TAKUKURU: Askofu na Viongozi Wakuu wa Kanisa la Avengelical assembless of God (EAGT) wachungunzwa kwa rushwa

Chabusalu:
Tatizo ni la kiuongozi na kukosa transparency.
1. Katika mikutano mikuu yote ndiko ambapo maswali na hoja zozote hujibiwa. Jambo hilo halifanyiki. Mara nyingi ikitokea hoja yoyote ambayo inagusa uongozi haijibiwi na unaamulishwa kukaa chini.
2. Kuhusu magari tupeane mawasiliano njoo nikuonyeshe ushahidi.
3. Taasisi yoyote huwa ina TIN namba moja njoo nikuonyeshe Tin namba 5 za dhehebu hili ambazo zimetumika.
4. Kuhusu majengo tangu yamenunuliwa na kukodishwa hakuna taarifa yoyote ya mapato wala matumizi. Na mengine mengi.
Kwa taarifa yako siongei hadithi ya kusimuliwa, mimi ninajua nina chokisema
Ndo maana nimekwambia kama kweli unataka ukweli na ushahidi wa jambo hili nitafute.
Mkuu mwaga hapa tupate faida wote, kuficha ficha tunazid kuliangamiza kanisa hili ambalo msingi wake mkubwa ni kueneza injili, ndo maana kuna idara kama CGM, WWI n.k. Muda wa kuficha ficha sio sasa.
 
Tunawaomba TAKUKURU waje na huku Roman Catholic. Waje Takukuru kuchunguza RC maana sio kwa michango na sadaka kwa lazima. Kila kigango au parokia mnatakiwa kuchangia kiasi fulani nk. Siku hz watu wengine hatuendi kanisani kwa sababu ya michango na sadaka...

Jamani situlikubaliana mnamchangia Mungu na kanisani mnaenda kumuabudu imekuaje tena
 
Mkuu
Makamu askofu Mkuu Mahene yeye ndiye alikuwa wa kwanza kuibua hoja ya ubadhilifu. Katika kuhoji mambo kadhaa akazuliwa kuwa yeye ni mnzinzi hivyo afukunzwe na Mwakipesile akafanya hivyo.
1. Tulimwuliza Mwakipesile adhibitishe tuhuma hizo akadai kuwa kuna nabii ameonyeshwa na Mungu. Na siyo tu kuonyeshwa na Mungu nabii huyo akadai kuwa amemrekodi Mungu wakati akisisitiza kuwa Mahene hafai kuwa makamu. Katika minutes alizo andika katibu mkuu Mwizarubi ameandika hivyo. ( ushahidi ninao wa minutes hizo).
2. Kuhusu issue ya ukabila, dhehebu hilo limekuwa kama makabila mawili ndo yenye hati miliki (i) Wasukuma ( ¡¡) Wanyakyusa, Tangia mwanzo. Nguvu ya wazee wa kinyakyusa ilianza kutokana na mchango mkubwa waliokuwa nao kwa Askofu Kulola hasa wakati wa mgogoro wa kwanza.
1.Askofu M.Kulola- msukuma
Makamu M.Mwamwenda- nyakyusa
Katibu: Ngobito - mgogo.
2. Awamu nyingine:
Askofu M.Kulola - sukuma
Makamu M. Mwamwenda
Katibu M.Mhina- Tanga
M/Hazina E. Andrew- Msukuma.
3.Awamu nyingine tena:
Askofu M Kulola- sukuma
MakamuA. Mwaisabila- nyakyusa
Katibu B. Mwakipesile- nyakyusa
Unaweza kupata picha ya uongozi huo.
Kwenye uongozi huu wa mwisho
4.Askofu B. Mwakipesile- Nyakyusa
Makamu J.Mahene- Sukuma
Katibu L.Mwizarubi- kerewe.
Hivyo ukiacha awamu tatu za mwanzo hii ya nne imepunguza ukabila kwa sehemu.
Hivyo tukizungumzia ukabila upoupo lakini issue ilikuwa baada ya kuhoji ubadhilifu ambao umefanyika wakati wote askofu Mwakipesile akiwa ni kiongozi wajuu. Inasemekana ili kukata mzizi wa fitina askofu alicante mbinu za kumwengua/ kutemwa makamu wake kama ulivyo sema, jambo hilo lilipingwa na mahakama ilitengua maamuzi hayo.
Hii ni stori ndefu:
Lakini kwa kifupi, Mgogoro huu ni wa kiuongozi na mbinu za kuficha baadhi ya matendo hasa yale yasiyo na maadili.
Watu wenye mapenzi mema walishauri uongozi wote ukae pembeni na tupate viongozi wa muda walinusuru dhehebu lakini always ukubwa ni mtamu.
Nimejitahidi kueleza kwa kirefu ili kwa wale wasiojua angalau wawe na mwanga.
Mkuu upo sahihi, lete vitu, na inasemekana Wanyakyusa wameungana na wengine wamemchagua askofu wao, so Kwasasa EAGT lina maaskofu wawili, hebu eleza kiungaubaga Mwakipesile alikuwa katibu mkuu wa mzee Kulola, je Kulola hakuona udhaifu huu unaousema hadi amuache kuwa katibu wake??
 
