TAKUKURU angalieni na hili Waziri Lugola maliza sakata la Lugumi

Kikelelwa

Senior Member
Dec 14, 2010
176
124
Ni miaka miwili na nusu sasa tangu Watanzania walipoanza kusikia kuhusu sakata la Kampuni ya Lugumi Enterprises
kushindwa kufunga vifaa vya kuchukulia alama za vidole kwenye vituo 108 vya Polisi, kama mkataba wa kampuni hiyo na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ulivyotaka.

Jambo hilo liliibuliwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof.Juma Assad, katika taarifa yake ya ukaguzi ya mwaka wa fedha 2011/2012.

Jambo hilo limewahi kupapaswa na mhimili wa Bunge na kutoa maelekezo kwa Serikali kulifanyia kazi tangu Agosti 2016, mpaka leo hakuna kilichofanyika. Katika kipindi cha miaka miwili na nusu ya utawala wa Rais John Magufuli, mawaziri wawili wa Mambo ya Ndani ya Nchi wamepita bila kumaliza mjadala wa sakata hilo. Mawaziri hao ni Charles Kitwanga pamoja

na Dk. Mwigulu Nchemba, ambao kwa nyakati tofauti wameiongoza wizara hiyo,huku sakata la Lugumi likiendelea kufukuta bila kumalizwa, kwa ama jamii kuambiwa hapakuwa na jambo lolote ama wahusika kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Sakata hilo limeibuliwa upya Julai 2, mwaka huu na Rais John Magufuli, baada ya kumwapisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola. Wiki kadhaa baadaye waziri huyo ameonyesha kuhitaji kukutana na mmliki wa Kampuni ya Lugumi Enterprises, Said Lugumi.

Ni matumaini yetu kwamba mkutano huo utakuwa ni wenye manufaa kwa pande zote; mosi, kuhakikisha teknolojia hiyo ya alama za vidole inafungwa katika vituo vyote ili kukidhi matarajio ya kununua teknolojia hiyo, lakini kama kumekuwa na ulaghai ni wakati sahihi hatua stahiki zikachukuliwa kwa masilahi mapama ya Tanzania.

Kitendo cha Said Lugumi, ambaye ndiye mmiliki wa Kampuni ya Lugumi Enterprises, kusema yuko tayari kukutana na waziri katika mazingira yoyote yatakayoonekana yanafaa, ni mwanzo mzuri katika kuelekea kukamilisha na kufunga kabisa mjadala huo.

Rai yetu kwa Waziri Lugola ni kuhakikisha sakata hilo analishughulikia na kulimalizakwa uwazi kama ambavyo ameahidi katika mkutano wake na wanahabari. Lakini pia wananchi wanasubiri kuona kama yeye atakuwa tofauti na watangulizi wake, ambao sakata hilo lilikuwa sawa na mfupa mgumu usiolika.
 
Lugumi alipewa kazi ya kumnyamazisha Mange Kimambi.

Baada ya kufanikiwa hiyo kazi na kesi yake imekufa kifo cha mende ndio maana hata juzi kati wakati Zungulee anapaishwa mpaishhaji akutaja issue za Lingumi aaha Lugumi
 
Back
Top Bottom