Tajiri Nambari Moja Duniani Atua Arusha Kimyakimya

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Tajiri Nambari Moja Duniani Atua Arusha Kimyakimya

TAJIRI namba moja duniani, Bw. Mukesh Ambani (53) (pichani) raia wa India amewasili nchini jana alfajiri kimyakimya kwa safari ya
kitalii.
Tajiri huyo aliwasili jana saa 10.15 alifajiri Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) akiwa na ndege nne binafsi akifuatana na wafanyabiashara wakubwa zaidi ya 50.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na mmoja wa waratibu wa safari hiyo hapa nchini, Bw. Godfrey Famandes zimeeleza kuwa lengo la safari yake ni kutembelea hifadhi za taifa, hususan Hifadhi ya Serengeti.

Bw. Ambani kwa mujibu wa mitandao mbalimbali ya kimataifa ndiye tajiri namba moja akimiliki dola za Marekani bilioni 63.2 (zaidi ya sh. trilioni 90), akifuatiwa na Carlos Slim Helu kutoka Mexico mwenye dola za Kimarekani bilioni 62.2993 na Mmarekani William Bill Gates akifuatia kwa karibu akimiliki dola za Marekani bilioni 62.29.

Katika kundi hilo dogo la matajiri watano duniani nafasi ya nne inashikiliwa na Warren Buffett kutoka Mexico ambaye anamiliki dola 55.9 na kufuatiwa na Lakshmi Mittal wa India mwenye kitita cha dola bilioni 50.9.Akizungumza na njia ya simu jana, Bw. Famendes ambaye ni Mkuu wa Oparesheni wa Kampuni ya Gapco Tanzania ambaye pia ndiye msemaji wa kampuni hiyo na mwenyeji wa
tajiri huyo, alikiri kuwasili kwa tajiri huyo na kusita kuzungumzia safari hiyo zaidi.
Safari yenyewe ni ya binafsi zaidi, hivyo sina cha kukueleza zaidi ya kukuthibitishia kuwa ni kweli amewasili…sina uhakika na idadi ya wafanyabiashara aliofuatana nao,� alisema Bw. Famendes kwa njia ya simu.

Habari zaidi kuhusiana na safari hiyo zimeeleza kuwa tajiri huyo pamoja na wenzake wamewasili Hifadhi ya Serengeti, ambayo ina hadhi ya urithi wa dunia, na tayari jana walifanya mzunguko wa kwanza wa kutembelea hifadhi hiyo na kujionea maajabu ya dunia ya hifadhi hiyo.
Kuja kwa mfanyabiashara huyo na wenzake na fahari kubwa kwa Tanzania, kwani ni kielelezo kuwa tayari dunia imeanza kujua vivutio tulivyo navyo, nchini na umuhimu wake duniani, alisema mmoja wa wakurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) huku akisizitiza kuwa hana habari lakini akiahidi kufuatilia ujio huo.

Bw. Ambani alizaliwa Aprili 19 mwaka 1957, huko Aden (Colony of Eden) sasa Yemen akiwa na uraia wa India. Kwa sasa anaishi Antilia, Mumbai Maharashtra na mke wake Nita Ambani, wakiwa na watoto watatu, Akash, Anant na Isha

Alisoma Chuo Kikuu cha Mumbai na baadaye Stanford, Uingereza. Kwa sasa ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reliance Industries chini ya Ambani Group of Campanies.
(Chanzo:Gazeti Majira)
 
Hapo kwenye bold hapo....kuna ukweli?
 
Mbona in Forbes Mukesh Amabani ni tajiri no 4? Hawa majira vp? Source zao zipi?
 
Majira wanatumia source gani? Uandishi wa Tanzania bana....
 
Doh Warren Buffet wa Mexico!! Hii hatari kweli!
Anyway according to Forbes list ni kama ifuatavyo.
1.Carlos Slim Helú
2.William Gates III
3.Warren Buffett
4.Mukesh Ambani
5.Lakshmi Mittal
6.Lawrence Ellison
7.Bernard Arnault
8.Eike Batista
9.Amancio Ortega
10.Karl Albrecht
 
KUTOKA WIKIPEDIA

Mukesh Dhirubhai Ambani (born on 19 April 1957) is an Indian business magnate and the chairman and managing director of Reliance Industries,[4] the largest private sector enterprise in India, a Fortune 500 company,[5] and one of the largest private sector conglomerates in the world. His personal stake in Reliance Industries is 48%.[6]

As of July 2010, he is the richest man in Asia[7] and the fourth richest man in the world with a personal wealth of US$29.0 billion.
On 29 October 2007, a strong rally in the Indian stock market and the appreciation of the Indian rupee boosted the market capitalisation of all Reliance group companies, making him for a while the world's richest man,[8] with net worth climbing to US$63.2 billion leaving Bill Gates behind at around $56 billion.[9][10] According to Forbes Magazine forecasts, he is expected to regain the title of the richest man in the world in 2014.[11][12]

Doh Warren Buffet wa Mexico!! Hii hatari kweli!
Anyway according to Forbes list ni kama ifuatavyo.
1.Carlos Slim Helú
2.William Gates III
3.Warren Buffett
4.Mukesh Ambani
5.Lakshmi Mittal
6.Lawrence Ellison
7.Bernard Arnault
8.Eike Batista
9.Amancio Ortega
10.Karl Albrecht
hata mimi naweza kuja na list yangu ila inategemea ww umeangalia mwaka gani na vigezo
 
Jambo la muhimu hapa ni kwamba kwa kuja kutalii nchini mwetu atachangia katika pato la taifa litokanalo na utalii. Hiyo ndio issue
 
Alisoma Chuo Kikuu cha Mumbai na baadaye Stanford, Uingereza. Kwa sasa ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Reliance Industries chini ya Ambani Group of Campanies.

Jamani Editor should be sacked, toka lini Stanford iko Uingereza, na huyo jamaa ni dropout!
 
Jambo la muhimu hapa ni kwamba kwa kuja kutalii nchini mwetu atachangia katika pato la taifa litokanalo na utalii. Hiyo ndio issue

Tuna system chafu hapa Tanzania unaweza kukuta anapewa offer ya kutembelea mbuga bure
 
Hivi hajauziwa hata kiwanja kweli maana kwa dili izo chama cha mafisadi ndo wenyewe !
kama c kiwanja lazma kajibebea hata mbuni !
ndo taifa letu !
 
Back
Top Bottom