Usilolijua ni kama usiku wa giza. Hadi sasa hakuna mali yoyote ya TAG iliyoporwa ndugu zangu tusiwe tunasikiliza propaganda za watu, hadi sasa ni viwanja na makanisa yaliyo jengwa na wamissionary wa Assemblie of God toka Springfield Missouri USA ambazo zilibakia kwa kanisa la mahali pamoja.
Hivyo propaganda za kuporwa nadhani huo ni upotovu na uzushi. Tuepuke kusema tusilolijua.
Vipi kuhusu kile kiwanja cha kanisa la EAGT pale Temeke? Kesi si ipo mahakaman na tetesi zinasema TAG wanaenda kuwin, ipoje hii?
 
Kulola alijua kuwanyonya wote. Toka afe kila mmoja anataka ALE keki. Kulola alikula peke yake na akajua kuwatawala kisawa sawa.
Acha kufuru, Kulola amekula nini? Maneno mengine kwa watumishi wa Mungu yatasababishwa upigwe laana tu, Kulola amekufa akiwa maskin wa kutupwa we unasema amekula, mzee alikuwa buzy na injili, ndo maana ombwe la uongozi limebaki kuwa tatizo EAGT kwasababu mzee aliamin kt injili. Ukisema mzee Kulola alikula mali za kanisa sio kweli.
 
Haya
VIONGOZI WAKUU WA KANISA LA EVANGELICAL ASSEMBLESS OF GOD OF TANZANIA [E.A.G.T] AKIWEMO ASKOFU MKUU WACHUNGUZWA KWA RUSHWA

Ndugu WanaHabari,

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU – Brig Jen. John Mbungo, napenda kuujulisha Umma kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU – Makao Makuu, inafanyia uchunguzi malalamiko dhidi ya Viongozi Wakuu wa Kanisa la EVANGELICAL ASSEMBLESS OF GOD OF TANZANIA (E. A.G.T) nchini.

Bila shaka baadhi yenu mlisikia na kuona malalamiko ya baadhi ya wachungaji wa kanisa la EAGT ambao waliyatoa siyo tu kwenye vyombo vya habari lakini pia katika ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU.

Wachungaji hao, ambao kwa ujumla wao ni zaidi ya 540, kwa pamoja wanalalamikia vitendo vya Rushwa, Ufisadi pamoja na wizi ndani ya kanisa yakiwemo mambo yafuatayo;
  1. Uingizwaji wa vyombo vya moto yakiwemo magari zaidi ya 50 na pikipiki kwa jina la Kanisa la EAGT, vyombo ambavyo inadaiwa viliingizwa nchini kwa kupitia jina la kanisa na kupata msamaha wa kodi lakini vyombo hivyo vya moto - kanisa halivitambui na wala halijawahi kuvipokea.
  2. Lalamiko jingine ni ubadhirifu wa fedha na mali ya kanisa unaodaiwa kufanywa na viongozi wa kanisa hilo kuhusiana na mkataba ulioingiwa kati ya kanisa la EAGT na wapangaji wa Duka la IMALASEKO SUPERMARKET INVESTMENT kwani inadaiwa mapato yanayotokana na majengo hayo hayajawekwa wazi hivyo kuashiria kuwepo kwa ubadhirifu.
  3. Ubadhirifu wa fedha za kanisa kwenye ununuzi wa shule iitwayo OASIS EDUCATION AND COMMUNITY DEVELOPMENT iliyopo Kahama.
  4. Kuwepo kwa TIN tofauti zaidi ya tano zilizosajiliwa kwa jina la Kanisa la EAGT na TIN hizo kutumika kuingiza magari kwa jina la kanisa na kusamehewa kulipa ushuru wa Forodha wakati magari hayo hayajanunuliwa na kanisa.
  5. Taarifa za mapato na matumizi ya kanisa kutokuwekwa wazi wala Kanisa halina Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.
  6. Uingiaji wa mikataba mibovu na isiyo wazi inayoikosesha Serikali mapato yake halali.

