ni mahakama hivyo ni bora wachukuliwe hatua zaidi," alisema Bw. Zitto, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini.
Cha msingi jambo hilo liwe concurred na vikao husika na si mtu binafsi kusimamia na kuonekana yeye ndio anajua zaidi demokrasia!
Actually likikubalika litaonyesha kiasi fulani cha transparency na kufuta manung'uniko.
 
kwanini Takukuru inaogopwa? Tuhuma ziende kule. Hawa waliotuhumiwa hawawezi kuwa safi katika maisha yao km wataishi na tuhuma. Tuwafikirie na wao pia. Namna njema kwa CDM pia ni kuonyesha wanacho kisema kipo ndani ya sheria.
 
Back
Top Bottom