TAKUKURU kuchunguza mila za Kichaga

TAKUKURU kuchunguza mila za Kichaga

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
9,144
Reaction score
19,690
Takukuru kuchunguza mila za kichaga
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imeanza kuchunguza utaratibu wa familia za kabila la Kichaga kutumia majani maarufu kama ‘sale’ kufunika au kumaliza kienyeji kesi zinazohusu ukatili wa kijinsia na mimba za wanafunzi.

E86A1658.JPG


Majani hayo ya masale kwa mila na tamaduni za kabila la Wachaga, hutumika kuashiria amani, kuomba msamaha na kumaliza tofauti zao.


Ofisa wa Takukuru Wilaya ya Hai, Denis Mazigo, alifichua siri hiyo ya kuanza kwa uchunguzi dhidi ya mila hiyo wakati wa uwasilishaji ripoti ya kamati ya ulinzi wa mtoto.


“Haliwezi kutangulizwa jani la sale peke yake, lazima kuna mazingira ya kutolewa kwa fedha kama rushwa, ndiyo msamaha uweze kukubalika. Sasa sisi kama Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa tumeanza kufanyia kazi jambo hili, kwa sababu tumeona kesi nyingi za ukatili zikikwama huku zikiwa na ushahidi wa kutosha,” alisema Mazigo.


Chanzo: Nipashe
 
Yaani MTU anatia mimba mwanafunzi halafu unaenda na hilo jani kuyamaliza .hiyo ni hongo ya wazi wazi ambapo majaji wanahongwa majani hayo
Wamasai wanachinja mbuzi wanakula pamoja na kesi inaishia hapo! Wakurya wanaongea tu kikubwa wanapeana pombe na chakula kesi inaisha ila kwa vile our very target ni Wachagga there we go!! Kwa nini tu serikali isilipige marufuku hilo kabila?? Au serikali itangaze tu sisi tutawashughulikia! Mbona Myanmar wameweza kuwatokomeza warohingya? Kwa nini sisi tushindwe?
 
Hii taasisi itakuwa imekosa kazi za msingi za kufanya na kuunza kufuatilia mambo ya kipuuzi.
Mambo ya kimkakati wewe unayaita ya kipuuzi?? We hujui tu wachagga walivyoustawisha upinzani tanzania!
 
Back
Top Bottom