Ndugu WanaHabari,

Kupitia taarifa hii tunapenda umma ufahamu kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Makao Makuu ilishaanza kufanyia uchunguzi malalamiko haya ambayo baadhi ya tuhuma zinaangukia chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 na kwamba mpaka sasa yafuatayo yameshafanyika:
  • Tumeshafanya mahojiano na baadhi ya walalamikaji,
  • Tumekusanya baadhi ya vielelezo na
  • Tunaendela kuwaita na kuwahoji walalamikiwa na leo hii Februari 16, 2021 tumemhoji Askofu Mkuu wa Kanisa hilo – Askofu ABEL MWAKIPESILE.
Ndugu WanaHabari,

Lengo la uchunguzi wetu huu pamoja na mambo mengine ni kutaka kufahamu ukweli wa malalamiko haya ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
IMETOLEWA NA DOREEN J. KAPWANI
AFISA UHUSIANO WA TAKUKURU
KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
 
Wachungaji wengi wanaolalamika ni wa kanda ya ziwa, wasukuma.

Hao wachungaji ni wanafiki, mbona hawakusema toka zamani kuna ubadhirifu mkubwa kanisani hadi wagombane kwenye vyeo ndio waje kusema kuna TIN tano sijui ujinga gani, kama wao ni waadilifu na waaminifu mbona hawakusema mapema hilo hadi mgogoro wa uongozi utokee ndio walalamike?

Binafsi sio muumini wa dini yoyote maana najua Mungu hayupo ingawa nina historia ama najua historia pana ya makanisa na madhehebu mbalimbali hapa Tanzania.

EAGT ndio kwanza wamefugua milango ya migogoro, wanarudi kule kule kwa muasisi wao Kulola alipoanzisha mgogoro na TAG akahama kanisa na kung'ang'ania majengo ya TAG, wanaelekea kule kule.

Halafu TAKUKURU mbona waislamu wanailalamikia bakwata kila uchwao hatijawahi kusikia viongozi wa bakwata wamehojiwa?
Zamani ofisi zatakururu inawezekana hawakua na watumishi
 
Huko kwenye taasisi za dini sio kusafi sana. Sio hawa EAGT tu, bali hata haya makanisa "makubwa" pia. TAKUKURU wapeleke pua zao kote huko, wasiishie EAGT tu.
 
Hizo ni habari za kufikirika; kwamba yule Mnyakyusa anaweza kuhonga serikalini dhidi ya mwalimu? Hivi unajua Mahene (Mahene ndio man of this match, alitengwa na huyo Mnyakyusa kwasababu ya kupenda sana K za kina mama) ni mwalimu by proffesinal na kafundisha baadhi ya very senior gorvonrment officials? Unadhani rushwa ya huyo Mnyakyusa inaweza kua na nguvu hadi hao senior official waache kumsaidia mwalimu wao? Yote haya ya kuhonga anae yatengeneza ni ni huyo huyo Mahene baada ya kushindwa kuthibitisha kuhusu magari na KODI; by the way, mbona tena juzi hao maaskofu wanao unga mkono upande wa Mahene wamepoteana wenyewe kwa wenyewe? Wamejirekodi tena Youtube, ka search tu utaipata; NAkupa homework brother; katika wale wachungaji 540 wanao unga mkono Dr. Mahene, tafuta kama kuna walau wachungaji 20 ambao ni form four levers; ukiwapata walau 20 nitajie majina yao, ukishindwa pia just kua muungwana. Sisali kanisa lenu but hu mgogoro naufahamu vizuri sana. Mtu mzima tena mchungaji kuunga mkono upande wa UZINZI ni bora kuacha kabisa kwenda KANISANI, nawaonea huruma waumini wanao sali makanisa ya hao wachungaji 500+
Hilo la kuzaa linafahamika na alizaa kabla hata hajaingia kwenye huduma kisa uaskofu mkuu ndio huyo mnyakyusa akaamua kutumia kick ya kuzaa(uzinzi)ili kumchafua .Huyo mnyakyusa hakuna kiongozi wizara ya mambo ya ndani ya nchi kitengo cha usajili wa madhehebu ambaye hajala hela zake amehonga sana huyo mnyakyusa ni mchafu kupindukia hakuna asiyejua hilo
 
