Kwa sasa wewe hakikisha tu kwamba una mahitaji yale ya msingi kabisa, chakula na malazi. Usihangaike kuwa na kila kitu kama ilivyokuwa siku za kawaida. Ukishaweza kuwa na chakula na familia yako basi, kaa kimya na kuchukua tahadhari kubwa mno dhidi ya ugonjwa. La sivyo utapata ugonjwa na ndani ya wiki 2 utakuwa umekufa. Usiangalie eti biashara imeyumba, nakwambia bado hakijayumba kitu subiri utaona kuanzia mwezi wa 6 utatafuta ugali tu na ukipata utashukuru Mungu. Hivyo usilalamike hili ni janga fanya ya msingi tu na kujilinda usipate ugonjwa manake ukipata ndio mbaya kuliko chochote kwa sasa.