Tajiri wa Kesho: Mchakato wa Mafanikio

Tajiri wa Kesho: Mchakato wa Mafanikio

Dr Arshavin

Member
Joined
May 14, 2024
Posts
26
Reaction score
78
TAJIRI WA KESHO YUKO KWENYE MCHAKATO LEO!

Usifikirie uko nyuma fikiri uko njiani.
Kila hatua unayoichukua leo ni tofauti kati ya wewe wa sasa na tajiri utakayekuwa kesho.

Mchakato Unauma Lakini Unabadilisha
Mohammed Dewji leo anaitwa bilionea mdogo zaidi Afrika.
Lakini kabla ya hapo alifanya kazi ya kujisomea biashara,akashindwa, akajaribu tena.
Hakuna aliyempa taji alipigana nalo.
Uchungu wa leo ni nguvu ya kesho.

Kujifunza Ni Silaha Si Starehe
Reginald Mengi mwanzoni hakuwa na chochote. Alianza kufanya kazi kwa wengine, akajifunza kila siku, akafungua IPP Media, akajenga milki kubwa Tanzania. Aliacha ulimwengu ukimkumbuka.
Tajiri wa kesho anasoma leo wakati wengine wanalala.

Anza Kidogo Ukue Kubwa
Said Bakhresa alianza na mkokoteni wa mkate mdogo Zanzibar.
Leo Azam Group inasimama imara Afrika Mashariki vyakula, maji, televisheni na zaidi.

Hakuanza kwa milioni alianza kwa ujasiri.
Usidharau mwanzo wako mdogo ndio mzizi wa mti mkubwa.

Thamani Yako Ni Mtaji Wako
Diamond Platnumz hakuanza studio kubwa.Alianza kwa ndoto, kipaji na nidhamu ya kufanya kazi bila kuchoka.
Leo ana WCB Wasafi, biashara za kimataifa na jina linalofahamika duniani kote.

Ujuzi wako wa leo ni dhahabu usiyoijua bado.

Subira Ni Sehemu Ya Mchakato
Hakuna tajiri aliyeamka tajiri usiku mmoja.

Wote walipitia usiku wa giza, mashaka na muda wa kutojua jibu. Tofauti yao ni moja tu hawakuacha.
Ukiendelea tayari unashinda wengi walioacha njiani.

Tajiri wa kesho sio mtu mwingine
NI WEWE ukiendelea leo bila kukata tamaa!

Mchakato si adhabu ni bei ya maisha unayoyastahili.
Endelea.

Jifunze.

Wekeza.

Subiri.

Shinda.
 
Back
Top Bottom