Wachungaji wengi wanaolalamika ni wa kanda ya ziwa, wasukuma.

Hao wachungaji ni wanafiki, mbona hawakusema toka zamani kuna ubadhirifu mkubwa kanisani hadi wagombane kwenye vyeo ndio waje kusema kuna TIN tano sijui ujinga gani, kama wao ni waadilifu na waaminifu mbona hawakusema mapema hilo hadi mgogoro wa uongozi utokee ndio walalamike?

Binafsi sio muumini wa dini yoyote maana najua Mungu hayupo ingawa nina historia ama najua historia pana ya makanisa na madhehebu mbalimbali hapa Tanzania.

EAGT ndio kwanza wamefugua milango ya migogoro, wanarudi kule kule kwa muasisi wao Kulola alipoanzisha mgogoro na TAG akahama kanisa na kung'ang'ania majengo ya TAG, wanaelekea kule kule.

Halafu TAKUKURU mbona waislamu wanailalamikia bakwata kila uchwao hatijawahi kusikia viongozi wa bakwata wamehojiwa?
Upo sahihi kabisa Mkuu.
 
Mkuu cool d nadhani sio busara kwa Serikali kuyafuta hayo makanisa bali inaweza kuleta utaratibu au mwongozo ambao Makanisa "Maslahi" yatajifuta yenyewe. Mfano Serikali inaweza kuyataka makanisa yote yawasilishe :

1. Bodi ya wadhamini wa kila kanisa AMBAYO haichaguliwi na Kiongozi mkuu wa Kanisa WALA haiwezi kuvunjwa na kiongozi mkuu wa Kanisa
2. Mtiririko wa Kimaamuzi ya kinidhamu pale kiongozi Mkuu wa kanisa au Wachungaji wengine wanapokengeuka (Backslide)
3. Account number za Kanisa zilizosajiliwa kwa majina ya Kanisa ambapo Watia saini watoke A : Wachungaji B: wadhamini

Hatua ndogo kama hizi zitaanza kuwaondoa viongozi Maslahi na pia hatua kama hizi zinaanza kuyageuza taratibu Makanisa ya kifamilia kuwa taasisi.

Naomba kukosolewa

Ahsante
Uko sawa kabisa, makanisa yaendeshwe kitaasisi na siyo kwa nguvu za familia na serikali inatakiwa kusimamia hilo Ili kuwalinda wenzetu wenye kuongozwa kwa akili za kushikiwa, inafika sehemu mama mjane au mstaafu anaambiwa apeleke hati ya nyumba au atoe hela zake zote za kustaafu Ili abarikiwe kwaajili ya mchungaji kijana aliyekimbia kazi za wahindi akaona hazilipi Sasa anajipatia kipato kwa njia hizo na serikali inaona tu kwa vile haijaweka Sheria za kuwabana hawa watu, nauhakika ikiwekwa misingi mizuri kanisani kuwa taasisi watalipwa kwa mshahara na kuhamishwa kwenda sehemu zingine bila kufanya mazoea na sehemu moja na vyeo vitapanda kwa vigezo na siyo kwa ujanja na hata kustaafu muda ukifika imagine hao watu Sasa hivi hata NSSF hawalipi kwaajili ya mafao ya uzeeni Kama makanisa taasisi tunayojua yalivyo na nidhamu zao tunaziona na vijana wanaandaliwa tunaona Sasa hawa mpaka uzeeni na wivu wao wanawaogopa kuandaa watu ndo maana niliwaza Bora yafutwe Ila ukatoa wazo zuri Sheria zikiwekwa kutengeneza taasisi yatajifuta yenyewe.
 
