TAKUKURU: Askofu na Viongozi Wakuu wa Kanisa la Avengelical assembless of God (EAGT) wachungunzwa kwa rushwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,805
11,965
VIONGOZI WAKUU WA KANISA LA EVANGELICAL ASSEMBLESS OF GOD OF TANZANIA [E.A.G.T] AKIWEMO ASKOFU MKUU WACHUNGUZWA KWA RUSHWA

Ndugu WanaHabari,

Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU – Brig Jen. John Mbungo, napenda kuujulisha Umma kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU – Makao Makuu, inafanyia uchunguzi malalamiko dhidi ya Viongozi Wakuu wa Kanisa la EVANGELICAL ASSEMBLESS OF GOD OF TANZANIA (E. A.G.T) nchini.

Bila shaka baadhi yenu mlisikia na kuona malalamiko ya baadhi ya wachungaji wa kanisa la EAGT ambao waliyatoa siyo tu kwenye vyombo vya habari lakini pia katika ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU.

Wachungaji hao, ambao kwa ujumla wao ni zaidi ya 540, kwa pamoja wanalalamikia vitendo vya Rushwa, Ufisadi pamoja na wizi ndani ya kanisa yakiwemo mambo yafuatayo;
  1. Uingizwaji wa vyombo vya moto yakiwemo magari zaidi ya 50 na pikipiki kwa jina la Kanisa la EAGT, vyombo ambavyo inadaiwa viliingizwa nchini kwa kupitia jina la kanisa na kupata msamaha wa kodi lakini vyombo hivyo vya moto - kanisa halivitambui na wala halijawahi kuvipokea.
  2. Lalamiko jingine ni ubadhirifu wa fedha na mali ya kanisa unaodaiwa kufanywa na viongozi wa kanisa hilo kuhusiana na mkataba ulioingiwa kati ya kanisa la EAGT na wapangaji wa Duka la IMALASEKO SUPERMARKET INVESTMENT kwani inadaiwa mapato yanayotokana na majengo hayo hayajawekwa wazi hivyo kuashiria kuwepo kwa ubadhirifu.
  3. Ubadhirifu wa fedha za kanisa kwenye ununuzi wa shule iitwayo OASIS EDUCATION AND COMMUNITY DEVELOPMENT iliyopo Kahama.
  4. Kuwepo kwa TIN tofauti zaidi ya tano zilizosajiliwa kwa jina la Kanisa la EAGT na TIN hizo kutumika kuingiza magari kwa jina la kanisa na kusamehewa kulipa ushuru wa Forodha wakati magari hayo hayajanunuliwa na kanisa.
  5. Taarifa za mapato na matumizi ya kanisa kutokuwekwa wazi wala Kanisa halina Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.
  6. Uingiaji wa mikataba mibovu na isiyo wazi inayoikosesha Serikali mapato yake halali.

Ndugu WanaHabari,

Kupitia taarifa hii tunapenda umma ufahamu kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa – TAKUKURU Makao Makuu ilishaanza kufanyia uchunguzi malalamiko haya ambayo baadhi ya tuhuma zinaangukia chini ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na. 11 ya Mwaka 2007 na kwamba mpaka sasa yafuatayo yameshafanyika:
  • Tumeshafanya mahojiano na baadhi ya walalamikaji,
  • Tumekusanya baadhi ya vielelezo na
  • Tunaendela kuwaita na kuwahoji walalamikiwa na leo hii Februari 16, 2021 tumemhoji Askofu Mkuu wa Kanisa hilo – Askofu ABEL MWAKIPESILE.
Ndugu WanaHabari,

Lengo la uchunguzi wetu huu pamoja na mambo mengine ni kutaka kufahamu ukweli wa malalamiko haya ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
IMETOLEWA NA DOREEN J. KAPWANI
AFISA UHUSIANO WA TAKUKURU
KWA NIABA YA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU
 

Attachments

  • 1613490292140_FINAL EAGT PRESS RELEASE .doc
    133.5 KB · Views: 41
Wachungaji wengi wanaolalamika ni wa kanda ya ziwa, wasukuma.

Hao wachungaji ni wanafiki, mbona hawakusema toka zamani kuna ubadhirifu mkubwa kanisani hadi wagombane kwenye vyeo ndio waje kusema kuna TIN tano sijui ujinga gani, kama wao ni waadilifu na waaminifu mbona hawakusema mapema hilo hadi mgogoro wa uongozi utokee ndio walalamike?

Binafsi sio muumini wa dini yoyote maana najua Mungu hayupo ingawa nina historia ama najua historia pana ya makanisa na madhehebu mbalimbali hapa Tanzania.

EAGT ndio kwanza wamefugua milango ya migogoro, wanarudi kule kule kwa muasisi wao Kulola alipoanzisha mgogoro na TAG akahama kanisa na kung'ang'ania majengo ya TAG, wanaelekea kule kule.

Halafu TAKUKURU mbona waislamu wanailalamikia bakwata kila uchwao hatijawahi kusikia viongozi wa bakwata wamehojiwa?
 
Makanisa ya kilokole ni ya wenye dhambi na ili uingie humo unatubu na kusema dhambi zako. .. Hivyo mambo ya wizi ni kawaida
 
Siyo hao. Lakini hawa ni wevi. Nadhani tokea walipopora mali za TAG kupitia Moses Kulola ambaye serikali za Nyerere na JK zilimpendelea.
I'm curious na huo uporaji mkuu

Kuna uzi wowote unazungumzia hiyo historia niutafute?
 
Siyo hao. Lakini hawa ni wevi. Nadhani tokea walipopora mali za TAG kupitia Moses Kulola ambaye serikali za Nyerere na JK zilimpendelea.
Mgogoro wa Kulola na TAG umetokea kipindi cha pili cha utawala wa Mwinyi (baada ya 1990), na Kulola kuanzisha EAGT 1992. Serikali ya Nyerere inaingiaje hapo?!
 
Back
Top Bottom