Taji Liundi avunja ukimya kuhusu COVID-19

Taji Liundi avunja ukimya kuhusu COVID-19

Anaandika Taji Liundi

AKIBA INAISHA.
Tunaingia mwezi wa pili sasa baadhi yetu kwenye sekta binafsi/wajasiriamali hatujafanya kazi.
Mimi ni Mshereheshaji.
Djs wangu hawajafanya kazi
Kumbi zimefungwa zote
Watengeneza cake
Wapambaji wengi wanalalamika sana.
Event Planners wanakosa kazi.
Hadi caterers wakubwa wanalia.

Nikipima mbele, napatwa hofu kwamba May na June pia zitapita tupu. Labda July na August pia. Kiufupi 2020 imeharibika kabisa.
Sikujiandaa.
Nisingeweza kujiandaa kabisa na janga hili.

*Mahitaji ya maisha hayakomi, yanaendelea. Kodi. Chakula. Matibabu.
*Najitahidi sana, mpaka sio kawaida kubana matumizi. Lakini bidhaa nyingi zimeongezeka sana bei.

Najiuliza nitafanya nini nikibaki na tuseme 300.000/ May katikati.
Nitamkopa nani?
Nitakopa wapi?

Na marafiki wengi ambao tayari wananiomba hata 30.000/ wadundulize?
Natoaje ikiwa na mimi sina mfuko mrefu?

Wewe ungefanya nini?
Nasoma nje kuhusu stimulus package ya $400/600 kwa mwezi kwa miezi 6 na jinsi waMarekani wanahaha kuipata!

Tunaona kote duniani watu wanapinga kufungwa kwa biashara. Watu wanakaidi. Wanaasi.
Hapa Dar, ukipanda Boda na Bajaj na Uber ndo utasikia malalamiko.
Ukienda sokoni au dukani. Ukienda Mlimani na kujikuta peke yako corridor nzima.

Tufanyeje?
Tutoke turisk?
Tukae bila ajira tufilisike?

Ndio maana nataka kuona takwimu za kweli.
Kila siku.

Ni namna moja ya kupima tulipo. Mafanikio ya kupunguza maambukizi. Inajenga moyo wa kwamba kuna siku maisha yatarejea kama kawaida.

Nimeshabana mkanda mpaka sipumui.
Tupeane ushauri.
Hapo ni partial lockdown ,tukiingia total lockdown tutatafutana.
 
Mkuu hata uendelee miaka miwili as long kwamba nafanya kazi na naingiza mapato nakosaje mshahara?? sio kwamba natamani ugonjwa uendelee, HAPANA! Ila Dharau zao kwetu watumishi wa Umma zikome kabisa
Hata mtumishi wa umma mwenye mshahara bado anamtegemea mjasiriamali na watu wengine wa sekta binafsi.

Hali ikiendelea hivi hata huu mshahara hautakuwa na Msaada tena maana huenda ukakosa bidhaa ya kununua.

Utakula hela?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole Taji, hali ni mbaya kote, walimu shule binafsi tumepewa likizo bila malipo, hata mshahara wa April hatujapewa, bora wewe una laki 3 ndani...... Ummy tunakupenda na kukuombea kila siku tunaomba takwimu tujue tuko wapi
Zitto alishauri serikali itoe Stimulus Packages ya Shilingi laki 3 kwa mwezi kwa kila familia!! Wadau wameshauri NSSF/PPF watoe mafao kwa wafanyakazi walioapata redundancy,waliopata likizo bila malipo etc kutokana na corona !! Serikali ina midege minane huku wakiwa na ventilator moja TZ nzima tena wamenunua juzi ni aibu.
 
Hawa ndio waliongoza kutudharau Watumishi wa Umma kwamba tunaishije na mishahara kidoogo na madeni kibao? Iendelee kidogo tusheshimiane, shenzytpe!!
Lini alikudhadarau? Halafu ulivyo mtupu unafikiri uchumi ukisimama kabisa mshahara wa wewe kulipwa utadondoka kama manna toka mbinguni? No wonder hukuwa na akili za kujiajiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ombea corona ipite nakuhakikishia Huwezi kupata mshahara km hali itaendelea hivi

Nikustue ujipange usije ukawa unatapanya mali
Mkuu Bia yetu,kwani kuchapa kazi kumesimama lini mpaka akose mshahara? Au na ninyi CCM mmeanza uvivu?
 
hii corona mwaka huu tutaheshimiana asee. masikini na matajiri tutatoka ngoma droo.hakuna kupanda ndege wala kwenda wapi ni mguu kwa mguu mpaka tutakapo komea

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo maana Magufuli na CCM hawataki itajwe kabisa maana inawasaidia kuongeza kasi ya kuwafanya watanzania wengi waishi Kama mashetani
 
Hawa ndio waliongoza kutudharau Watumishi wa Umma kwamba tunaishije na mishahara kidoogo na madeni kibao? Iendelee kidogo tusheshimiane, shenzytpe!!
Fikiria mara mbili kabla ya kuandika.
Unafikiri serikali itaweza kulipa watumishi wa umma mishahara yao kamili siku za usoni kama hali itaendelea hivi hadi mwezi wa sita na wa saba?

Tafakari!!
 
Fikiria mara mbili kabla ya kuandika.
Unafikiri serikali itaweza kulipa watumishi wa umma mishahara yao kamili siku za usoni kama hali itaendelea hivi hadi mwezi wa sita na wa saba?

Tafakari!!
We tafakari tena Mkuu kuna shughuli gani za serilaki zimesimama hadi leo? au kwakuwa upo nyuma ya keyboard basi unajitutumua?
 
Back
Top Bottom