Acha kupotosha umma, waliompa tuzo ni Tanzania Assemblies of God (TAG). kwani wewe wakati ule wa Corona hukuona mchango mkubwa wa Rais Magufuli?. aliunganisha nchi kwa imani zote kufunga na kumuomba Mungu na kwakwel matokeo yalionekana. Maaskofu, Mapadre, Wachungaji, Masheikh, Mitume na Manabii hakuna aliyejitokeza hadharani kutangaza maombi kwa watanzania wote.

wivu tu, ndio alipewa tuzo kwa kutambua mchango wake wa kupambana na Corona. Na lazima ujue kuwa kama kweli unamjua Mungu na una hofu naye. katika kupigana vita unapigana Kimwili na kiroho pia na ushindi lazima upatikane. Rais alichagua kupigana kiroho.
hapo nimeuliza, sijasema.

Mnasoma shule gani ambazo hamfundishwi maana ya alama za kuuliza???

By the way tafuta pesa upeleke watoto kwenye shule nzuri ili wasiwe wazito kuelewa kama mama yao.
 
Hilo la kuzaa linafahamika na alizaa kabla hata hajaingia kwenye huduma kisa uaskofu mkuu ndio huyo mnyakyusa akaamua kutumia kick ya kuzaa(uzinzi)ili kumchafua .Huyo mnyakyusa hakuna kiongozi wizara ya mambo ya ndani ya nchi kitengo cha usajili wa madhehebu ambaye hajala hela zake amehonga sana huyo mnyakyusa ni mchafu kupindukia hakuna asiyejua hilo
Mkuu, jibu hili; Happiness ana umri wa miaka mingapi na mzee alianza lini kua mchungaji Bugando? Tunaongea kwa data. Kwani ile kesi pia aliofungua mahakama ya hakimu mkazi Mwanza iliishaje? Na by the way, wapi nimezungumzia habari ya mzee kuzaa nje ya ndoa? Si unaona unavyo jichanganya? Well, nimekupa homewhork pale juu, nitajie walau wachungaji 20 wanao muunga mkono Mahene ambao walau wana form four ya darasani; tatizo almost wote pale hawana shule kabisa,darasa la saba na wengine darasa la nne na wengine hawaujui mlango wa darasa and hence ufahamu wao wa kawaida tu hawana kabisa; kwa taarifa yako, nimefanya mazungumzo na baadhi yao; wanadhani mtu akienda kushtaki tu hua wanajua tayari kashinda kesi, very stupid ideas kwa watu wanachunga makanisa kua na ufahamu mdogo kiasi hicho.
Ukiendelea kubisha ntakwambia hata aliyemfahamisha huyo Mnyakyusa habari za Mahene kua na nyumba ndogo alikua nani, Mahene alihojiwa na akakiri mbele ya wenzie kama sita ( 6 ) hivi na sahihi aliweka. Sibahatishi, naujua hu mgogoro vizuri sana kuliko unavyo dhani, namfahamu huyo "msemaji wake" wa sasa bwana Lesilwa, nawafahamu kina Majembe wa Geita, namjua Kazeba wa Mwanza, ninamfahamu vizuri sana yule mzee wa Mbeya waliye mvika kofia na ninamfahamu sana mchungaji mmoja wa Dar ambaye anachezesha hi match, ni mtu fulani maarufu so i know, sibahatishi, ni vile tu mengine huwezi yaandika humu cause bado hao ni watumishi wa Mungu. Narudia, mtu unae jiita Mkristo kua upande wa WAZINZI ni upumbavu, nawaonea huruma wanao toa sadaka kwenye makanisa ya kina Majembe wa Geita nk
 
Wasukuma sijui wana shida gani na masuala ya elimu; mwaka 2006 nilikua Mwanza, mwaka 2005 walifanya uchaguzi wa viongozi wao wa jimbo, walimchagua mzee mmoja hivi anaishi mitaa ya Bugando, simkumbuki jina lake but nadhani yule mzee ni mwenyeji wa mkoa wa Mara, ni kabila moja na mwl Nyerere if i am not mistaken, kuna mchungaji mmoja alikua anapiga friend match na wadada, huyu askofu akamuwajibisha; huyo mchungaji nae alikua msukuma but kabla ya hiyo adhabu kutolewa, huyo Mzanaki wa watu alikua amewajengea imani wachungaji wenzie kwamba lazima tujenge shule ya sekondari sisi kama jimbo, wakanunua kiwanja mitaa ya Buhongwa kule; baada sasa kumuwajibisha huyu mchungaji ambaye alikua anazini zini hovyo na wanawake, Wasukuma wenzie wakamshtaki kwa mzee Kulola, mzee kulola sijui alidanganywa nini kumuhusu huyu Mzanaki, mzee akamnyang'anya uongozi, Mwanza ikazimika; nakumbuka walifanyaga mkutano pale Furahisha, Mzee Kulola ndio muhubiri, mkutano ulikua mgumu sana, makanisa yalikua yana mtazamo tofauti juu ya hatua alizozichukua mzee Kulola dhidi ya yule Mzanaki wa watu; mwishoni yule mchungaji aliyetengwa akakutwa kaachana kabisa na mambo ya Imani, but moja kati ya shutuma alizopewa huyu Mzanaki ni kwamba eti anaachangisha ili wajenge shule, mradi wa shule ukafia hapo; nashangaa tena wamewashtaki kina Mwakipesile kwa issue ya shule tena; Wasukuma mna aleji na ELIMU!?
Yule mzee anaitwa Mchungaji Kuguru,kama namuona vile na Toyota Hilux yake chakavu ya buluu
 
Mkuu, jibu hili; Happiness na umri wa miaka mingapi na mzee alianza lini kua mchungaji Bugando? Tunaongea kwa data. Kwani ile kesi pia aliofungua mahakama ya hakimu mkazi Mwanza iliishaje? Na by the way, wapi nimezungumzia habari ya mzee kuzaa nje ya ndoa? Si unaona unavyo jichanganya? Well, nimekupa homewhork pale juu, nitajie walau wachungaji 20 wanao muunga mkono Mahene ambao walau wana form four ya darasani; tatizo almost wote pale hawana shule kabisa,darsa la saba na wengine darasa la nne na wengine hawaujui mlango wa darasa and hence ufahamu wao wa kawaida tu hawana kabisa; kwa taarifa yako, nimefanya mazungumzo na baadhi yao; wanadhani mtu akienda kushtaki tu hua wanajua tayari kashinda kesi, very stupid ideas kwa watu wanachunga makanisa kua na ufahamu mdogo kiasi hicho.
Ukiendelea kubisha ntakwambia hata aliyemfahamisha huyo Mnyakyusa habari za Mahene kua na nyumba ndogo alikua nani, Mahene alihojiwa na akakiri mbele ya wenzie kama sita ( 6 ) hivi na sahihi aliweka. Sibahatishi, naujua hu mgogoro vizuri sana kuliko unavyo dhani, namfahamu huyo "msemaji wake" wa sasa bwana Lesilwa, nawafahamu kina Majembe wa Geita, namjua KAzeba wa Mwanza, ninamfahamu vizuri sana yule mzee wa Mbeya waliye mvika kofia na ninamfahamu sana mchungaji mmoja wa Dar ambaye anachezesha hi match, ni mtu fulani maarufu so i know, sibahatishi, ni vile tu mengine huwezi yaandika humu cause bado hao ni watumishi wa Mungu. Narudia, mtu unae jiita Mkristo kua upande wa WAZINZI ni upumbavu, nawaonea huruma wanao toa sadaka kwenye makanisa ya kina Majembe wa Geita nk

Mkuu Mazindu Msambule salam kwako. Naomba ikupendeza utupatie Upadate za mgogoro husika. Mimi ni mojawapo wa waliomjua Kristo kupitia mikutano ya mzee Askofu Kulola na pia ni mojawapo ya wanafunzi wa mwl Askofu Lazaro. Sifurahishwi na jinsi Viongozi wetu wa sasa wanavyobomoa misingi iliyowekwa na wazee wetu.

Ahsante
 
VIONGOZI WAKUU WA KANISA LA EVANGELICAL ASSEMBLESS OF GOD OF TANZANIA [E.A.G.T] AKIWEMO ASKOFU MKUU WACHUNGUZWA KWA RUSHWA

Ndugu WanaHabari,

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU – Brig Jen. John Mbungo, napenda kuujulisha Umma kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU – Makao Makuu, inafanyia uchunguzi malalamiko dhidi ya Viongozi Wakuu wa Kanisa la EVANGELICAL ASSEMBLESS OF GOD OF TANZANIA (E. A.G.T) nchini.

Bila shaka baadhi yenu mlisikia na kuona malalamiko ya baadhi ya wachungaji wa kanisa la EAGT ambao waliyatoa siyo tu kwenye vyombo vya habari lakini pia katika ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU.

Wachungaji hao, ambao kwa ujumla wao ni zaidi ya 540, kwa pamoja wanalalamikia vitendo vya Rushwa, Ufisadi pamoja na wizi ndani ya kanisa yakiwemo mambo yafuatayo;
  1. Uingizwaji wa vyombo vya moto yakiwemo magari zaidi ya 50 na pikipiki kwa jina la Kanisa la EAGT, vyombo ambavyo inadaiwa viliingizwa nchini kwa kupitia jina la kanisa na kupata msamaha wa kodi lakini vyombo hivyo vya moto - kanisa halivitambui na wala halijawahi kuvipokea.
  2. Lalamiko jingine ni ubadhirifu wa fedha na mali ya kanisa unaodaiwa kufanywa na viongozi wa kanisa hilo kuhusiana na mkataba ulioingiwa kati ya kanisa la EAGT na wapangaji wa Duka la IMALASEKO SUPERMARKET INVESTMENT kwani inadaiwa mapato yanayotokana na majengo hayo hayajawekwa wazi hivyo kuashiria kuwepo kwa ubadhirifu.
  3. Ubadhirifu wa fedha za kanisa kwenye ununuzi wa shule iitwayo OASIS EDUCATION AND COMMUNITY DEVELOPMENT iliyopo Kahama.
  4. Kuwepo kwa TIN tofauti zaidi ya tano zilizosajiliwa kwa jina la Kanisa la EAGT na TIN hizo kutumika kuingiza magari kwa jina la kanisa na kusamehewa kulipa ushuru wa Forodha wakati magari hayo hayajanunuliwa na kanisa.
  5. Taarifa za mapato na matumizi ya kanisa kutokuwekwa wazi wala Kanisa halina Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.
  6. Uingiaji wa mikataba mibovu na isiyo wazi inayoikosesha Serikali mapato yake halali.

Ndugu WanaHabari,

Kupitia taarifa hii tunapenda umma ufahamu kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Makao Makuu ilishaanza kufanyia uchunguzi malalamiko haya ambayo baadhi ya tuhuma zinaangukia chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 na kwamba mpaka sasa yafuatayo yameshafanyika:
  • Tumeshafanya mahojiano na baadhi ya walalamikaji,
  • Tumekusanya baadhi ya vielelezo na
  • Tunaendela kuwaita na kuwahoji walalamikiwa na leo hii Februari 16, 2021 tumemhoji Askofu Mkuu wa Kanisa hilo – Askofu ABEL MWAKIPESILE.
Ndugu WanaHabari,

Lengo la uchunguzi wetu huu pamoja na mambo mengine ni kutaka kufahamu ukweli wa malalamiko haya ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
IMETOLEWA NA DOREEN J. KAPWANI
AFISA UHUSIANO WA TAKUKURU
KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
Zile Trilion 1.5 zenyewe walichunguza?
 
Usipotoshe!! Assemblies of God mission toka Marekani ndio ndio waanzilishi wa kanisa hilo hapa nchini. Baada ya kuwa kazi ya Mungu wameifikisha mahali ambapo wenyeji wanaweza kuiendesha na kuisimamia, walikabidhi kanisa hilo rasmi kwa wenyeji chini ya kanisa lililosajiliwa la TAG na chini ya Askofu wa kwanza mwenyeji Askofu Emmanuel Lazaro kwenye miaka ya sitini. Viwanja vyote na majengo yote wakamilikishwa TAG, na wammisionary wakaachana na mambo ya uongozi wakajikita na umisheni tu. Ndivyo ilivyokuwa mpaka miaka ya themanini mwanzoni wakati mgogoro ulipoana kufukuta kwa chini chini. Mwishoni mwa miaka ya themanini uasi ulipokomaa aliyekuwa makamu wa Askofu mkuu akajitangaza kuwa ndiye Askofu mkuu wa TAG wakati Askofu mkuu aliyechaguliwa kikatiba bado yupo na muda wake haujaisha!! Hivyo kulikuwa na kanisa moja na maaskofu wakuu wawili, Yule aliyejiweka mwenyewe na akapata baadhi ya wachungaji waliomuunga mkono na Yule aliyechaguliwa kikatiba na wapo wachungaji wengi tu ambao hawakuchukuliwa na uasi waliendelea kumuunga mkono. Kipindi hicho serikali ulikuwa imepiga marufuku usajili wa mashirika mapya ya kidini.
Baadaye miaka ya tisini serikali iliruhusu tena usajili wa mashirika ya kidini hapo ndipo kundi lililoasi TAG likapata mwanya wa kusajili kanisa la EAGT. Kumbuka kabla ya uasi walikuwa wanatumia majengo na viwanja vya TAG ilivyokabidhiwa na Assemblies of God mission ya Marekani na TAG ndiyo yenye hati ya hivyo viwanja. Baada ya uasi waliendelea kutumia majengo na viwanja hivyo hivyo! Hayo makanisa na viwanja waliving'ang'ania mpaka kesho japo hati miliki hawana!! Mfano wa kanisa moja la hivyo ni EAGT Temeke!
Yote kwa yote adui katika sakata lote hili ni shetani Wala siyo mwanadamu! Anachoshangaa shetani Ni kuwa kote huko TAG na EAGT Kuna maelfu ya watu waliookoka!! La muhimu kwa washirika Ni kutokujiingiza kwenye migogoro ya kiuongozi na kubaki kuwaombea viongozi wao ili wasimame imara. Wakristo waliojiingiza kwenye migogoro ya kiuongozi wengi walikufa kiroho! na viongozi bado wanaendelea kumtumikia Mungu maana Mungu anawasaidia katika majaribu yao. Lakini wewe mkristo ukijiingiza katika jaribu lisilokuhusu ( la viongozi) yawezekana usipate neema ya kukushindia!!!
Ubarikiwe sana mtumishi
 
Mgogoro wa Kulola na TAG umetokea kipindi cha pili cha utawala wa Mwinyi (baada ya 1990), na Kulola kuanzisha EAGT 1992. Serikali ya Nyerere inaingiaje hapo?!
Ndugu yangu mgogoro huu ni wa miaka mingi sana toka 1980. Huo ulikuwa wakati wa Rais Nyerere
 
Wachungaji wengi wanaolalamika ni wa kanda ya ziwa, wasukuma.

Hao wachungaji ni wanafiki, mbona hawakusema toka zamani kuna ubadhirifu mkubwa kanisani hadi wagombane kwenye vyeo ndio waje kusema kuna TIN tano sijui ujinga gani, kama wao ni waadilifu na waaminifu mbona hawakusema mapema hilo hadi mgogoro wa uongozi utokee ndio walalamike?

Binafsi sio muumini wa dini yoyote maana najua Mungu hayupo ingawa nina historia ama najua historia pana ya makanisa na madhehebu mbalimbali hapa Tanzania.

EAGT ndio kwanza wamefugua milango ya migogoro, wanarudi kule kule kwa muasisi wao Kulola alipoanzisha mgogoro na TAG akahama kanisa na kung'ang'ania majengo ya TAG, wanaelekea kule kule.

Halafu TAKUKURU mbona waislamu wanailalamikia bakwata kila uchwao hatijawahi kusikia viongozi wa bakwata wamehojiwa?
Una hakika kwamba wote ni wasukuma ?
 
Back
Top Bottom